Friday 10 October 2014

BREAKING NEWS!!! MWALIMU WA SEKONDARI KAGEMU AMEUWA KWA MAPANGA KANISANI

Ili ndio eneo halisi ndani ya kanisa walipokatiwa mapanga watu hao.


Taarifa ya awali alizotoa mchungaji wa kanisa hilo ambaye amejitambulisha kwa jina moja la  FAUSTINE JOSEPH, amesema kuwa usiku saa 5, yeye alimaliza ibaada yao, ambapo mwalimu alisema kuwa hawezi kwenda nyumbani kwasababu anatokea mbali, hivyo akaamua kupumzika Kanisani na mwenzake ambaye jina lake halijafaamika aliyekatwa mguu, ndipo usiku wakavamiwa na kuawa Mwl huyo aliyekuwa anafundisha Kagemu sekondari, na aliyekuwa naye kukatwa mguu ambaye ni Temistocres.
Mchungaji  FAUSTINE JOSEPH
Mchungaji CREODWARD EDWARD, ambaye ni mwenyekiti wa makanisa ya Kipentekoste amesema wanakaa kikao na wacvhungaji wote wa makanisa ya kikristo kutoa tamko kwasababu matukio ya namna hii yamekuwa yakitokea katika makanisa yao yasiyo yakawaida na yanawasikitisha sana.
Mchungaji CREODWARD EDWARD
Polisi wamefika katika eneo hilo na kuondoka na mwili wa marehemu  pamoja na majeruhi, kwajili ya kumpeleka hospitali, na inaelezwa kuwa amelazwa katika hospitali ya mkoa ambapo wachungaji wanakuta saa5 leo kutoa tamko.

NMB YATOA MSAADA WA MADAWATI KATIKA SHULE YA MSINGI KEMONDO BUKOBA VIJIJINI

 Upungufu wa madawati katika shule za msingi na sekondari ni changamoto kubwa kwa shule nyingi hapa nchini,katika kukabiriana na tatizo hilo benki ya NMB imeliona hilo na kuweza kusaidia kwa kiasi fulani katika sekta ya elimu.kushoto ni Bw Samwel Mushote kutoka NMB kanda ya ziwa Mwanza akimkabidhi Katibu tawala wa wilaya ya Bukoba Bw Clement Ndyamukama madawati 55 yenye thamani ya shilingi milioni tano kwa ajiri ya shule ya msingi Kemondo.
 Madawati 55 yaliyotolewa na NMB
 Wanafunzi wa shule ya msingi Kemondo
 Wanafunzi wakicheza muziki
 Mgeni rasmi akiwasili
 Wananchi wa kata ya Kemondo
 Mh Diwani wa Kata ya Kemondo akifungua hafla ya kukabidhi madawati
 Meneja wa NMB tawi la Bukoba Bw Mushobozi akielezea shughuri za NMB
 Wanafunzi wakiigiza
 Mgeni rasmi akitoa hotuba

Wednesday 8 October 2014

TANGAZO,HAFRA YA AINA YAKE YA KUMSIMIKA KAMANDA MTEULE WA VIJANA KATA YA BILELE 11-10-2014 LINA'S


 Uongozi wa kata ya Bilele unawatangazia wanachama wote na wapenzi wa chama cha mapinduzi kata ya Bilele kujitokeza kwa wingi kwenye hafla ya kumsimika kamanda mteule wa kata ya Bilele Ndugu Ashiraf Kalumuna.Shughuri itaanza kuanzia saa 3.00 asubuhi kwa maandamano kuanzia ofisa ya kata Bilele kupitia maeneo mbalimbali ya kuelekea katika ukumbi wa Lina's,Katika ukumbi wa Lina's Mgeni rasmi atakuwa ni mh mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi wa Bukoba Mjini Mh Abdul Kagasheki ambae atamsimika Kamanda. Pia kutakuwa na Burudani mbalimbali na badae wageni waalikwa wote watapata chakula cha pamoja na kuburudika.KARIBUNI SANA.
Kushoto ni Mjumbe wa halmashauri kuu ya ccm Taifa wa Bukoba Mjini Mh Abdul Kagasheki ndio atakuwa mgeni rasmi na kumsimika Kamanda Mteule wa kata ya Bilele Ashiraf Kalumuna. KARIBUNI SANA.

DKT JAKAYA MRISHO KIKWETE APOKEA RASIMU YA MWISHO YA KATIBA INAYOPENDE​KEZWA OKTOBA 08,2014 – UWANJA WA JAMHURI DODOMA

 Mwenyekiti wa Bunge maalum la katiba Mhe.Samuel Sitta akikabidhi rasimu ya katiba inayopendekezwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho kikwete na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt.1mohamed Ali Shein katika hafla iliyofanyika katika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma leo.
Rais jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar, Dk. Alli Mohamed Shein wakionesha Katiba hiyo iliyopendekezwa na Bunge Maalum la Mabadiliko ya Katiba.

Monday 6 October 2014

WAISLAMU WASWALI SWALA YA IDD LHAJI MSIKITI WA BILELE BUKOBA,WAISLAMU WATAKIWA KUMCHA MWENYEZIMUNGU

 Kulia ni Mgeni rasmi Balozi Kagasheki mbunge dawa jimbo la Bukoba mjini Baada ya kutoa salamu za Idd,amewataka waislamu wapendane na kumcha mwenyezi mungu,Pia amechangia shilingi milioni kumi kwa ajili ya ujenzi wa kitegauchumi cha msikiti  Bilele unaoendea,pia Mnec wa ccm Bukoba Vijijini Nazir Karamagi alimuunga mkono Balozi Kagasheki kwa kuchangia Milioni kumi na tano.
 Msikiti wa Bilele
 Waumini
 Mwenyekiti wa Bakwata Bukoba manispaa Alhaji Kagire akitoa mkono wa Idd
 Shekhe Kakweke akitoa taarifa ya msikiti wa Bilele
 Waumini wengine waliswalia nje
 Shekhe Kichwabuta amewataka waislamu wasitumie teknologia ya mitandao kwa kutukana watu na matusi
 Mkuu wa wilaya Missenye Kanal mstaafu Njiku  nae alichangia shilingi laki tano kusaidia ujenzi wa kitega uchumi cha msikiti
 Jengo litakalokuwa la ghorofa ujenzi ukiendelea
 Mgeni rasmi akitoa salamu za Idd Balozi Kagasheki
 Kanal Njiku akitoa salamu za Idd
 Nyumbani kwa familia ya Jamal Kalumuna

jamcobukoba.blogspot.com inawatakia Idd Lhaji njema waislamu wote duniani.