Friday 27 March 2015

TANGAZO LA MAADHIMISHO YA SIKU YA UPANDAJI MITI KITAIFA TAREHE 1-4-2015 WILAYA YA MISSENYE.

OFISI YA MKUU WA MKOA WA KAGERA KWA KUSHIRIKANA NA WIZARA YA  MALIASILI NA UTALII INAWATANGAZIA WANANCHI WOTE MAADHIMISHO YA SIKU YA UPANDAJI MITI KITAIFA  YATAKAYOFANYIKA TAREHE  1-4-2015  MAKAO MAKUU YA WILAYA MISSENYE KATIKA UWANJA WA MASHUJAA (BUNAZI) NA MGENI RASMI ATAKUWA KATIBU MKUU WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII DR ADELHELM MERU, KAULI MBIU YA MWAKA HUU NI  MISTU NI MALI, PANDA MITI. WANANCHI WOTE MNAOBWA KUHUDHURIA KWA WINGI KUANZIA SAA TATU ASUBUHI. KARIBUNI SANA.

Wednesday 25 March 2015

LOWASSA AMSHANGAA NAPE,KAZI IPO MWAKA HUU.

MH.LOWASSA ASHANGAZWA NA KAULI YA NAPE
'MH.LOWASSA ASHANGAZWA NA KAULI YA  NAPE
Siku moja baada katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha mapinduzi (CCM) Nape Nnauye kutoa kauli ya chama hicho kuhusu makundi yanayojitokeza kumshawishi waziri mkuu mstaafu Mhe Edward Lowassa kugombea urais, kuwa yanaweza kumkosesha sifa kiongozi huyo ya kuwania nafasi hiyo Mhe Lowassa amejibu kauli hiyo na kudai anashangazwa nayo huku akihoji imetokana na maamuzi ya kikao gani ndani ya CCM.
Mhe Lowassa anatoa kauli hiyo katika muendelezo wa kupokea makundi mbalimbali ya jamii kumshawishi kuwania nafasi urais ambapo safari hii waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda zaidi ya 60 na wananchi wa kawaida wamefunga safari kutoka wilayani mbarali mkoa wa Mbeya mpaka mjini Dodoma kumshawishi agombee ambapo amesema kauli ya Nape Nnauye inamshangaza kwani chama cha mapinduzi kina utaratibu wake wa kujadili mambo kama hayo kupitia vikao mbalimbali.
 
Mhe Lowassa pia akawataka wanaoendelea kumnyooshea vidole kuhusu hatua ya wananchi wenye imani naye kujitokeza kumshawishi awanie nafasi hiyo wasubiri ufike wakati muafaka ili wana-CCM na wananchi waweze kutoa maamuzi yao huku akisisitiza watu hasa vijana kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ili wapate haki yao ya kikatiba ya kuchagua kiongozi wanayemuhitaji.
 
Awali kundi hilo la vijana na bodaboda waliosafiri umbali wa kilometa zaidi ya 600 wakiongozwa na kamanda wa UV-CCM wilaya mbarali Ibrahim Ismaili wamesema lengo la safari yao hiyo ni kuungana na watanzania wengine kumtia moyo Mhe Lowassa ashawishike kuwania urais kwani wana imani kubwa naye huku wakidai pamoja na mambo mengine kama alivyoweza kujenga shule za kata nchi nzima pia ataweza kutegua bomu la tatizo la ajira hasa kwa vijana.' Siku moja baada katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha mapinduzi (CCM) Nape Nnauye kutoa kauli ya chama hicho kuhusu makundi yanayojitokeza kumshawishi waziri mkuu mstaafu Mhe Edward Lowassa kugombea urais, kuwa yanaweza kumkosesha sifa kiongozi huyo ya kuwania nafasi hiyo Mhe Lowassa amejibu kauli hiyo na kudai anashangazwa nayo huku akihoji imetokana na maamuzi ya kikao gani ndani ya CCM.
Mhe Lowassa anatoa kauli hiyo katika muendelezo wa kupokea makundi mbalimbali ya jamii kumshawishi kuwania nafasi urais ambapo safari hii waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda zaidi ya 60 na wananchi wa kawaida wamefunga safari kutoka wilayani mbarali mkoa wa Mbeya mpaka mjini Dodoma kumshawishi agombee ambapo amesema kauli ya Nape Nnauye inamshangaza kwani chama cha mapinduzi kina utaratibu wake wa kujadili mambo kama hayo kupitia vikao mbalimbali.

