Saturday 3 October 2015

MGOMBEA UDIWANI KATA YA KAGONDO SMART BAITANI ASEMA NDANI YA SIKU 90 KATIKA UONGOZI WAKE KAGONDO MPYA ITAONEKANA.

 Mgombea udiwani ccm kata ya Kagondo Bukoba Manispaa Smart Baitani, katika ufunguzi wa kampeni zake amesema ajenda namba moja kwake ni maendeleo kwa Kagondo,amesema amedhamilia kwa dhati kuibadilisha Kagondo na kuiletea maendeleo,amesema anaomba wanakagondo wamuamini wampe ridhaa kwa kumpa kura za kutosha na yeye ndani ya siku 90 wataona mabadiliko makubwa ndani ya kagondo,ameendelea kusema amekuwa nchini Marekani kwa zaidi ya miaka 20, lakini kupitia shirika lisilo la serikali Cosad yeye kama mkurugenzi limefanya mambo mengi kwa ajili ya kupambana na umasikini katika jamii, na hata Kagondo iko miradi mingi ambayo Cosad imesaidia wananchi.Bw Smart amesema wanakagondo hawana sababu ya kubabaika,waachane na walaghai wanaowatumia kwa kujipatia madaraka na baada ya hapo wanawadhulumu haki zao kwa jeuri na kiburi na kujinufaisha wenyewe.


 Mgombea udiwani kata Ijuganyondo Almasoud Kalumuna akisalimiana na Bw Smart Baitan.
 Kushoto Bw Samora Lyakulwa mgombea udiwani kata Kashai akiwa na Bw Jamco.
 Wananchi waliofika kwenye mkutano.
 Bw Bernard Matungwa akieleza wananchi aina ya kiongozi anaetakiwa Kagondo.
 Katibu wa ccm Mkoa wa Kagera.
 Mwenezi wa ccm Bukoba mjini Ramadhani kambuga akitoa neno.
 Ngoma ikachezwa.
 Katibu wa UWT Bukoba mjini akimwaga sera, Mwajabu Galiatano.
 Mama Katomero , shangazi ya bw Smart Baitan akimuombea kura mwanae.
 Bw Smart Baitan akiongea na wananchi wa Kagondo.
 Mgombea ubunge jimbo la Bukoba mjini Balozi Kagasheki nae akaongea na wana Kagondo.
Endelea kufuatilia matukio jamcoblog.

MATUKIO KATIKA PICHA MAZISHI YA MAREHEMU GABRIEL KABUHAYA, KATOMA BUKOBA.

jamcobukoba.blogspot.com wanawapa kwa pole familia yote.