Mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali imesababisha maafa makubwa ya nyumba kuezuka na mazao mbalimbali kuharibika mashambani katika kata ya Bugandika wilaya ya Missenye Mkoa wa Kagera,Upepo mkali na Mvua zilizonyesha 28-10-2017 zimeacha vilio na hali ya masikitiko kwa baadhi ya familia katika kata ya Bugandika, Hali hii inatokea baada ya siku moja kutolewa taarifa kutoka Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania kuwa vipindi vya mvua kubwa vinatarajiwa katika baadhi ya maeneo ya ukanda wa ziwa victoria na magharibi mwa nchi kwa mikoa ya Mara , Mwanza, Simiyu, Shinyanga, Geita, Kagera,Kigoma, Tabora, Katavi na Rukwa,na hali hii itatokea tarehe 28-10-2017 na 29-10-2017.
Ni vizuri kuchukua tahadhari kwa maeneo yaliyotajwa.