Saturday 21 December 2013

IVO MAPUNDA NA MASOTI WAANZA DHIDI YA YANGA


Simba line up: Ivo Mapunda, Haruna Shamte, Issa Rashid, Joseph Owino, Donald Musoti, Jonas Mkude, Haruna Chanongo, Henry Joseph, Amisi Tambwe, Said Hamis na Awadh Juma.

MTANI JEMBE: SIMBA VS YANGA - OKWI AANZIA BENCHI - KASEJA AANZA KIKOSI CHA KWANZA

1.Juma Kaseja - 29
2.Mbuyu Twite - 6
3.David Luhende - 3
4.Nadir Haroub "Cannavaro" - 23(C)
5.Kelvin Yondani "Cotton" - 5
6. Athuman Idd " Chuji" - 24
7.Mrisho Ngassa - 17
8.Frank Domayo - 18
9.Didier Kavumbagu - 7
10.Hamis Kiiza - 20
11.Haruna Niyonzima - 8
Subs:
1.Deogratius Munishi "Dida" -30
2.Juma Abdul - 12
3.Oscar Joshua - 4
4.Rajab Zahir - 14
5.Reliants Lusajo - 9
6.Nizar Khalfani - 16
7.Saimon Msuva
8. Hassan Dilunga - 26
9.Jerson Tegete - 10
10.Emmanuel Okwi - 25
11. Said Bahanuzi - 11
12.Hamis Thabit - 22

ICC yaahirisha kesi ya Rais Kenyatta


Rais Uhuru Kenyatta
Kesi inayomkabili Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta huenda ikachelewa kuanza baada ya mwendesha mashtaka mkuu wa Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa jinai (ICC) Kukiri kuwa hana ushahidi wa kutosha wa kuendeleza kesi hiyo.
Rais wa Kenya amekanusha mashtaka ya dhulma dhidi ya ubinadamu zinazohusiana na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007. Zaidi ya watu elfu moja waliuawawa katika mapiganao hayo na maelfu yaw engine kupoteza makazi yao.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari Bi. Fatou Bensouda amesema kuwa uamuzi huo unatokana na mashahidi wawili wakuu katika kesi hiyo kukataa kutoa ushahidi dhidi ya Rais Kenyatta. Mmoja wao amesema kuwa hayuko radhi kusema anayojua kuhusu kesi hiyo ilhali wa pili amesema kuwa alidanganya katika ushahidi wake wa awali katika kesi hiyo.
Kujiondoa kwa mashahidi hao imemfanya kiongozi wa mashtaka kusema kuwa kesi dhidi ya Bwana Kenyatta haifikii kiwango cha ushahidi kinachohitajika jambo lililomchochea kuomba kesi hyo isimamishwe kwa muda ili aweze kusawazisha na kukusanya ushahidi zaidi.
Kesi ya Bwana Kenyatta ilipaswa kuanza huko The Hague tarehe 5 Februari mwaka ujao . Bwana Kenyatta alishtakiwa pamoja na naibu wake William Ruto na mtangazaji Joshua Arap Sang kwa makosa ya mauji, kusababisha watu kuhamishwa kwa nguvu katika makazi yao, kusababisha mateso kwa umma na ubakaji kufuatia ghasia zilizotokana na matokeo ya urais katika uchaguzi huo.
Kesi ya Kenyatta na naibu wake imekuwa ikifuatiliwa kwa karibu na jamii ya kimataifa haswa baada ya Umoja wa Afrika kutishia kuyaondoa mataifa ya Afrika katika uanachama wa mahakama hiyo iliyobuniwa chini ya mkataba wa Roma. Umoja wa Afrika umekuwa ukidai mahakama hiyo imekuwa ikiwalenga viongozi wa bara Afrika.

Friday 20 December 2013

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII BALOZI KHAMIS KAGASHEKI AJIUZULU

Waziri wa Maliasili na Utalii  Balozi Khamis Kagasheki amejiuzuru  bungeni, Baada ya kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira kutoa taarifa ya ukiukwaji mkubwa uliofanyika katika zoezi zima la Operesheni Tokomeza.

MAPOKEZI YA MWILI WA MAREHEMU RAJESH JOSEPH BANDARI YA BUKOBA LEO

                                        Ni ndugu na jamaa wa marehemu Rajesh






















 

Wednesday 18 December 2013

MSANII WA BONGO FLEVA ANAYEISHI NCHINI ITALIA REMMY WILLIAMS ATUA NCHINI KWA MAPOKEZI MAKUBWA


Remmy Williams akiwa ameshikwa mkono na meneja wake wa Tanzania, Mcdennis Mgatha.


MSANII wa Muziki wa Bongo Fleva, Remmy Williams, anayefanya shughuli zake nchini Italia jana ametua jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya kazi na wasanii wenzake hapa nchini.

Akizungumzia ujio wake mara baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar, alisema kuwa anawapenda wasanii wote wa Tanzania wanavyofanya vema nchini na kazi zao nyingi zinavuka mipaka kwa ajili ya kujitangaza kimataifa.

