Tuesday, 17 June 2014

MAHOJIANO YA MOJA KWA MOJA NA MSANII ANNA MWALAGHO KUHUSU TAMASHA LIJALO

Anna Mwalagho.
Photo Credits Anna Mwalagho Facebook page

Karibu katika mahojiano mafupi na ya moja kwa moja kati ya msanii Anna Mwalagho na Kwanza Production kwenye kipindi cha NJE-NDANI Jumamosi Juni 14, 2014.Amezungumzia tamasha kubwa linaloendelea ambalo atatumbuiza pamoja na kikundi chake kwa siku tatu.
Tamasha hilo linaandaliwa kwa ushirikiano wa watu wa Oman na maktaba ya sanaa za waAfrika hapa Washington DC
Karibu usikilize

MSANII AY NA MREMBO FARAJA KOTTA NYALANDU WATEULIWA KUWA MABALOZI WA UNICEF.

Mrembo aliyewahi kushika taji la Miss Tanzania ,Faraja Kotta Nyalandu akiwa na msanii wa muziki wa Bongo Fleva Ambwene Yesaya "AY"katika viwanja vya hosptali ya wilaya ya Hai.
Mwakilishi wa Unicef Tanzania Dk Jamal Gulaid akiwatangaza Mrembo aliyewahi kushika taji la Miss Tanzania ,Faraja Kotta Nyalandu akiwa na msanii wa muziki wa Bongo Fleva Ambwene Yesaya "AY kuwa mabalozi wa UNICEF katika kampeni ya Tokomeza Ukatili dhidi ya watoto.
Mrembo aliyewahi kushika taji la Miss Tanzania ,Faraja Kotta Nyalandu akiwa na msanii wa muziki wa Bongo Fleva Ambwene Yesaya "AY" wakati wa kutangazwa kuwa mabalozi wa UNICEF.
Mwakilishi wa Unicef Tanzania Dk Jamal Gulaid akimkabidhi barua ya uteuzi Mrembo aliyewahi kushika taji la Miss Tanzania ,Faraja Kotta Nyalandu ya kuteuliwa kuwa balozi wa UNICEF katika kampeni ya Tokomeza Ukatili dhidi ya watoto.
Mwakilishi wa Unicef Tanzania Dk Jamal Gulaid akimkabidhi barua msanii wa muziki wa Bongo Fleva Ambwene Yesaya "AY" ya kuwa balozi wa UNICEF katika kampeni ya Tokomeza Ukatili dhidi ya watoto. 

Monday, 16 June 2014

WORLD CUP 2014: GERMANY 4 - 0 PORTUGAL, THOMAS MULLER AFUNGA HAT-TRICK...PEPE ALIMWA RED CARD!

