Friday, 4 October 2013

RAIS JAKAYA KIKWETE AZINDUA RASMI KIWANDA CHA BAKHRESA FOOD PRODUCTS LTD




Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa SSB Group, Said Salim Bakhresa alipofika kwenye kiwanda hicho, eneo la Mwandege katika mkoa wa Pwani leo, kwa ajili ya kukifungua rasmi. Katikati ni Mama salma Kikwete
Rais Kikwete akiwasalimia baadhi ya viongozi wa kampuni hiyo. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Pwani, Hajjat, Mwantum Mahiza.
 Rais Jakaya Kikwete akimsikiliza Said Salim Bakhresa (kulia) wakati akitoa ufafanuzi kuhusu kiwanda chake hicho kinavyopambana ana hasara inayosababishwa na kutokuwa na umeme wa Tanesco
 Mazungumzo yakiendelea kwenye ukumbi wa kiwanda hicho
 Rais Kikwete akitazama baadhi ya bidhaa za 'Malt' za kiwanda hicho
 "Naam. bidhaa hizi ni Bora", akasema Rais Kikwete
 Rais Kikwete akieleza haja ya Tanesco kuwekeza huduma zake kwenye kiwanda hicho ili kupata fedha kwa manufaa ya Shirika hilo la Umeme
 Rais Kikwete na mwenyeji wake Saidi Bakhresa wakitoka kwenye mazungumzo tayari kwa ajili ya Rais kutembelea maeneo mbalimbali ya uzalishaji kiwandani hapo
 "Unaona hukooo"  Bakhresa akimuonyesha kitu Rais Kikwete katika eneo la uzaloishaji vinywaji vya Azam Malt.




 Bidshaa zenyewe ndizo hizo....
 Rais akipata maelezo kutoka kwa mtaalam katika chumba cha maabara ya kiwanda hicho
 "tunafanya hivi halafu hivi.... kujidhirisha kuwa bidhaa ni bora anasema mtaalam

UKITAZAMA HIZI PICHA, UTAKUWA NA KILA SABABU YA KUMSHUKURU MUNGU KWA KUKUWEKA MZIMA



Stori: Imelda Mtema
HAKIKA ni mateso, tena makubwa. Mtoto Selemani Rajabu mwenye umri wa miaka 17, mkazi wa Ukonga kwa Guta, jijini Dar yuko katika mateso makali baada ya mguu wake mmoja kuvimba mithili ya tairi la gari kiasi kwamba hawezi kufanya jambo lolote zaidi ya kujiburuza tu.
Akizungumza na gazeti hili nyumbani kwao akiwa na simanzi kubwa, kijana huyo amesema kwamba anakumbuka amezaliwa akiwa na ulemavu kidogo chini ya nyayo za miguu yake ambazo zilikuwa nene kiasi cha kumfanya ashindwe kutembea na badala yake akawa ni mtu wa kutambaa tu.
Alisema wakati huo alikuwa akiishi na wazazi wake wote wawili, lakini baadaye wazazi hao walitengana na kumfanya aishi na mama yake huko Pugu Kajiungeni. Kutokana na uwezo duni wa mama yake, alimpeleka hospitali mara moja tu, licha ya mguu wake kuendelea kuvimba kila siku.
“Nakumbuka mama yangu aliwahi kunipeleka hospitali mara moja tu nilipokuwa mdogo, lakini sikumbuki kama aliwahi kunipeleka tena,” alisema Selemani akiwa na sura ya kukata tamaa.
Alisema tangu wakati huo, mguu wake uliendelea kuvimba siku hadi siku mpaka akashindwa hata kutambaa kama mwanzo na sasa akalazimika kujiburuza licha ya uzito mkubwa wa mguu wake kutokana na kuongezeka kwa uvimbe.
Kutokana na hali hiyo kuzidi kuwa mbaya, alisema mwaka jana mama yake alimpeleka Hospitali ya CCBRT ambako baada ya madaktari kumuangalia walisema mguu wake hauna maji ambayo wangeweza kuyanyonya ili kuyatumia kupata vipimo na kujua tatizo linalomsumbua.
Hata hivyo, kwa bahati mbaya, mama yake mzazi alifariki na kumlazimu baba yake kwenda kumchukua na kumpeleka kwa bibi yake huko Manzese.
“ Hali ya bibi haikuwa nzuri kiafya, hivyo baba alinichukua tena na kuishi naye kwake nikiwa na mama wa kambo,” alisema Selemani.
Mtoto huyo analalamika kuwa anatamani hata mguu wake huo ukatwe kutokana na adha anayoipata kwani anakosa raha kama watoto wengine wanaotoka nje wenyewe tofauti na yeye anayetolewa kwa kuburuzwa na watu zaidi ya wawili.
“Siku zote na raha kunapokucha najiona kama sina thamani, natamani hata mguu huu ukatwe, siwezi kufanya kitu chochote, natamani kuwa kama watoto wenzangu,” alisema.
Licha ya adha hiyo, Selemani alisema kingine kinachomuumiza ni kufanya haja zote  sehemu alipokaa na hivyo kutoa wito kwa wasamaria, akiwemo Rais Jakaya Kikwete kumsaidia ili aweze kupata matibabu.
Kwa wenye nia ya kumsaidia mtoto Selamani, kwa matibabu au chakula, wanaombwa kuwasiliana na chumba cha habari kwa simu namba 0713 612 533.