Hata hivyo yeye amejitokeza kuupaisha muziki huo kwa kushirikiana na wasanii atakaochaguliwa kushirikiana nae.

Akizungumzia ujio wa msanii huyo, meneja wake nchini Tanzania, Mcdennis Mgatha, amesema msanii huyo kaja nchini kwa ajili ya kufanya kolabo na wasanii hapa nchini hivyo wapenzi wa muziki wakae mkao wa kula kwani ana vitu vingi sana alivyowaandalia ikiwemo nyimbo mpya pamoja na kufanya shoo kwa ajili ya kutambulisha nyimbo hizo.

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Remmy Williams akiwa na maua baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea nchini Italia.
 
 Remmy (kushoto) akiwa na meneja wake wa nchini Italia, Wactor Fizio, walipowasili nchini.
Remmy Williams (katikati) akilakiwa na baadhi ya warembo waliojitokeza kumpokea uwanjani.

ANGALIA JOKATE ALIVYOZINDUA KIDOTI CLUB


Pichani kulia ni aliyewahi kuwa Miss Tanzania namba mbili mwaka 2006,Jokate Mwegelo akizungumza na baadhi ya Wanahabari (hawapo pichani) kutoka vyombo mbalimbali mapema leo Mikocheni jijini Dar kuhusiana na uzinduzi wa klabu yake iliyojulikana kwa jina la KIDOTI CLUB,Shoto ni mmoja waratibu,Mtangazaji wa East Africa Radio aitwaye Bhoke.

Mmoja wa Mashuhuda akitoa ushuhuda wake mara baada ya kujiunga kwenye klabu ya KIDOTI CLUB,kwa njia ya simu kwa kutuma neno KIDOTI kwenda namba 15678 na kuanza kupata taarifa mbali mbali kutoka kwake katika kampeni hiyo ijulikanayo kwa jina la Kidoti Ng’aring’ari.


Baadhi ya wanahabari waliofika kwenye uzinduzi huo uliofanyika Mikocheni,jijini Dar.


========= ======== ========


Baada ya kutamba na mitindo ya nywele na nguo aina ya Kidoti brand, msichana mwenye vipaji vingi hapa nchini, Jokate Mwegelo ameanzisha klabu yake ijulikanayo kwa jina la Kidoti Club.

Akizungumza katika uzinduzi wa klabu hiyo jana, Jokate alisema kuwa Kidoti Club ni tofauti na vilabu vingine kwani katika ujio wake huo mpya, atakuwa anajihusisha na mambo mbali mbali katika jamii hususani masuala ya urembo na mitindo. Jokate pia alizindua aina mpya ya nywele zake za kisasa katika mtindo wa kidoti Brand.

Jokate alisema kuwa kupitia klabu yake atakuwa anatoa ushauri mbali mbali katika jamii na ikiwa pamoja na taarifa za muziki, filamu, wasanii mbalimbali na nyinginezo kwa ajili ya rika tofauti. Alisema kuwa lengo lake kubwa ni kupanua mtandao wake kwa jamii na anaamini watu wengi watajiunga naye.

Kwa mujibu wa Jokate ambaye ni Miss Tanzania namba mbili mwaka 2006, ili uwe mwanachama wa klabu hiyo, unatakiwa kutuma neno kidoti kwenda namba 15678 na kuanza kupata taarifa mbali mbali kutoka kwake katika kampeni hiyo ijulikanayo kwa jina la Kidoti Ng’aring’ari.

“Huu ni mfumo wa kisasa katika kutoa taarifa mbali mbali kwa jamii,Beyonce amefanya hivyo na kwa sasa hakuna mtu anayeingia katika shoo zake bila kuwa mwanachama wa klabu yake, mimi pia naelekea huko kwani nitaweka taarifa zangu mbali mbali na ili kupata lazima uwe mwanachama,” alisema Jokate ambaye pia ni mtangazaji na mbunifu wa mavazi. Alisema kuwa pia ataendesha mashindano mbali mbali kwa wanachama wake na kutoa zawadi kwa washindi.

“Kama unavyojua, lengo langu kubwa ni kutumia ujuzi na kipaji chake kwa watanzania wote, nataka wafaidike na vipaji vyangu name kusimama mwenyewe katika maisha bila ya kumtegemea mtu yoyote, natoa wito kwa vijana wenzangu kuwa wabunifu katika kukabiliana na masuala mbali mbali ya maisha,” alisema.

Monday 16 December 2013

Pichaz 30 za After Skul Bash Wanafunzi Full kujiachia Ni Shidaaa!!


Mambo yalikuwa si mambo ndani ya After School Bash baada ya madadaz na makakaz walipoamua kupendeza na kujitokeza pande za MbalaMwezi Desemba 14 Jumamosi iliyopita,huku burudani zikitolewa na wasanii mbalimbali.
Angalia picha hizi hapa uone kichojiri Desemba 14 Jumamosi iliyopita Mbala  Mwezi Beach