Monday 27 January 2014

MBUNGE WA JIMBO LA BUKOBA MJINI KAGASHEKI AKUTANA NA MABALOZI WA NYUMBA KUMI ZAIDI YA 800 WA JIMBO LAKE LOTE

 Mbunge wa jimbo la Bukoba mjini Balozi Khamis Sued Kagasheki amekutana  na mabalozi  wa nyumba kumi  wa  kata zote 14 ,Balozi kagasheki  amesema anawathamini sana na ndio maana aliweka utaratibu wa kukutana nao kila mwaka kwa mara moja au mbili. Mh Kagasheki baada ya kueleza kwa kirefu kwa kutokuwepo vikao mbalimbali vya madiwani katika manispaa ya Bukoba kufuatia migogoro ndani ya manispaa hiyo,amewataka  Mabalozi kusaidia kuleta hali ya maelewano katika maeneo wanayoishi na kumaliza tofauti zilizokuwepo na sasa kuwa kitu kimoja kwa masilahi ya chama na wananchi wote kwa ujumla.
 Ni Mabalozi wakiwa katika ukumbi wa lina's
 Mzee Kaizirege akiwa na Ma Yustina
 Mwenyekiti wa wilaya ccm Yusuf Ngaiza akiongea na Mabalozi wa nyumba kumi jimbo la Bukoba mjini
 Katibu wa vijana Bukoba Manispaa akiongea na mabalozi
Mh Diwani Mwajabu akiongea na Madiwa kwamba sasa anaomba wawe wamoja yaliyopita wasahau

No comments:

Post a Comment