Tuesday 8 September 2015

MWILI WA MAREHEMU JOSEPH MSHUMBUSI WAWASILI DAR,KUZIKWA NYUMBANI KWAKE BUKOBA KANAZI 11-9-2015 IJUMAA.

 Mwili wa marehemu Joseph Mshumbusi umewasili Dar jana usiku tarehe 9-10-2015 Jumatano majira ya saa tatu usiku kutokea Dubai ambako mauti yalimkuta akiwa safarini akitokea Hong kong China,Marehemu Mshumbusi ataagwa na ndugu na jamaa wa Dar leo kuanzia saa saba mchana katika kanisa la Last Mt.akw Martha Mikocheni,Baada ya misa mwili utapelekwa kulala uwanja wa kimataifa Dar na siku ya Alhamisi saa tatu asubuhi mwili utapelekwa Bukoba kwa ndege ya kukodi,Kwa mujibu wa msemaji wa mipango ya mazishi ndugu Protas Ishengoma amesema marehemu Mshumbusi atazikwa siku ya Ijumaa nyumbani kwake kijiji cha Rulongo Kanazi kwa kutanguliwa na Ibada ya mazishi itakayoanza saa saba mchana,Marehemu katika uhai wake amekuwa karibu sana katika shughuli za kidini na hasa kanisa katoriki, hivyo inatarajiwa maaskofu, mapadre, waumini, na jamii kwa ujumla kujitokeza kwa wingi sana kumzika.
Marehemu Mshumbusi katika uhai wake akiwa na mkewe, Pumzika kwa amani Mzee Mshumbusi, mtu wa watu.utakumbukwa daima kwa upendo wako, utani wako, ucheshi wako, ukarimu wako katika jamii.

2 comments:

  1. Pumzika kwa amani Joseph Mushumbusi. Maishani ulipenda kusaidia watu wenye shida kwa siri bila kujulikana. Sasa Mungu akuzawadi kwa wema wako. RIP

    ReplyDelete
  2. Pumzika kwa amani Joseph Mushumbusi. Maishani ulipenda kusaidia watu wenye shida kwa siri bila kujulikana. Sasa Mungu akuzawadi kwa wema wako. RIP

    ReplyDelete