Saturday, 4 April 2015

BW JULIUS RUGEMARILA ACHANGIA ZAIDI YA MILIONI 36 KATIKA KUUNGA MKONO WANANCHI KATIKA MIRADI YA MAENDELEO WILAYA YA MISSENYE .

 Bw Julius Rugemarila (mwenye suti nyeusi) akiwa na baadhi ya viongozi wakiwa katika moja ya maeneo katika jimbo la Nkenge akikagua na kujionea utekelezaji wa ilani ya ccm kaika maendeleo katika Jimbo la Nkenge,Bw Julius Rugemarila ambae ni Mjumbe wa mkutano mkuu Taifa wa ccm na mlezi wa uvccm wilaya ya Missenye amechangia vifaa kama saruji, matofali na pesa taslimu kwa ajili ya ujenzi wa madarasa, maabara na mambo mengine  vyenye thamani ya milioni 36,450.000 kwa ajili ya kusaidia wananchi kuwapunguzia kasi ya uchangiaji . Bw Julius alifanya ziara katika  jimbo la Nkenge hivi karibuni.
 Bw Julias akiongea na wananchi.
 Wananchi wakimsikiliza Bw Julius.
 Moja ya Darasa ambalo halijamaliziwa ujenzi.
 Bw Julius amesisitiza kuwa katika swala la maendeleo ya wananchi wa Nkenge kwake ni ajenda ya kudumu.
 Baadhi ya maeneo mahitaji yalikuwa ni saruji.
 Wananchi wakishuhudia.
 Maeneo mengine mahitaji ilikuwa ni matofali na saruji, bw Julius alikabidhi.
Bw Julius akiongea na wananchi mara baada ya kukamilisha ziara yake.

ALHAJ ADAM KYAMA AZIKWA NYUMBANI KANYIGO BUKOBA

Alhaj Adam Kyama amezikwa nyumbani kwake Kanyigo Kigarama na mamia ya waombolezaji waliojitokeza ,Marehemu Adam Kyama alifariki Ghafla kwenye  hospital ya Mkoa wa Kagera baada ya kupata shinikizo la damu na kupelekea kupoza upande mmoja wa mwili wake na kukimbizwa hospital na mauti kumkuta, Marehemu amestaafu utumishi wa umma mwaka 2012 baada ya kulitumikia taifa katika sekta mbalimbali serikalini.( Katika picha wa pili kulia ni shekhe mkuu wa Mkoa wa Kagera Haruna Kichwabuta akiwa na viongozi wengine wa dini.
Kushoto ni Bw Hamada Abdulnur Suleiman akiongea na wanafamilia wa marehemu.
Mjane wa maerehemu.
Mratibu wa shughuli nzima ya mazishi akitoa utaratibu.
Bw Taimul(kushoto) akiwa msibani.
Marehemu akiswaliwa.
Dua baada ya maerehemu kuswaliwa na kupelekwa kuzikwa.
Katikati bi Khadija suleiman akiwa na jamaa zake.
Innah lilah wainna lilah ihyajiun.