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII MH. KAGASHEKI AONGOZA MATEMBEZI YA SIKU YA TEMBO DUNIANI JIJINI ARUSHA YALIYO CHUKUA ZAIDI YA KILOMETA 4 LEO.


 Muheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Kagasheki akikata utepe kuashiria uzinduzi wa matembezi ya amani ya Tembo Duniani kupinga mauaji ya Tembo hao.
 Muheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Kagasheki akionesha moja ya vibao ambavyo vinawaonesha Tembo wakati wa Matembezi hayo ya amani.
 Kutoka kushoto ni Mrs. Tibaijuka akifuatiwa na Muheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Kagasheki,Mwenyekiti wa Tanzania Association of Tours Operators Willbert Chambulo, na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Muheshimiwa Magesa Mulongo.
 Baadhi ya Wanafunzi wakiwa katika Matembezi ya Siku ya Tembo Duniani
 Baadhi ya Wanaharakati wakiwa katika Matembezi ya siku ya Tembo Duniani
 Ma elfu ya Wananchi kutoka Arusha pamoja na wadau wengine kutoka Mikoa na nchi mbalimbali wakiwa katika Matembezi ya siku ya Tembo Duniani yaliyo Fanyika Arusha Leo
 Hawa ni Watoto Shupavu kabisa waliojitolea Mstari wa mbele katika Matembezi ya Tembo leo
 Muheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Kagasheki akisaini katika moja la bango la siku ya Tembo , ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu
 Maandamano yakiwa yanaendelea
 Wa kwanza kutoka kushoto ni Mr. Peter ambaye ndiye alikuwa katika kamati kuu ya Maandalizi ya Siku ya Matembezi ya Tembo Duniani, na pia Makamu mwenyekiti wa Tanzania Association of Tours operators akiwa katika matembezi hayo
 Muheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Kagasheki akiongoza Ma elfu ya watu wakiingia katika viwanja vya AICC ambapo ndipo ilikuwa kilele cha Matembezi hayo
 Afisa Mtendaji wa Chama cha Wakala wa Utalii TATO Ndugu Sirili Akko akitoa Maneno machache kabla ya ufunguzi Rasmi wa Kilele cha Matembezi ya Tembo Duniani.
 Meza kuu wakiongozwa na Muheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Kagasheki wa nne kutoka kushoto wakiwa wamesimama kwa mda wa dakika moja kuwakumbuka Waliokufa katika Tukio la Westgate Kenya pamoja na Tembo walio uwawa .
 Mc akiwa anaanza Tukio rasmi kwa kuwakaribisha viongozi mbalimbali kwa ajili ya Kutoa salam zao na Risala
 Dr. Alfred kikoti Akitoa Mada yake juu ya Idadi ya Tembo ambao wamebakia , pia kuelezea kutokomeza kwa Biashara haramu ya uuzaji wa uuzaji wa Meno ya Tembo, na kusisitiza Tanzania inategemea Tembo katika Utalii.
Mwenyekiti wa Tanzania Association of Tours Operators Ndugu Wilbert Chambulo akielezea juu ya kusimamisha biashara kubwa ya Meno ya tembo ambayo inaongozwa na Nchi ya China na kuziomba Nchi zengine kusimamisha Biashara hiyo Haramu .
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya  Mongela wa Arusha Akimkaribisha Muheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Muheshimiwa Magesa Mulongo akiwashukuru wananchi wa Arusha kwa kushiriki kikamilifu zoezi la matembezi ya siku ya Tembo Duniani na kumkaribisha Mgeni Rasmi Muheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Kagasheki  kutoa hotuba yake.
Muheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Kagasheki akizungumza na wanaharakati waliofika katika siku ya Matembezi ya Tembo Duniani, kwa kutoa Salamu kutoka kwa Muheshimiwa Rais Kikwete kwamba Oparesheni ta kutokomeza majangili imeanza na Haitasimama, alisisitiza kwamba Wanasheria wafunge midomo yao kuhusu kutetea haki za binadamu , Aliongeza kwamba majangili wauwawe huko huko wakikamatwa kurahisisha msongamano wa kesi mahakamani, na Mwisho aliongeza kwamba Wanasiasa wasiingilie swala hili la kupambana na ujangili.
Muheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Kagasheki akikabidhi vyeti kwa Shule Zilizo Shiriki Katika Matembezi ya Tembo Duniani
Muheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Kagasheki akipokea zawadi kutoka kwa TATO Anaye mkabidhi zawadi hiyo ni Makamu Mwenyekiti wa TATO Mr. Peter
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Magesa Mlongo akipokea zawadi kutoka TATO Anayemkabidhi ni Bi. Tibaijuka
Mkurugenzi mkuu wa Hifadhi za Taifa Ndugu. Allan Kijazi akitoa neno la Shukurani wakati wa kufunga Kilele cha siku ya Matembezi ya Tembo Duniani leo
Hawa ni Wale waliotembea katika Matembezi ya Kupinga mauaji ya Tembo Kutoka Arusha hadi Dar es salaam Mwendo wa Kilometa 650 kwa Siku 12 Kutoka kushoto ni Binti Mdogo mwenye umri wa Miaka 20 Kaptorina Manange,Mkazeni Y. Mkazeni, Rehema Y. Najema, na Livingstone Y. Mkazeni.

