Wakati
uandaaji wa onyesho la muziki la Coca-Cola Coke Studio msimu wa tano
unaendelea jijini Nairobi nchini Kenya linalojumisha kolabo za
wanamuziki wa kitanzania kwa kushirikiana na wanamuziki wa nje,
washabiki wa muziki nchini wamezisubiri kwa shauku kolabo hizo.
Burudani
za onyesho hili ambalo limepata umaarufu mkubwa nchini kutokana na
kufuatiliwa na wapenzi wengi wa muziki kupitia luninga litaanza kurushwa
mapema mwezi Septemba na kwa upande wa Tanzania wasanii ambao wako
ndani ya nyumba ni Rayvanny, Izzo Bizness na Nandy.
Katika
onyesho la Coke Studio msimu mwa mwaka jana wakali wa muziki nchini
ambao walishiriki walikuwa ni Ally Kiba,Vanessa Mdee,Ben Pol na Fid Q
ambao walishirikiana na wanamuziki Wangechi, Maurice Kirya, Victoria
Kimani na 2Face.
Katika
msimu wa Coke Studio wasanii wanaoshiriki wanatokea katika nchi za
Kenya,Afrika ya Kusini, Uganda, Tanzania, Rwanda, Ethiopia, Nigeria,
Ghana, Angola, Zimbabwe, Togo, Cote d’Ivoire, Madagascar, Mauritius,
Mozambique, DRC na Cameroon wakisindikizwa na mwanamuziki nguli wa
kimataifa kutoka nchini Marekani Jason Derulo.
Mbali
na wasanii kutoka Tanzania wakali wengine wa muziki kutoka nchi za
Afrika wanaoshiriki msimu huu ni Khaligraph Jones na Band Becca
(Kenya),Sami Dan (Ethiopia),Bebe Cool, Eddy Kenzo , Sheebah, Ykee Benda (
Uganda).
Wengine
ni Nasty C, Busiswa, Mashayabhuqe kutoka Afrika ya Kusini, Youssoupha
kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Runtown na Yemi kutoka Nigeria,
Dji Tafinha kutoka Angola, Laura Beg kutoka Mauritius,Jah Prayzah na
Slapdee kutoka Central Africa Republic,Bisa Kdei na Worlasi kutoka Ghana
Taarifa
kutoka kampuni ya Coca-Cola ambayo iliyotolewa hivi karibuni imeeleza
kuwa onyesho la Coke Studio ambalo umaarufu wake umekuwa ukiongezeka
mwaka hadi mwaka msimu huu utakuwa na burudani za aina yake kutoka
kolabo za wasanii nguli barani Afrika kuanzia Afrika Magharibi mpaka
Afrika ya Kusini na litarushwa na vituo vya luninga kwenye nchi zaidi ya
30 barani Afrika na kuzidi kuifanya Afrika izungumze lugha moja tu ya
muziki.
Imelielezea
zaidi kuwa onyesho hilo kuwa lina lengo la kukusanya pamoja wasanii na
kuonyesha uwezo na vipaji vya muziki vilivyopo Afrika ikiwemo kutoa
fursa kwa wasanii chipukizi kufanya kazi na baadhi ya wasanii na
watayarishaji wa muziki wa kimataifa,vilevile Kuwakusanya wasanii
wanaofanya aina tofauti ya muziki, wanaotoka katika nchi tofauti za
Kiafrika kuwawezesha kutengeneza sauti ya Afrika kupitia burudani ya
muziki
Msanii Rayvanny (katikati) akiwa na wasanii wenzake wakifanya moja ya Mashup hivi karibuni
Mwanamuziki Izzo Business akiwa amepozi ndani ya studio jijini Nairobi
Baadhi
ya wasanii nguli waliopo kwenye matayarisho ya Coke Studio msimu wa
tano wakiwa katika picha ya pamoja jijini Nairobi hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment