Saturday 13 June 2015

KINANA AINGIA WILAYA YA NGARA LEO, AKAGUA MIRADI YAMAENDELEO NA KUTOA CHANJO KWA WATOTO


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpa matone ya chanjo mtoto Benita Cosmas, wakati alipozindua utoaji matone ya chanjo kwa watoto chini ya miezi sita, katika Kituo cha Afya cha Kashinga, kata ya Nyakisasa, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CM na uhai wa Chama katika wilaya ya Ngara mkoani Kagera, leo. Mama wa mtoto huyo ni Editha Rubambura.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpa kidonge cha chanjo mtotoFrank Laurent, wakati alipozindua utoaji vidonge vya chanjo kwa watoto chini ya mmwaka mmoja, katika Kituo cha Afya cha Kashinga, kata ya Nyakisasa, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CM na uhai wa Chama katika wilaya ya Ngara mkoani Kagera, leo. Mama wa mtoto huyo ni Janeth Leopard.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akipanda mti wa kumbukumbu, katika Kituo cha Afya cha Kashinga, kata ya Nyakisasa, alipokagua ujenzi wa kituo hicho cha afya akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CM na uhai wa Chama katika wilaya ya Ngara mkoani Kagera, leo.
Mkuu wa mkoa wa Kagera, John Mongela akizungumza na waananchi,  baada ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana  alipokagua ujenzi wa kituo cha afya cha Kashinga, katika kata ya Nyakisasa, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CM na uhai wa Chama katika wilaya ya Ngara mkoani Kagera, leo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara aliofanya leo Ngara mjini, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama, katika wilaya ya Ngara mkoani Kagera
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza katika mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana aliofanyika leo mjini Ngara mkoani Kagera
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipatiwa maelezo kuhusu mradi wa maji katika mji wa Ngara akiwa katika ziara kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM na uhai wa Chama katika mkoa wa Kagera, leo
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akijadili jambo na Mkuu wa mkoa wa Kagera, alipokuwa akikagua ujenzi wa mradi wa Umeme Vijijini (REA) katika mji wa Ngara mkoani Kagera leo
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizindua chama cha Maendeleo ya Kina mama katika wilaya ya Ngara, kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara mjini Ngara mkoani Kagera leo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikata keki kuzindua akizindua Chama cha Maendeleo ya Kina mama wa Wilayani Ngara mkoani Kagera kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika mji wa Ngara leo
Wananchi wakishangilia CCM wakati wa mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana aliofanyika leo baada ya mapokezi ya kuingia wilaya ya Ngara akitokea Kyerwa, uliofanyika katika mji mdogo wa Benacc wilayani Ngara
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika mji mdogo wa Benacco baada ya msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kuwasili katika wilaya ya Ngara ukitokea Kyerwa kuendelea na ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama mkoani Kagera leo
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akihutubia mkutanao wa hadhara katika mji mdogo wa Benacco, baada ya kuwasii wilayani Ngara, leo kuendelea na ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama mkoani Kagera
Mmmoja wa wakazi wa mji mdogo wa Benacco, kuwa aliwahi kuwa kada wa Chadema akajitoa kutokana na chama hicho kuendekeza amaandamano, akieleza kero walizo nazo wananchi wa mji huo, katika mkutano wa hadhara wa Kinana uliofanyika katika mji huo leo
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano wa hadhara aliofanya katika Kijiji cha Rulenge wilayani Ngara mkoani Kagera leo
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisaidia kumpatia bati fundi aliyekuwa akipaua, wakati alipotembelea jenzi wa Ofisi ya CCM tawi la Mujebwe, wilayani Ngara mkoani kagera leo
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimwisha ndoo ya maji Francisca Katana, baada ya kuzindua mradi wa maji wa Kijiji cha Rulenge wilayani Ngara mkoani kagera
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika leo katika Kijiji cha Rulenge wilayani Ngara mkoani Kagera leo
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara wa Kinana uliofayika katika kijiji cha Rulenge, wilayani Ngara mkoani Kagera leo
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara wa Kinana uliofayika katika kijiji cha Rulenge, wilayani Ngara mkoani Kagera leo
Wananchi wakishangilia katika mkutano wa hadhara wa Kinana uliofanyika katika Kijiji cha Rulenge wilayani Ngara mkoani Kagera
Mmoja wa wazee wa Kijiji cha Rulenge wilayani Ngara mkoani Kagera akiomuonyesha vielelezo kuhusu kero za mashamba zinazowakabili wananchi wa kijiji hicho, leo
Burudai zikiendelea baada ya mkutano mkubwa wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM uliofanyika leo katika kijiji cha Rulenge wilayani Ngara mkoani Kagera leo.

PICHA ZA ALI KIBA AKITENGENEZA VIDEO AFRICA YA KUSINI.



