Thursday 17 December 2015

WILFRED MUGANYIZI RWAKATARE NA WADAU WENGINE KUFANYA KONGAMANO KUBWA KWA MAENDELEO YA BUKOBA 27-12-2015

 Mbunge wa Jimbo la Bukoba mjini Wilfred Muganyizi Rwakatare kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanaoishi Bukoba na wanaoishi nje ya Bukoba wameandaa Kongamano kubwa lakujadili dhima ya Maendeleo ya mji wa Bukoba litakolofanyika 27-12-2015 kuanzia saa 9.00 Alasili katika ukumbi wa St Thereza Bukobawakatare, Kongamano linatambulika kama BUKOBA MUNICIPAL,DEVELOPMENTAL,CONFERENCE(BUMUDECO)Mh Rwakatare ambae ndie mratibu wa Kongamano hilo amesema  shughuli zitakazofanyika na malengo yanayokusudiwa kufikiwa katika Kongamano hilo ni pamoja na kuwasilisha mpango kazi wa Mbunge na Baraza la madiwani la Manispaa ya Bukoba kwa kipindi cha mwaka 2015-2020 kama walivyoahidi wakati wa kampeni, Kubainisha fursa za biashara,uchumi na maendeleo zinazopatikana ndani ya Manispaa ya Bukoba,kupokea mada na michango kutoka kwa wanataaluma,wawekezaji na wajasiriamali mbalimbali na washiriki wa Kongamano kwa ajili ya kupeana ufahamu na uzoefu,Mh Rwakatare ameendelea kusema kuwa Kongamano hili litakuwa na watu kutoka nje ya nchi wanaBukoba na wasio wanabukoba wadau wa maendeleo,amewaomba watu wajitokeze kwa wingi kwa ajili ya kuweka mipango ya kuipeleka mbele Bukoba kwa maendeleo ya haraka,bila kujari itikadi za kisiasa Bukoba kwanza.(katika picha mmiliki wa mtandao wa jamcobukoba.blogspot.com mwenye koti la draft akifanya mahojiano na Mh Mbuge wa jimbo la Bukoba mjini Wilfred Rwakatare)
 Katika mahojiano
usikose  27-12-2015 katika Kongamano la maendeleo ya Bukoba.

Tuesday 15 December 2015

MKOMBOZI BENKI YABISHA HODI BUKOBA,ASKOFU RWOMA AWASIHI WANANCHI KUTUMIA FURSA NA MKOMBOZI BENKI.

 Mhashamu Baba Askofu Desderius Rwoma Askofu wa jimbo la Bukoba akienda kukata utepe katika mlango mkubwa wa kuingia ndani ya jengo la Mkombozi benki Tawi la Bukoba kuashiria ufunguzi rasmi wa Benki,Baba Askofu Rwoma katika hotuba yake amesema kufunguliwa Tawi la Mkombozi Benki ni matarajio yake kuwa mkombozi wa wajasilia mali wadogo,wakati  na wakubwa watawezeshwa na kupiga kasi ya maendeleo katika biashara zao kwa haraka zaidi, Pia amewataka wafanyakazi wa Tawi la Mkombozi Benki Bukoba kufanya kazi kwa weredi na kuwajari wateja kwa kuwa na lugha nzuri, nyuso za furaha, bashasha na kufanya kazi kwa uadilifu na uaminifu ili wateja waweze kutofautisha huduma za Mkombozi Benki na benki zingine.
 Muonekano wa jengo la Mkombozi Benki tawi la Bukoba, barabara ya Jamhuri mkabala na  jengo la polisi Bukoba Manispaa.
 Wafanyakazi wa Mkombozi Benki wakisalimiana na baba Askofu Rwoma.
 Ibada ya misa ya ufunguzi ikiendelea.
 Makamu mwenyekiti wa Bodi  Bw Method Kashonda akisoma hotuba  kwa niaba ya wajumbe wa bodi,  amesema anamshukuru mungu kwa mafanikio makubwa ya Mkombozi Benki iliyoanzishwa 2009 na leo linafunguliwa tawi la sita katika Mkoa wa Kagera Manispaa ya Bukoba.
 Wananchi na wadau mbalimbali waliojitokeza.
 Wafanyakazi wa Mkombozi Benki.
 Kulia ni Meneja wa tawi la Mkombozi Benki Bukoba.
 Baba Askofu Rwoma akisoma hotuba yake.
 kakau band wakitumbuiza.
 Mh Mbunge wa jimbo la Bukoba mjini Wilfred Rwakatare akitoa shukrani kwa niaba ya wananchi wa Bukoba mjini kwa ufunguzi wa Mkombozi benki .
 Mc Rutakwa akiwa kazini.
 Baba Askofu Methodius Kilain akiongea na waalikwa wakiwemo wafanyabiashara akiwaomba kuitumia Mkombozi Benki na Biashara zao ziwezi kushamiri,maana Mkombozi Benki kuna wito wa mungu ndani yake.
 Wanahabari.
 Kulia ni Mkurugenzi mtendaji Edwina  Lupemba akisalimiana na Bw Danford Mbilinyi mkurugenzi wa Umojaswitch,.
 Kulia ni Meya wa Manispaa ya Bukoba Mh Chief Kalumuna, Blogger Jamal Kalumuna na Bw Basibila.
Fika katika jengo la Mkombozi Benki tawi la Bukoba ukiwa na barua ya mwenyekiti wa mtaa inayokutambulisha, picha mbili pasportsize, na 20elfu ufunguliwe account yako.