Maandamano haya yalitokea Jirani na Cultural Heritage Hadi Viwanja vya AICC Kijenge Jijini Arusha, Matembezi yaliyo andaliwa na Tanzania Association Tours Operators (TATO)

Tuesday, 1 October 2013

NJIA YA MAJI TAKA YAKISIWA KUWATOROSHA MAIDI WA AL SHAAAB HUKO NAIROBI


Wakati bado kuna maswali mengi kuhusu magaidi waliohusika na shambulio la Westgate kama kweli waliuawa kama isemavyo taarifa ya serikali ya Kenya, mtandao wa Mirror umetoa taarifa kuhusu tetesi za uwezekano wa magaidi hao kutorokea njia ya maji taka kutoka katika jengo hilo.
Mtandao huo umedai kuwa baadhi ya magaidi walitoroka kupitia njia ya maji taka iliyoko chini ya jengo la Westgate inayoenda kutokea katika mto Nairobi.

Kwa mujibu wa habari hiyo njia hiyo inaanzia eneo la maegesho ya magari katika jengo la Westgate na inaenda moja kwa moja kutokea katikati ya jiji la Nairobi. Magaidi hao wanahofiwa kutumia njia hiyo ya maji taka kutoroka na kuwaacha wengine wakiendelea kushambulia.

Taarifa hiyo inaendelea kudai kuwa wana usalama wanadai kuwa magaidi wa Al-shabaab walisafiri umbali wa nusu maili kwa magoti katika njia hiyo ya chini ya ardhi katika njia ya maji taka.

Chanzo kimoja kilisema “They escaped like sewer rats. The terrorists would have been able to pass through the underground tunnels at a rapid pace and surface almost unnoticed”.

Taarifa hiyo inaendelea kusema kuwa wachunguzi wa Kenya hawakuigundua njia hiyo ya kutorokea mpaka masaa 72 kupita baada ya shambulio kutokea.

Hapa ndipo inapotokea njia hiyo ya maji taka kutoka Westgate hadi katikati ya jiji la Nairobi

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU WAZEE DUNIANI NA WAZEE WA KOROGWE MKOA WA TANGA.


  Akivishwa vazi la Asili
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Wazee waliohudhuria katika sherehe za Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani, baada ya kuhutubia katika sherehe hizo zilizofanyika kwenye Uwanja wa Mandu, Korogwe Mkoani Tanga leo Okt. 01, 2013. Picha na OMR