Friday, 21 February 2014

JUSTIN AUGUSTIN NA EMIRIANA ABDALLAH WAFUNGA NDOA 21-2-2014

 Ni vijimambo ukumbini
 Bw harusi na Bi harusi wakitabasamu
 Wageni waalikwa waliitikia wito kweli
 Bw na  Bi Richard kwitega wakifurahia harusi
 Wazazi upande wa Bi harusi
 Wazazi upande wa Bw harusi
 Kijana Nelson akipata kinywaji
 Justin kijana mcheshi, wengi wanamjua kama Fundi umeme makini
 Ni staili ya tu
 Konyagi na safari, badae inakua hivi....
 Mzuka ukipanda
Ongera maharusi

ASUBUHI YA LEO NDANI YA JAMCOBARBER SHOP,WADAU WAKIFANYA USAFI KUELEKEA KWENYE HARUSI YA OCD WA KINONDONI WILBROD MUTAFUNGWA ANAEFUNGA NDOA LEO

 Bw Alan akiwa Bushira wakifanyiwa usafi
 Bw Basibila aliesimama ndie mratibu wa shughuli nzima kwa Bukoba mjini akiwa na Bw Bushira wakiwa Jamcobarber shop
 Bw Alan akifanyiwa scrub
Tutawaletea badae kinachojili kanisani na sherehe itakayofanyika nyumbani kwao Bugandika na badae katika ukumbi wa Lina's

Thursday, 20 February 2014

WATOTO MAPACHA WALIOKUWA WAMEUNGANA WAREJEA JIJINI DAR WAKITOKEA INDIA


 Watoto mapacha kutoka wilayani Kyela mkoani Mbeya waliokuwa wamepelekwa na serikali chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kufanyiwa upasuaji mkubwa wa kuwatenganisha wakiwasili nchini Tanzania kutokea nchini India walipokuwa wakipatiwa matibabu katika hospitali ya watoto ya Appolo. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Magonjwa ya Nje wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Edward Sawe, mama mzazi wa watoto hao Bi. Grace Joel na Daktari aliyekuwa akiwaangalia nchini India Dkt.Glory Joseph.
 Watoto hao wakiwa wamebebwa na Daktari aliyekuwa akiwaangalia nchini India Dkt.Glory Joseph (kushoto) na mama mzazi wa watoto hao Bi. Grace Joel.
Mama  mzazi wa watoto hao Bi. Grace Joel akiwa amewabeba watoto wake Elikana Erick (kushoto) ns Eliud Erick (kulia) mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
******************************
Picha na Stori Na. Aron Msigwa – MAELEZO
Hatimaye watoto mapacha kutoka wilayani Kyela mkoani Mbeya waliokuwa wamepelekwa na serikali chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kufanyiwa upasuaji mkubwa wa kuwatenganisha jana jioni wamerejea nchini wakitokea nchini India katika hospitali ya watoto ya Appolo walikokuwa wanapatiwa matibabu.
Mara baada ya kuwasili katika  Uwanja ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakiwa wameambatana  na mama yao mzazi Grace Joel na Daktari aliyekuwa akiwaangalia nchini India ambaye pia alikuwa masomoni akisomea magonjwa ya Moyo kwa watoto Dkt. Glory Joseph wamepokewa na Mkuu wa Kitengo cha Magonjwa ya Nje wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Edward Sawe  na baadhi ya wauguzi kutoka Taasisi ya Mifupa (MOI) .
Mapacha hao wa kiume wakiwa wenye  furaha na afya njema walichukuliwa katika gari maalum na kupelekwa katika Taasisi ya Mifupa (MOI) ambako watakaa kwa muda mfupi na kisha kuruhusiwa kuelekea wilayani Kyela jijini Mbeya ambako ndiko walikozaliwa.
 Kwa upande wake mama mzazi wa watoto hao akizungumza kwa furaha mara baada ya watoto wake kupatiwa matibabu ya kuwatenganisha kwa mafanikio makubwa amesema kuwa sasa maisha yake yamebadilika na ataishi kwa furaha na watoto wake.
“Najisikia furaha sana kwa hatua niliyofikia mpaka hapa watoto wangu Eliudi na Elikana sasa ni wazima naishukuru sana Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa msaada ilionipatia” amesema.
Kwa uipande wake Daktari aliyekuwa akiwaangalia nchini India ambaye pia alikuwa masomoni akisomea magonjwa ya Moyo kwa watoto Dkt. Glory Joseph akizungumzia matibabu ya watoto hao nchini India amesema kuwa hatua ya kuwatenganisha imekamilika na mwezi wa 8 mwaka huu watarudi tena nchini India kwa ajili ya uchunguzi na matibabu zaidi ya afya zao.
“Ni kwamba watoto hao wametenganishwa, kwa wakati huu wanaelekea MOI ambako watakaa kwa muda na baadaye wataruhusiwa kwenda kwao Mbeya kujumuika na jamaa zao” amesema.
Kwa upande wake msemaji wa wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bw. Nsachris Mwamwaja amesema kuwa watoto hao waliwasili jana jioni na ndege ya shirika la ndege la Oman baada ya kumaliza matibabu ya awamu ya kwanza.
Amesema upasuaji huo mkubwa wa kuwatenganisha watoto hao ulichukua saa 18 na kufafanua  kuwa kati ya hizo  saa 13 zilitumika kutenganisha viungo vilivyoungana sehemu ya chini ya uti wa mgongo,sehemu ya utumbo mpana,njia ya mkojo,kibofu cha mkojo na sehemu za uume huku saa 5 zikitumika kuunganisha sehemu zilizotenganishwa.
“Kumbukumbu zinaonyesha kuwa mpaka sasa duniani upasuaji wa aina hii umefanikiwa mara tano  kutenganisha mapacha watoto wa kiume walioungana” amesisitiza.
Ameongeza kuwa matibabu hayo ni juhudi za serikali katika kuhakikisha kuwa huduma za afya zinatolewa  kwa kila mwananchi kila inapowezekana na kutoa wito kwa jamii kujenga utaratibu wa kuwafikisha mapema kwenye vituo vya afya wale wote wenye matatizo ya kiafya badala ya kuwafikisha pindi hali zao zinapokuwa mbaya.

