Friday 16 May 2014

VIWANJA VYA GYMKANA BUKOBA WANAFUNZI WA CHUO CHA SECRETARIAL NA USHONAJI BAKITA WAKIWA KATIKA MICHEZO

 Camera yetu katika viwanja vya Gmkana Bukoba maeneo ya Bukoba club, ni wanafunzi wa chuo cha Bakita kinachotoa mafunzo ya Sekretarial na Ushonaji wakiwa katika kipindi cha michezo,wangine wakiwa nanacheza mpira wa pete na wa wengine wakisakata kabumbu.
 Hawa wakicheza mpira wa pete
 Ni waalimu nao wakifuatilia
 Michezo ni afya , lakini ni ajira pia
 Hawa wakicheza soka, inapendeza sana, Wanawake wanaweza kila kitu
 Huyu akichanjanja mbuga
 Chezeaaa Bakita weweee
 Huyu akakwatuliwa kiatu... yoko hoi mpaka chozi likamtoka.
jamcobukoba.blogspot.com tunawpongeza kwa kujari michezo na hasa soka la wanawake.

Thursday 15 May 2014

CAMERA YETU KIJIJI CHA BUGANDIKA NYUMBANI KWA BWANA KAMUZORA,AKIWA NA MAMA YAKE MZAZI ALIESTAAFU UTUMISHI WA UMMA IDARA YA AFYA

 Bw Kamuzora akiwa na mama yake mzazi anaeishi hapo nyumbani baada ya kustaafu utumishi wa umma na maisha yanaendelea kama mjini kijijini Bugandika.
 Ni nyumbani kwa BwKamuzora kijijini Bugandika
 Ilikuwa ni furaha kukutana na mama yake mzazi aliestaafu utumishi wa umma na sasa anaishi kijijini raha mustarehee
 Mama anaonekana mwenye furaha, tabasamu, si rahisi  kuelewa kama ni mama mstaafu katika idara ya afya na sasa yuko kijijini anaendelea na maisha, tumekuwa  tukiwaona watu wengi wanapostaafu kazi  maisha yana badilika na kupoteza mwerekeo, na wengi hukataa kurudi vijijini na kukatalia mijini kwa sababu  ya kutojipanga, mama huyu ni mfano mzuri wa kuigwa
 Iliweza kutueleza maisha yake ya kila siku na kusema maisha ya hapo kijijini ni mazuri sana , maana kila anachohitaji anakipata, miundo mbinu ya umeme hipo, hivyo anaweza kuweka, kuifadhi vyakula kwenye Friji, anapata habari zote za dunia kwa kutumia Tv, hivyo maisha mazuri ambayo angepata akiwa mjini anayapata akiwa Bugandika
 Bw Bushira akiwa na mama
 Ni utamaduni wa kihaya unapofika nyumbani kwa mtu unakarbibishwa kwa  kupewa kahawa ya kutafuna(akamwani)
 Hii ni picha ya baba mzazi wa Kamuzora aliefariki kwenye ajari ya meli ya Mv Bukoba
 Ni eneo la shamba
 Watoto majirani waekurahi na camera yetu
 Maisha yanaendelea  kama mujiniiiii
 Swaiba wake anafika ghafla nyumbani kwake
 Furahaaaa
 Bw Denis akiwa na Bw Bushira
Ongera mama mstaafu kwa kujiandaa vizuri, ni mfano wa kuigwa na wengine

Wednesday 14 May 2014

MVUA ILIYONYESHA JIJINI DAR JANA ILIVYOWATESA MADEREVA WA BAJAJI MIKOCHENI


 Dereva wa Bajaji yenye namba za usajili T 920 CMC, ambaye hakuweza kufahamika jina lake mara moja, akijaribu kuikwamua Bajaji yake katika dimbwi la Maji huku ndani akiwa na abiria baada ya kuzimika katikati ya Dimbwi hilo eneo la Mikocheni A, jijini Dar es Salaam, jana kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. Eneo hilo limeharibika vibaya na hasa kutokana na barabara hiyo iliuwa tayari imeanza kukarabatiwa kwa kushindiliwa kifusi cha udongo kwa ajili ya kuwekwa lami, lakini zoezi hilo imeelezwa kutoendelea tena kutokana na mmoja kati ya waliokuwa wakitia msukumo kutengenezwa kwa barabara hiyo kuhama eneo hilo na kufanya ujenzi huo kusimama na kuharibika hadi kusababisha ufumbufu kwa madereva watumiao njia hiyo.
 Dereva wa Bajaji akienelea kuikwamua Bajaji yake kuwanushuru abiria wake wasihadhirike katika dimbwi hilo.
 Hapa akifanikiwa kuikwamua huku mmoja kati ya abiria akipitia kidirishani na kuingia upande wa dereva ili kuongoza bajaji hiyo.
 Moja ya chemba ya maji machafu ikiwa imefurika na kutema maji nje yaliyosababisha kuharibika kwa eneo la barabara hiyo.
 Chemba zikizidi kuzibuka eneo hilo