Germany V Portugal
 Thomas Muller Leo hii huko Arena Fonte Nova Jijini Salvador, Brazil, amepiga Bao 3 na kuisaidia Nchi yake kuizamisha kwa Bao 4-0 Portugal ambayo ilicheza Mtu 10 kuanzia Dakika ya 37 baada ya Pepe kupewa Kadi Nyekundu.
Hii ilikuwa ni Mechi ya kwanza kwa Timu zote mbili ambazo zipo Kundi G la Fainali za Kombe la Dunia pamoja na Ghana na USA ambao wanapambana baadae Usiku huu.
Muller alitangulia kufunga Bao lake la kwanza Dakika ya 12 kwa Penati iliyotolewa baada ya Mario Gotze kuangushwa na Joao Pereira.
Germany v PortugalMimi ndie Mwamuzi...............Haisaidii...!!! Ronaldo akilalamika kwa mwamuzi baada ya kunyimwa penati baada ya mchezaji wao kuangushwa kwenye eneo hatariGermany V PortugalKilichofata kwa Ujerumani ni kuongeza bao mbili tuu kipindi cha pili..
Mats Hummels alifunga Bao la Pili Dakika ya 32 na ndipo ikafuatia Kadi Nyekundu katika Dakika ya 37 kwa Pepe ambae alivaana na Muller na Refa kuamua ni Frikiki na yeye kumzonga Mjerumani huyo aliekuwa kakaa chini na kuinamisha kichwa chake kwake kumgusa Mullar kitendo ambacho Refa Milorad Mazic wa Serbia alichukulia kama fujo.
Kabla Haftaimu, Muller tena akapiga Bao na kuifanya Germany 3 Portugal 0.
Kipindi cha Pili, Thomas Muller akaongeza Bao lake la 3 Dakika ya 78 na Germany kushinda Bao 4-0.
Mechi inayofuata kwa Germany ni Jumamosi Juni 21 na Ghana na Portugal kucheza na USA Jumapili Juni 22.
Germany V PortugalNje!!! umejitafutia mwenyewe!!! umeskia tumekuja vitani!!Germany V Portugal Pepe akijitafuta mabaya!!!Germany V PortugalHatukuja kutalii hapa Brazil....hacha tushangilie........Germany V PortugalHummels akitupia bao la pili na kufanya 2-0Germany V PortugalThomas Muller akifunga bao la kwanza kwa mkwaju wa penati usiku huu na kuitanguliza Nchi yake kwa bao 1-0 dhidi ya PortugalGermany V PortugalMashabiki wa Ujerumani wakitokelezea....tayari kupata alama tatu muhimu usiku huu...

FAMILY DAY YA ARUSHA TECHNICAL COLLEGE YAFANA

Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha,Dk Richard Massika(wa pili kulia)akiwa na wafanyakazi wenzake kwenye mazoezi ya viungo katika viwanja vya chuo hicho.
Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha,Dk Richard Massika kulia)akiwa na wafanyakazi wenzake kwenye mazoezi ya viungo katika viwanja vya chuo hicho.

MUSOMA VETERANI MABINGWA CASTLE LAGER PERFECT SIX KANDA YA ZIWA

Afisa Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania mkoani Mwanza Liston Chale (kulia), Meneja Matukio, TBL Mwanza Eric Mwayela, na Meneja wa Bia ya Castle Lager, Kabula Nshimo wakimkabidhi Kapteni wa timu ya Musoma Veterani, Ramadhani Magoe (kushoto) kombe baada ya kutawazwa mabingwa wa fainali za Castle Lager Perfect Six kanda ya Ziwa jana baada ya timu yake kuwafunga Milango Kumi FC ya Kahama mabao 3-2 katika mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza jana. Mabingwa hao wataiwakilisha Kanda ya Ziwa kwenye fainali za taifa. Wachezaji wa Timu ya Musoma Veterani, wakishangilia na kombe lao walolipata baada ya timu hiyo kuifunga timu ya Milango Kumi FC ya Kahama magoli 3-2 na kuibuka mabingwa wa Castle Lager Perfect Six kanda ya Ziwa katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza jana.