JIJINI DAR LEO BAADA YA RASHARASHA ZA MVUA


 Gari aina ya Isuzu likiwa limeanguka kwenye mtaro pembezoni mwa barabara ya Makongo eneo la Lugalo, haikuweza kufahamika kwa haraka chanzo cha ajali hiyo, lakini kubwa ikiwa ni utelezi katika eneo hilo kutokana na mvua za rasharasha zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam hii leo.  
 Wahusika wa gari hilo wakijadiliana jinsi ya kulikwamua gari hilo........
 Hapa ni eneo la Posta mpya barabara inayotoka Hidary Plaza, ikiwa imeharibika vibaya na kuwa na madimbwi yaliyofunikwa na maji ya mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha baadhi ya madereva wa magari wasiojua ramani ya barabara hiyo, kukwama kama linavyoonekana gari hili likiwa limekwama katika eneo hili. 
 Eneo hili lilipokwama gari hili kuna shimo kubwa lililowazi.......
 Kuku wa Kisasa wakiwa katika usafiri wa Pick up kuelekea Soko la Kisutu tayari kwa kuuzwa kwa wateja. Pembeni mwa gari hilo ni askari wa usalama barabarani wakidili na waendesha bodaboda wanaokatisha njia hiyo kwa kuvunja sheria za usalama barabarani.
Hili ni eneo la Jangwani walipohamishwa wananchi waliopelekwa Mabwe Pande likiwa limebaki dampo la chupa chakavu na huku baadhi ya wananchi wakionekana kuendelea kuishi eneo hilo katika vibanda.

Tuesday, 18 February 2014

KAMPUNI YA EDCAT INTERNATONAL LTD YAKABIDHI JENGO LA HAZINA BUKOBA BAADA YA KUKAMILISHA UKARABATI

 Huu ndio muonekano wa jengo la Hazina Bukoba lililofanyiwa ukarabati na kampuni ya EDICAT INTERNATIONAL LTD, jengo hili lipo mtaa wa kawawa Manispaa ya Bukoba,na kipindi cha mwanzo mamlaka wa mapato(TRA BUKOBA) walitumia jengo hili.
 Maeneo ya ndani
 Sehemu ya juu
 Mkurugenzi mtendaji wa Edicat International Ltd Bw  Edger Rutaraka,Bw Ezra Msanya kutoka wizara ya fedha makao makuu na Mrs Mary Mushobozi mkurugenzi wa fedha Edicat International wakiteta jambo kabla ya  makabidhiano ya jengo
 Ukaguzi wa jengo ukiendelea
 Bw Edger Rutaraka akitoa maelezo kwa Bw Mcharo , mkaguzi mkuu wa ndani(wizara ya fedha)
 Bw Kilo (mkurugenzi wa ushauri wakala wa majengo ya serikali akikagua jengo
 Utepe ukakatwa kuashiria  kukubali kupokea jengo rasmi
 Kweli jengo limependeza....
 Baada ya kazi, ni kujipongeza
 Ongera mama kwa kazi nzuri
 Mrs Mary Mushobozi akiwa na furaha kwa kukabidhi jengo
Bw Edger Rutaraka akiwa na wahudumu waliokuwa katika vitengo tofauti kipindi chote cha ukarabati