Mambo ya Ali Kiba hayo.

OB V
SHARE

Thursday 11 June 2015

LOWASSA KUWASILI BUKOBA JUMATATU 15-6-2015 KWA AJILI YA KUPATA WADHAMINI.

 Waziri mkuu mstaafu na mgombea urais 2015  Edward Lowassa atawasili katika Manispaa ya Bukoba 15-6-2015 siku ya Jumatatu kwa ajili ya kupata wadhamini,Kwa taarifa  ya uhakika kutoka kwa mmoja wa watu wa karibu sana wa Mh Lowassa ameseme atawasili majira ya saa tatu kamili katika uwanja wa ndege wa Bukoba kwa ndege maalumu,na baada ya hapo msafara wake utaondoka kuelekea ofisi za chama cha mapinduzi Mkoa wa Kagera na kukutana na wadhamini,Chanzo cha habari hii kimesema  hakuna kikomo cha wadhamini yeyote atakaejisikia na kuwiwa kudhamini anakaribishwa, Mh Lowassa kila mahala alipokuwa anakwenda watu wamekuwa wakijitokeza kwa wingi na kuonyesha mapenzi makubwa sana,(MANENO YA CHANZO CHA HABARI HII.)Hivyo amewaomba wale wote watakaoona wako tayari kudhamini wafike ,maana safari ya matumaini imewadia.
SAFARI YA MATUMAINI IMEWADIA.

Monday 8 June 2015

KINANA AKAGUA MIRADI,ANG'AKA NA WATENDAJI NA WANASIASA WABADHIRIFU WANAOWAIBIA WANANCHI.

Katibu mkuu wa ccm Taifa Abdulrahaman Kinana ametembelea miradi mbalimbali katika Manispaa ya Bukoba ikiwa ni ziara yake ya ukaguzi wa utekelezaji wa ilani ya ccm 2010 -2015,Pia amekutana na Halmashauri kuu ya ccm Manispaa kuwasikiliza na kujua kero mbalimbali za wananchi,Mh Kinana ametembelea uwanja wa ndege wa Bukoba uliokarabatiwa  kwa kiwango cha rami na kuangalia maendelea ya ujenzi wa jengo jipya la mapokezi, pia ametembelea mradi mkubwa wa maji unaoendelea katika jimbo zima la Bukoba,Mh kinana alifuatana na Bw Nape ametembelea vikundi mbalimbali vya vijana na akina mama kujionea namna wanavyoshughurika na miradi yao,Mh Katibu mkuu Taifa Abdulhamani Kinana akiwa katika uwanja wa Uhuru Plat Form akihutubia wananchi amesema ,Chama kipindi cha uchaguzi ndio kinatafuta dora, na baada ya hapo inaundwa serikali,ila anasikitika kuona watendaji ambao hawajui hata serikali imepatikanaje wanakuwa wajeuri na kunyanyasa wananchi kwa lugha mbaya na kuwaibia,akasema ipo haja sasa ya kurekebisha baadhi ya sheria ambazo zimepitwa na wakati zinazolinda wabadhilifu wa mali za umma,akiongelea sakata la mradi wa viwanja elfu tano ,amesema anaomba wananchi wawe na subira limefika mahala pazuri na watafidiwa,maana ni kweli waliibiwa.

 Wajumbe wa Halmashauri kuu ya ccm Bukoba Mjini wakiwa katika ukumbi wa St Francis.
 Bw Abdul Kagasheki Mnec Bukoba Mjini.
 Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba .
 Kushoto , Mwenyekiti ccm  Bukoba Mjini Yusufu Ngaiza, Mwenyekiti ccm Mkoa Kagera Constancia Buhiye, Mbunge Balozi Khamis sued Kagasheki.
 Vijana Wamachinga Mh Kinana alifungua Saccos yao.
 Ni eneo la soko kuu Bukoba Mh Kinana alitembelea.

 Meneja wa uwanja wa ndege Bukoba akitoa taarifa.
 Muonekano wa jengo jipya la mapokezi la uwanja wa ndege Bukoba.
 Mh Kinana akiangalia maeneo mbalimbali uwanja wa ndege Bukoba.
 Alitembelea umoja wa akina mama wa Kastamu.
 Mradi wa maji.
 Mh Kinana akisalimiana na wafanyakazi wa mradi mkubwa wa maji unaoendelea Bukoba.
 Mbunge akielezea mradi wa maji.
 Maelezo ya kina yakatakiwa maana muda wa makabidhiano umepita.
 Maagizo makali yakatolewa kukabidhi mradi.
 Mwenyekiti wa vijana mkoa Kagera Yahaya Kateme(kushoto) akiwa na bw Haridi.

Waendesha pikipiki wakiusindikiza msafara wa Kinana.