Tuesday 26 September 2017

HONGERA FIDEL & IRENE KWA KUUACHA UKAPERA.

 Ni nyuso za furaha katika picha, Bw Fidel na Bi Irene baada ya kuwekeana mkataba mbele ya waumini katika kanisa la katoliki Cathedral Bukoba Mjini,mungu awabariki sana na awaongoze katika maisha ya ndoa. ni maisha ya raha na changamoto za hapa na pale, kikubwa kumtanguliza mungu.
jamcobukoba.blogsot.com inawatakia maisha mema ya ndoa, kwa mahitaji ya video , picha za mnato na  kurushwa kwenye blog yetu piga simu 0788-707027,0754-757157,0622-757157 au 0714-707027.

HONGERA RAYMOND NA GEORGIA KWA KUFUNGA NDOA,ILIKUWA NI SHIDAAA NDANI YA KAHAMA.

 Wahenga walinena hayawi hayawi yamekua, ni maneno yaliyotimia kwa Bw Raymond na Bi Georgia. mbele ya waumini, ndugu , jamaa  na marafiki walikula kiapo cha maisha ya uhai wao wote hapa duniani kuishi kwa raha, upendo na shida kwa kipindi cha maisha yao yote ya ndoa,vifijo, nderemo na vigeregere vilisikika kwa vujo katika kanisa Katoliki jimbo la Kahama.Hongereni sana.
JAMCOBUKOBA.BLOGSPOT.COM itaendelea kuwaletea matukio kilichoendelea ukumbini. kwa mahitaji ya video, picha za maana zenye ubora piga simu 0788-707027, 0714-707027, 0622-757157 au 0754-757157.