Thursday 2 April 2015

ZITTO KABWE NAYE ATUNGA KITABU,KIMESHEHENI MAMBO MAZITO.

ZITTO KABWE NAYE ATUNGA KITABU KAMA MAKAMBA

kitabu kinawasilisha mawazo na maoni ya ndugu Zitto Zuberi Kabwe katika sehemu mbalimbali za utendaji na siasa. Makala na hotuba zake zimeambatanishwa katika mwendelezo wa mahojiano aliyoyafanya 2012 katika mtandao wa Kijamii maarufu kama JamiiForums.

 Mahojiano yalikuwa yameambatanisha maswali zaidi ta themanini na nne(84) yakiwa yamegawanywa katika vipengele kumi na sita(16). Maswali na majibu hayo yanagusa siasa za CCM, CHADEMA na upinzani kwa ujumla huku yakigusa utendaji, Uongozi na uwajibikaji. Mwisho kabisa kitabu hiki kimeongeza kipengele kimoja ambachi ni kipya kwa mahojiano hayo yaliyokuwa yamefanywa, nacho ni hotuba aliyokuwa aisome Bungeni ili kuaga rasmi kama Mbunge wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CHADEMA.

Mahojiano, hotuba na makalahizo zinatoa taswira ya Zitto Zuberi Kabwe katika ulimwengu wa siasa huku ikileta shauku kujua endapo maisha yake mapya kwenye chama kichanga cha siasa huku ikileta shauku kujua endapo maisha yake mapya kwenye chama kichanga cha siasa ni mwisho wa Zitto Zuberi Kabwe au Mwanzo tu wa safari.

No comments:

Post a Comment