KITOKOLOLO RAPA WA FM ACADEMIA AHAMIA BENDI YA MASHUJAA

Kitkololo akitangaza rasmi kujiunga na bendi ya Mashujaa leo kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Bw. Maximillian Luhanga. Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Bendi ya Mashujaa Bw. Maximillian Luhanga akizungumza katika mkutano huo wakati alipomtambulisha rapa Kitokololo kushoto kutoka bendi ya FM Academia kulia ni King Dodoo mshauri wa bendi hiyo. 
BENDI ya Mashujaa imemchukua rapa, Kalidjo Kitokololo ‘Kuku’ kutoka bendi ya FM Academia na kusaini naye Mkataba wa miaka miwili.
Akizungumza kwenye ukumbi wa Milenium Business Park leo , Kijitonyama, Dar es Salaam Mkurugenzi wa Mawasiliano wa bendi hiyo, Maximillian Luhanga amesema kupatikana kwa Chitokololo ni furaha kubwa kwao. “Kalidjo anakuwa rapa wa tatu katika bendi ya Mashujaa , baada ya Saulo John maaurufu Ferguson na Sauti ya Radi, ambao wote ni wakali, kwa marapa hao wote tunaamini bendi yetu itakuwa inatisha sana,”amesema Luhanga. 
Maxmilian Luhanga amesema Kitokololo anaanza kazi mara moja baada ya kusaini mkataba mpya.
Kwa upande wake, Kitokololo mwanamuziki kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) amesema amekuja Tanzania kutafuta maisha na Mashujaa imempa ofa nzuri ndiyo maana amejiunga na bendi hiyo.
Amesema ameondoka vizuri FM Academia akiwa amewaaga vizuri wenzake ambao wameridhia kuondoka kwake.
Kitokololo amesema kwamba amejiunga na Mashujaa akimfuata King Dodo ambaye kimuziki ni baba yake , King Dodoo ndiye aliyemleta nchini kwa mara ya kwanza mwaka 2004.
Mashujaa itamtambulisha rasmi mwanamuziki huyo katika onyesho maalum litakalofanyika ukumbi wa Letasi Lounge Ijumaa wiki hii. Mashujaa pia wanatarajiwa kuwa na ratiba ndefu mara baada ya mfungo mtukufu wa ramadhani ambapo Maximillian Luhanga amewaambia mashabiki wa bendi hiyo nchini kote kukaa mkao wa kula, Kwakuwa bendi hiyo itakuwa na ziara karibu mikoa yote ya Tanzania ili kutoa burudani kwa mashabiki wao.

WORLD CUP 2014: FRANCE 3 v HONDURAS 0, KARIM BENZEMA AIPA USHINDI UFARANSA USIKU HUU..AFUNGA BAO MBILI PEKE YAKE!