Tuesday 13 May 2014

JOKATE AWATAKA WAHITIMU WA VYUO VIKUU KUJIAJIRI


 Jokate Mwegelo akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika kongamano la 2014 Market Forum lililofanyika kwenye ukumbi wa Nkrumah. Mrembo na mbunifu wa mitindo huyo aliwataka wanafunzi wajiajiri mara wamalizapo masomo yao kutokana na ugumu wa soko la ajira.
 Jokate Mwegelo akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam iliyoandaa kongamano la 2014 Market Forum lililofanyika kwenye ukumbi wa Nkrumah. Mrembo na mbunifu wa mitindo huyo aliwataka wanafunzi wajiajiri mara wamalizapo masomo yao kutokana na ugumu wa soko la ajira.
Jokate Mwegelo akiwa na mshindi wa shindano la ubunifu, Jacqueline Rimoi ambaye alimzawadia sh, 300,000 kwa kutengeneza tangazo la kunadi bidhaa za kidoti kwenye ukumbi wa Nkrumah.
**********************************************
Na Mwandishi wetu
Mbunifu wa mitindo na Miss Tanzania namba mbili wa mwaka 2006 ametoa wito kwa wanafunzi wanao hitimu vyuo vikuu nchini kujihusisha na ujasiliamali na kutumia vilivyo vipaji vyao katika kupambana na soko la ajira.

Joketi alitoa wito huo juzi wakati akitoa mada ya jins ya kujiajiri mara baada ya kumaliza masomo ya elimu ya juu katika kongamano la wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) lijulikanao kwa jina la 2014 Market Forum.

Alisema kuwa pamoja na yeye kusomea mambo ya siasa na kuhitimu digrii yake chuoni hapo, mpaka sasa hajaweza kufanyia jambo lolote taaluma hiyo zaidi ya kujiajiri kupitia kampuni yake ya Kidoti Tanzania Limited ambayo inamuingizia fedha.
Alifafanua kuwa hatua hiyo imekuja kutokana na ugumu wa soko la ajira na kutokana na kuamua kujiajiri kwa njia mbadala (vipaji) vyake.
 “Wakati nasoma, lengo langu kubwa lilikuwa ni kuwa mwanasiasa, nilimaliza hapa hapa Chuo Kikuu na baadaye nilishauliwa nichukua ‘masters’, nilianza kusoma, hata hivyo nilihairisha masomo hayo baada ya kuamua kuanza kuwa mbunifu na mwaka 2013 nilizindua bidhaa yangu ya nywele na nguo zijulikanazo kwa jina la ‘kidoti brand’ na sasa nimeingiza sokoni kandambili aina ya kidoti,” alisema Jokate.

Alisema kuwa alifanya utafiti wa kina ili kuteka soko la bidhaa zake na mpaka sasa anazidi kubuni aina nyingine za mitindo ya nywele, nguo, kandambili na bidhaa nyingine.
“Tusitegemee ajira kutokana na kile tulichokisomea, tunatakiwa kuwa wabunifu na kutumia vipaji vyetu, ukiweka nia tafanikiwa pamoja na ugumu wa kupata mtaji na mambo mengine, kwa kufanya hivyo utaweza kumpa ajira mtu aliyesoma zaidi yako, ipo mifano mingi duniani na matajiri wengi hawana elimu ya kutosha, ila wamekuwa wabunifu na sasa wameajiri wataalam ambao ni wasomi, hata hivyo soko la ajira ni dogo na wachache ndiyo wanabahatika kupata kazi,” alisema.
Alisema kuwa kwa sasa lengo lake kubwa ni kutawala soko na kuwa milionea pamoja na kupata ushindani mkubwa katika soko kutokana na wingi wa bidhaa kama zake.