Saturday 2 July 2016

WANAPAMOJA GROUP WAMUAHANI MWENZAO DOTO RAMADHANI (MAMA RUBI) KWA KUFIWA NA MAMA YAKE MZAZI

 Wanachama wa umoja wa kusaidiana katika raha na shieda Pamoja group wamekwenda kumuahani mwanaumoja mwenzao Doto Ramadhani maarufu Mama Rubi aliempoteza mama yake mzazi(aliefariki) wiki moja iliyopita na kuzikwa huko mkoani Tabora,Wanapamoja group walifika nyumbani kwa mama Rubi Hamugembe Kashabo  Bukoba  na kushiriki futari kwa pamoja na baada ya hapo kukubidhi rambirambi zao.(katika picha mwenyekiti wa pamoja group wa kwanza kulia akiwa na katibu Prisilla Mwainunu wakikabidhi kiasi cha zaidi  ya shilingi milioni mbili kwa mfiwa mama Rubi mwenye ushungi wa njano) umoja huu una wanachama wasiozidi 40.
 Wanapamoja wakiwasili nyumbani kwa mama Rubi kashabo Bukoba mjini.


Daima pamoja group katika ubora wao.

MTANZANIA ALIYEIBUKA MSHINDI WA KWANZA AFRIKA NA WA SITA DUNIANI KATIKA MASHINDANO YA KUSOMA QUR-AN KWA NJIA YA TAJIWEED AWASILISHA TUNZO KWA MZEE MWINYI



Mwanazuoni kutoka Kondoa, Tanzania, Sheikh Rajay Ayub ambaye ameibuka mshindi wa kwanza Afrika na wa sita Duniani katika mashindano ya 37 ya Kimataifa ya usomaji Qur-an kwa njia ya Taj-weed, yaliyofanyika mwezi uliopita nchini Iran akikabidhi tuzo zake kwa Rais Mstaafu, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, wakati wa hafla ya kumpongeza iliyofanyika leo, kwenye Viwanja vya Makao Makuu ya Baraza la Waislam Tanzania-BAKWATA, Kinondoni, Dar es Salaam. Kulia ni Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu Aboubakary Bin Zubeir na Watatu kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kondoa, Alhaj Omary Kariati ambaye aliratibu hafla hiyo. 

Monday 27 June 2016

FAMILIA YA KALUMUNA WAFUTURISHA WANAFUNZI WA KAIZIREGE WANAOFUNGA ZAIDI YA 200

 Mwezi mtukufu wa ramadhani ukiwa umeingia katika fungu la kumi la mwisho, familia ya Kalumuna wakazi wa manispaa ya Bukoba wamefuturisha wanafunzi zaidi ya 200 wa  Kaizirege.wakati akiongea neno kwa niaba ya familia ,Jamal Kalumuna almaarufu Jamco amewasihi wanafunzi kusoma kwa bidii na kutambua gharama kubwa wanazotumia wazazi kuwasomesha, hivyo wanapaswa kusoma kwa bidii na kufauru, na mwisho amewatakia mfumgo mwema kwa siku zilizobaki.
 Jamila Jamal akihudumia watoto,
 Jamal Kalumuna (kushoto) akiwa na Ashiraf kalumuna.
 Rehema Kalumuna.
 Ashiraf Kalumuna(kushoto) akiwa na mh diwani ALMASOUD KALUMUNA
 Kalumuna's family wakiwa na watoto wakifuturu.
 Bw Jamal Kalumuna akizungumza na wanafunzi baada ya futari.
 Mh Diwani akiwa na mwananchi wake ktk kata.
 Ekotite.
 Wanafunzi wakimsiliza mwanafamilia ya Kalumuna.
 Baada ya Futari hapo, full kuchangamka.
 Mh Diwani wa kata ya Ijuganyondo akimsaidia mtoto.