Friday 11 March 2016

KASSIMU MAJALIWA KUTUA BUKOBA JUMAPILI 13-3-2016,MONGELA AKUTANA NA WAANDISHI.ABADILISHA RATIBA GHAFLA KWA MANISPAA YA BUKOBA


 Waziri mkuu Kassimu Majaliwa anategemea kuwasili siku ya jumapili katika uwanja wa ndege wa Bukoba na kuanza ziara ya siku  tatu, Mkuu wa mkoa kagera John Mongella akiongea na waandishi wa habari alisema Mh waziri mkuu mara baada ya kuwasili atakwenda kufungua kiwada cha maji Bunena, na siku ya Jumanne kuelekea wilaya ya Missenye kutembelea Lanchi  ambazo zimekuwa kwenye mgogoro wa muda mrefu sasa, na baada ya hapo ataelekea wilaya ya Ngara,Mara baada ya taarifa hiyo,badae jioni ratiba ikabadilika ,na kutolewa maelezo mapya, mh waziri mkuu atatembelea kujionea maendeleo ya mradi wa maji  mkubwa unaoendelea kujengwa,baada ya hapo ataongea na watumishi wa manispaa ya Bukoba na Wilaya ya Bukoba kwenye ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa Kagera,na baada ya hapo atakwenda kwenye mkutano wa hadhara uwanja wa uhuru platform kuzungumza na wananchi.
 Aliesimaa ni Afisa habari ofisi ya mkuu wa Mkoa Bw Silvester akimkaribisha mkuu wa mkoa kuzungumza na waandishi.
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera  John Mongera akizungumza na waandishi.
 Msaidzi wa mkuu wa mkoa.