Tuesday 25 July 2017

IRENE-SUZAN KOKWENDA AZIKWA NYUMBANI KWAO BUZI-BUGABO BUKOBA.

 Majonzi na vilio vilitawala katika familia ya Mzee Wilson Ndyamukama Ndyetabula wa Buzi Bugabo Bukoba wakati wa kuaga na kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Irene -Suzan Kokwenda(Baby Kokwenda).Marehemu alifariki 20-7-2017 jijijni Dar na kusafirishwa na kuzikwa  25-7-2017 Bukoba,Marehemu amekuwa akisumbuliwa na saratani ya titi, ameacha mtoto mmoja,katika picha kuanzia kushoto ni Bw  Edson Kamugisha kaka wa marehemu akiwa amembeba mtoto wa marehemu Dariano Deogratius Mugassa, Bi  Adventina Kagemulo ,dada wa marehemu, Bi  Juliet Kokulengya dada wa marehemu, Bw Emmanuel Rutiinwa, Bw  Oscar Omukama Mujuni, Bw  Rumanyika Rogers(wote kaka wa .marehemu.) Pumzika kwa amani Irene -Suzan Kokwenda
 Picha ya marehemu Irene -Suzan Kokwenda( Baby Kokwenda)
 Mzee  Wilson  Ndyamukama Ndyetabula(Baba mzazi wa marehemu) akiwa katika jeneza la mwanae,
 Mzee Pius Ngeze, Mwenyekiti mstaafu wa ccm Mkoa wa kagera (kushoto) akimsalimia Baba mzazi wa maremu.
 Madad, mawifi katika picha ya pamoja.
 Bi   Adventina   Kagemulo dada mlezi wa marehemu akiwa na wanae.
 Makaka wa marehemu.
 Katikati ni mtoto wa marehemu.
 Wakati wa chakula.
 Bi  Adventina Kagemulo akiwa na mme wake, walezi wa marehemu.
 Umati uliofika mazikoni.
 Ibada ya  misa ikiendelea.
 Katekista akiendelea na Ibada.
 Wanafamilia wa marehemu.
 Wanafamilia wa marehemu.
 Mwenye fimbo Mzee Faustine Kamareck katibu mstaafu ccm Mkoa wa Kagera akitoa heshima za mwisho.
  Rafiki wa marehemu  Reggie Mary akitoa heshima za mwisho.
 Mzee Pius Ngeze Mwenyekiti mstaafu ccm Mkoa wa Kagera akitoa heshima za mwisho.
 Mama  Ngeze akitoa heshima za mwisho.
 Mtoto wa marehemu akiwa kwenye jeneza la mama yake.
 Ndugu wa karibu wa marehemu wakiaga.
 Mlezi wa marehemu Bi Adventina  Kagemulo akiaga mwili wa marehemu.
 Mawifi wa marehem
 Wasaidizi wa marehemu.
jamcobukoba.blogspot.com inawapa pole sana ndugu, jamaa na marafiki wote, kwa mahitaji ya picha za mnato na video na kurushushwa katika blog yetu piga simu 0754-757157 au 0714-707027.