Na Joachim Mushi wa TBN
WAZIRI wa
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa leo
ametembelea mradi wa ujenzi wa barabara za juu unaoendelea eneo la
Tazara jijini Dar es Salaam na kuridhishwa na kasi ya ujenzi
inayoendelea chini ya Kampuni ya Sumitomo Mitsui Construction Co. Ltd ya
nchini Japan.
Akizungumza
katika ziara hiyo alisema lengo ni kuangalia maendeleo ya ujenzi wa
mradi huo ili kuhakikisha unakamilika mapema kama ulivyopangwa. Prof.
Mbarawa alisema ameridhishwa na maendeleo ya mradi huo ambao mara baada
ya kukamilika utarahisisha shughuli za usafiri kwa wananchi watumiao
barabara hizo mbili za Nyerere na Mandela jijini Dar es Salaam.
Mradi
huo wa ujenzi unatarajiwa kukamilika ifikapo Oktoba 2018 huku
ukitarajiwa kugharimu takribani shilingi bilioni 100, ambapo kati ya
fedha hizo shilingi bilioni 93.44 zitatolewa na Japan kupitia Shirika la
Ushirikiano wa Kimataifa (JICA), na Serikali ya Tanzania itatoa
shilingi Bilioni 8.3.
Mhandisi Mkazi wa Kampuni ya Sumitomo Mitsui Construction Co. Ltd
inayojenga barabara za juu eneo la Tazara, Kiyokazu Tsuji (kulia) akitoa
maelekezo kewa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame
Mbarawa (katikati) maendeleo ya daraja hilo wakati alipotembelea
kuangalia maendeleo ya mradi huo. Kushoto ni Balozi wa Japan nchini
Tanzania, Masaharu Yoshida akishuhudia.
Mhandisi Mkazi wa Kampuni ya Sumitomo Mitsui Construction Co. Ltd
inayojenga barabara za juu eneo la Tazara, Kiyokazu Tsuji (kulia)
akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame
Mbarawa (katikati) muonekano wa ramani ya daraja hilo na ujenzi
unavyoendelea wakati alipotembelea kuangalia maendeleo ya mradi huo.
Kushoto ni Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharu Yoshida
akishuhudia. Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (wa pili kushoto) akipata maelezo juu ya maendeleo ya mradi huo Muonekano wa ujenzi wa barabara za juu unaoendelea eneo la Tazara jijini Dar es Salaam. Muonekano wa ujenzi wa barabara za juu unaoendelea eneo la Tazara jijini Dar es Salaam.