Mhe Lowassa pia akawataka wanaoendelea kumnyooshea vidole kuhusu hatua ya wananchi wenye imani naye kujitokeza kumshawishi awanie nafasi hiyo wasubiri ufike wakati muafaka ili wana-CCM na wananchi waweze kutoa maamuzi yao huku akisisitiza watu hasa vijana kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura ili wapate haki yao ya kikatiba ya kuchagua kiongozi wanayemuhitaji.
Awali kundi hilo la vijana na bodaboda waliosafiri umbali wa kilometa zaidi ya 600 wakiongozwa na kamanda wa UV-CCM wilaya mbarali Ibrahim Ismaili wamesema lengo la safari yao hiyo ni kuungana na watanzania wengine kumtia moyo Mhe Lowassa ashawishike kuwania urais kwani wana imani kubwa naye huku wakidai pamoja na mambo mengine kama alivyoweza kujenga shule za kata nchi nzima pia ataweza kutegua bomu la tatizo la ajira hasa kwa vijana.

Sunday 22 March 2015

KAGASHEKI AZUNGUMZA NA WAAJIRI WAKE,MAELFU WAJITOKEZA KUMSIKILIZA,AWATAKA WATENDAJI SERIKALINI KUWAJARI WANANCHI.


Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Balozi Khamis Sued Kagasheki  katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Uhuru plat form  Bukoba amewataka watendaji ndani ya serikali katika maeneo tofauti kuwasikiliza wananchi na kutatua kero zao bila vitisho na matusi.Balozi Kagasheki ameseme unapofika wakati wa uchaguzi viongozi wa kisiasa wanakuwa na wakati mgumu kwa wananchi kwa ajiri ya baadhi ya watendaji wachache wanaonyanyasa wananchi katika matatizo mbalimbali, kitu kinachopelekea wananchi wengi kuwa na hasira na serikali yao inayoongozwa na chama cha Mapinduzi, Kitu ambacho amesema  hakuna kiongozi wa chama anaetoa huduma katika ofisi za serikali, na kibaya zaidi baadhi ya watendaji wamekuwa na kauli mbaya kwa wananchi kwa kusema kuwa  Si serikali ya ccm, kitu ambacho kinajenga chuki wananchi na chama.Pia ameongerea michango mingi inayobuka na hasa mashuleni na kusababisha kero kubwa kwa wazazi,Kwa upande wa wafanyabiashara  amezungumzia kero iliyokuwepo ya Tozo ya Ushuru ambayoiriwekwa na sheria ndogondogo  iliyopitishwa na Manispaa na kuonekana utaratibu unaotumika kudai hiyo pesa uangaliwe upya na kwa utaratibu ambao hautareta kero kwa wafanyabiashara, kwa maana ya mfumo unaotumika sasa wa kuweka viwango vikubwa.
 Wananchi waliojitokeza kwa wingi wakimsikiliza Mbunge.
 Bwa Rugambwa  kwa raha zake.
 Wanasema vijana wa mjini Nyomi ya watu walifurika.
 Ukafika wakati wa kuchangia wasanii waliotoa albam ya nyimbo tatu kwa ajiri ya Mshikamano kwa wanaBukoba.
 Wamama wakipata raha ya Taarabu.
 Mh Mbunge akiwasiliri katika uwanja akipokelewa.
 Mwenyekiti wa CCM Bukoba Mjini Yusuf Ngaiza akimkaribisha Mbunge.
 Katibu mwenezi wa ccm Bukoba Mjini Ramadhani Kambuga akiendesha ratiba.
 Kulia ni Katibu wa ccm Bukoba Mjini.
 Mwenyekiti wa bodi maji Buwasa samora Lyakulwa (kulia) akiwa na Katibu msaidizi wa ccm mkoa.
 Kamanda wa vijana UVCCM Bukoba mjini Phirbert Nyerere akiongea na wananchi.

 Vijana katika hamasa.
 Kaimu mstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba Ngalinda.
 Mwenezi wa Mkoa wa Kagera akiongea na wananchi.
 Katibu wa Mkoa ccm akiongea na wananchi.
 Bw Muganyizi.
 Wasanii waliozindua albam maalumu kwa ajiri ya mshikamano Bukoba.
 Mwenyekiti ccm Bukoba mjini Yusuf Ngaiza akizungumza na wananchi.
 Mh Mbunge akiongea na wananchi, akuzungumzi swala la hali ya usalama katika jimbo,na hasa mauaji ambayo yamekuwa yakitokea na swala la kuchoma makanisa, amewataka wananchi kushirikiana na jeshi la police kuwabaini wote wanahusika na mauaji ,kwa upande wa kuchoma makani ,Mbunge amesema  ni kitu kipya kimezuka kwa ajiri ya makusudio  fulani, lakini vyombo vya usalama wanashughulika nalo.
 Uzinduzi wa albamu ya mshikamano,mh Mbunge amewachangia milioni moja  ili ziwasaidie katika mahitaji yao.
 Bw Muganyizi akiwachangia vijana katika uzinduzi wa albamu yao.
 A lamin nae akawachangia vijana waliozindua albam yao.
Hakika ulikuwa ni mkutano mkubwa,na mwisho kabisa Balozi Kagasheki akasema yuko uwanjani katika kugombea ubunge na wananchi wasiwe na wasiwasi Bukoba ni ileile, watu ni walewale, nguvu ni ileile, na Kagasheki ni yuleyule kwa hiyo hana shaka.