Tuesday 2 February 2016

SEND OFF YA PRAKSEDA .C. NDAMUGOBA YAFANA UKUMBI WA BUKOBA COOP.

Prakseda akiwa na kaka yake wakiingia katika ukumbi wa Bukoba coop(Yasira hotel zamani)wakiingia kwa staili ya aina yake.
Mama Semeo mtaalam maalufu wa kutengeneza keki akiandaa mambo yake.
Ndugu wa Bi harusi mtarajiwa.
Kundi la Kibeta one wakiingia ukumbini.
Wadada wakicheza kwa madahaa.
Akiwa na Bw harusi mtarajiwa.
Akikata keki.
Akimrisha keki kaka yake.



Sunday 31 January 2016

JAJI MKUU MHE.OTHMAN CHANDE AFUNGUA RASMI MAADHIMISHO YA WIKI YA SHERIA NCHINI MWAKA 2016



Watumishi wa Mahakama ya Tanzania na wadau mbalimbali wa wakiingia katika viwanja vya Mnazi mmoja kwa maandamano leo jijini Dar es salaam wakati wa Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria.

Watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), Askari wa Jeshi la Magereza na Watumishi wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) wakiwa wamebeba mabango ya Ofisi zao wakati wa Ufunguzi wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria Nchini leo jijini Dar es salaam.

Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande (Mwenye T-shirt nyeupe kulia), Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Mecki Sadiki (wa Pili kulia) na Watendaji wa Mahakama ya Tanzania wakishiriki mazoezi ya viungo ya pamoja na wadau mbalimbali wa Mahakama leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria Nchini.

NAIBU WAZIRI WA AFYA AZINDUA DUKA LA DAWA LA MSD JIJINI ARUSHA


Msimamizi wa Duka la MSD Arusha Twaha Kabandika akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Kigwangalla wa namna mfumo unaotumika kwa mauzo unavyofanya kazi.Kulia ni M/Kiti wa Bodi MSD, Prof Idris Mtulia, Mkurugenzi wa MSD Laurean Bwanakunu (Kushoto0 na Mkuu wa Wilaya ya Arusha mjini Fadhili Nkuru.
Naibu Waziri wa Afya akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya MSD Prof. Idris Mtulia alipowasili duka la MSD Mount Meru, Arusha kwa ajili ya kulizindua rasmi jana. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bw. Laurean Bwanakunu, akifuatiwa na Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda na Huduma kwa Wateja Bw. Cosmas Mwaifwani.




MAJANGILI YAUA RUBANI BAADA YA KUTUNGUA KWA RISASI NDEGE YA TANAPA



RUBANI wa helikopta ya Doria ya Mamlaka ya Wanyamapori Nchini, (TANAPA), Roger Gower raia wa Uingereza ameuawa baada ya kupigwa risasi akiwa angani na watu wanaosadikiwa kuwa majangili kwenye pori la akiba maswa lililoko wilaya ya Meatu mkoani Simiyu majira ya jioni Januari 30, 2016.
Kamanda wa Upelelezi wa Mkoa wa Simiyu, Jonathan Shana ambaye alikuwa kwenye eneo la tukio, amesema, askari mmoja wa wanyamapori aliyekuwemo ndani ya helikopta hiyo amejeruhiwa.
“Helikopta hiyo haikudunguliwa, bali risasi ilimpata Rubani na hivyo akauawa na helikopta kupoteza mwelekeo na kuanguka.” Alifafanua Kamanda wa Upelelezi Mkoa wa Simiyu, Jonathan.
“Tutawasaka pori kwa pori, pango kwa pango, kijiji kwa kijiji hadi tuwatie mbaroni wahalifu hao. Tumeleta FFU wenye silaha za nkutosha, ili kutekeleza amri ya kamanda IGP, Kamanda DCI na RPC, ndio maana tuko hapa na silaha nzito.” Alisema Mkuu huyo wa upelelezi wa Mkoa wa Simiyu.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Allan Kijazi, walifika eneo la tukio na kushngazwa na tukio hilo ambapo waziri alisema, sasa wahalifu hawa wamefikia kiwango cha juu cha uhalifu hadi kuhujumu teknolojia ya kuhifadhi mazingira, kwa kuwashambulia watendaji wetu, Waziri alisema kwa huzuni na kuongeza kuwa Serikali haitavumilia uhalifu huo na kuahidi kuwasaka popote walipo.
Hili ni tukio la kwanza kwa majangili kutungua kushambulia helikiopta ikiwa angani na kusababisha kifo.
 Waziri Profesa Maghembe, akizungumza baada ya kufika kwenye eneo la tukio. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Allan Kijazi
 Waziri akionyeshwa sehemu risasi ilipopenya kwenye helikopta hiyo
Askari na maafisa wa serikali wakionyeshana sehemu helikopta hiyo ilipopigwa risasi na kuanguka baada ya rubani kuuawa