Wednesday 18 November 2015

WAZIRI MKUU MTEULE KASSIMU MAJALIWA,ULETAJI WA BAHASHA BUNGENI WAWA GUMZO.

 Zile presha zilizokuwa miongoni mwa watanzania mbayo ndani wengi nani atakuwa waziri mkuu, hatimae rais Jo hn Pombe Magufuli ameteua jina la Mh Kassimu Majaliwa kuwa waziri mkuu wa serikali a awamu ya tano,mmoja ya kitu ambacho kimefurahisha ni namna ya usiri mkubwa uliokuwepo na namna ya jina lilivyoletwa bungeni, Mlinzi wa rais akiwa na maafisa kadhaa kutoka Ikulu walileta bahasha kubwa ambayo ndani yake zilikuwemo bahasha zingine mbili ndogo kufikia barua aliyoandikiwa spika iliyokuwa imeandikwa kwa mkono wake rais.
Katika picha wa kwanza kulia Waziri mkuu mteule Kassimu Majaliwa akizungumza na  Mh Richard Kasesela  mkutano mkuu wa Taifa ccm kupitisha jina la mgombea urais Dodoma.

NI MWAKA MMOJA LEO TANGU MAREHEMU LEONARD MTENSA AFARIKI,ANGALI BAADHI YA MATUKIO KATIKA MAZISHI YAKE

 Nakumbuka ilikuwa ni mstuko mkubwa katika kila kona ya Manispaa ya Bukoba na maeneo mengine pale mtu alipopata taarifa za msiba wa Mtensa,watu wengi walionekana kutoamini taarifa hiyo kwani wapo waliokuwa na marehemu masaa machache kabla ya kifo akiwa mzima, wapo wa siku moja nk,lakini yote hayo ni maneno tu ya mwanadamu kwani tarehe ikifika hakuna kizuizi,Mtensa leo ni mwaka sasa hatuko nawe tunakukumbuka kwa mahusiano yako mazuri katika jamii kwa ujumla,Unakumbukwa na familia yako,ndugu , jamaa na marafiki, Kipekee umoja wako wa Pamoja group unakukumbuka sana,tunaamini kimwili hatuko wote bali kiroho tuko pamoja, Pumzika kwa amani Leornard Mtensa Mkurugenzi wa Lina's.Siku ya jumamosi tarehe 21-11-2015 itakuwepo misa ya kumkumbuka nyumbani kwake Kyakairabwa aliko zikwa.





 Mr Ernest Nyambo akiweka shada la maua.
 Rafiki kipenzi wa marehemu Mr Bube.
 Wafanyakazi wote wa Lina's wakimuaga bosi wao.



Hakika wanapamoja kama vile hawaamini kile killichokuwa kinafanyika.