Karim Benzema akishangilia bao lake la tatu baada ya kuifungia timu yake France usiku huu na hata lile la kwanza na la pili likisababishwa na yeye pia..Pongezi kwake katika mtanange huu ameibeba nchi yake......
Karim BenzemaKipa wa Honduras  N. Valladares alijifunga bao baada ya Karim Benzema kuachia shuti lililogonga posti na kurudi upande wa kipa na kipa kuumalizia mpira huo ndani ya lango lake katika kipindi cha pili dakika ya 48. Dakika ya 72 Karim Benzema amewaongezea tena bao Ufaransa na goli kuwa 3-0 dhidi ya Honduras.Goalkeeper Noel Valladares of Honduras scores an own goal, France's second, as he fumbles the ball over the line during the 2014 FIFA World Cup Brazil Group E match between France and Honduras at Estadio Beira-Rio on June 15, 2014 in Porto Alegre, Brazil.Kipa wa Ufaransa akijifunga bao hapa..Karim Benzema of France looks back as goalkeeper Noel Valladares of Honduras fails to save France's second goal during the 2014 FIFA World Cup Brazil Group E match between France and Honduras at Estadio Beira-Rio on June 15, 2014 in Porto Alegre, Brazil.Unachezea mimi...utajiju!!! 2-0 kwenye neti...France players celebrate their team's second goal during the 2014 FIFA World Cup Brazil Group E match between France and Honduras at Estadio Beira-Rio on June 15, 2014 in Porto Alegre, Brazil.Raha ya ushindi ndio hii...Wachezaji wa Ufaransa wakipongezana 
France wanapata bao kwa mkwaju wa penati na mchezaji wa Honduras W. Palacios anatolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumsukuma mchezaji wa Ufaransa Pogba kwenye eneo hatari la kipa. Wilson Palacios of Honduras is shown a red card by referee Sandro Ricci during the 2014 FIFA World Cup Brazil Group E match between France and Honduras at Estadio Beira-Rio on June 15, 2014 in Porto Alegre, Brazil.
Karim Benzema anaifungia bao hilo kwa mkwaju wa penati katika dakika za mwishoni mwa kipindi cha kwanza katika dakika ya 45. Ufaransa wanaenda mapumziko wakiwa mbele ya bao 1-0 dhidi ya Honduras.Patashika za hapa na pale zilitokea baada ya mchezaji wa Honduras kumfanyia rafu mbaya PogbaKarim Benzema of France shoots and scores his team's first goal on a penalty kick during the 2014 FIFA World Cup Brazil Group E match between France and Honduras at Estadio Beira-Rio on June 15, 2014 in Porto Alegre, Brazil.Karim akichonga penati...na kuitangulia mapema Ufaransa bao 1-0......Karim Benzema of France celebrates scoring his team's first goal on a penalty kick during the 2014 FIFA World Cup Brazil Group E match between France and Honduras at Estadio Beira-Rio on June 15, 2014 in Porto Alegre, Brazil.Karim Benzema akishangilia bao alilolifunga kwa mkwaju wa penatiPaul Pogba of France battles for the ball with Wilson Palacios of Honduras during the 2014 FIFA World Cup Brazil Group E match between France and Honduras at Estadio Beira-Rio on June 15, 2014 in Porto Alegre, Brazil.Pogba chini Mchezaji wa Honduras Wilson Palacios huku mwamuzi akiwa na yeye!Patrice Evra of France lies on the field as teammates Antoine Griezmann (2nd L) and Karim Benzema look on with referee Sandro Ricci during the 2014 FIFA World Cup Brazil Group E match between France and Honduras at Estadio Beira-Rio on June 15, 2014 in Porto Alegre, Brazil.Mchezaji wa Ufaransa Evra chini...chali!!France pose for a team photo prior to the 2014 FIFA World Cup Brazil Group E match between France and Honduras at Estadio Beira-Rio on June 15, 2014 in Porto Alegre, Brazil. Kikosi cha FranceHonduras pose for a team photo prior to the 2014 FIFA World Cup Brazil Group E match between France and Honduras at Estadio Beira-Rio on June 15, 2014 in Porto Alegre, Brazil.Kikosi cha Honduras
Mashabiki wa France wakitokelezea usiku huu wakati wa timu yao wa Taifa ikichuana na HondurasFrance shirts hang in the dressing room prior to the 2014 FIFA World Cup Brazil Group E match between France and Honduras at Estadio Beira-Rio
VIKOSI:
France:
 Lloris, Debuchy, Varane, Sakho, Evra, Pogba, Cabaye, Matuidi, Valbuena, Benzema, Griezmann.
Subs: Ruffier, Cabella, Giroud, Mavuba, Mangala, Sagna, Digne, Sissoko, Remy, Koscielny, Schneiderlin, Landreau.

Honduras: Valladares, Beckeles, Bernardez, Figueroa, Izaguirre, Najar, Wilson Palacios, Garrido, Espinoza, Bengtson, Costly. 
Subs: Lopez, Osman Chavez, Montes, Juan Garcia, Jerry Palacios, Mario Martinez, Delgado, Oscar Garcia, Rony Martinez, Claros, Marvin Chavez, Escober.
Referee: Sandro Meira Ricci (Brazil)

Sunday, 15 June 2014

NYALANDU APOKEA HELKOPTA YA KISASA KUTOKA MAREKANI ILI KUKABILIANA NA UJANGILI KATIKA HIFADHI.

Waziri wa Mali asili na Utalii, Lazaro Nyalandu (wapili kushoto) akipokea funguo ya helkopta kutoka kwa ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Helicopter Charter (EA) Ltd, Peter Achammer iliyotolewa msaada na Taasisi ya Howard Buffet kwaajili ya kusaidia mambambano dhidi ya ujangili katika hifadhi za taifa nchini. Makabidhiano hayo yalifanyika jana jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na Balozi9 wa Marekani nchini Tanzania, Mark Childress (wapili kulia) na Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii, Peter Msigwa.
Wadau mbalimbali wakipiga picha ya pamoja baada ya makabidhiano.
Waziri akipiga picha na wageni pamoja na Askari wanyama Pori