Saturday, 3 September 2016

ERIC NA PEACE WAACHANA NA UKAPERA,ILIKUWA BONGE LA HARUSI UKUMBI WA LINA'S BUKOBA 2-9-2016

 Eric nahaidi kuwa nawe katika shida na raha,magonjwa na afya mpaka mwisho wa maisha yangu.... Ni maneno mazuri na ya kutia faraja na kiapo yaliyotamkwa na Peace mbele ya washarika wa kanisa la KKKT Bukoba Manispaa na watu mbalimbali waliojitokeza kwa wingi kushuhudia ndoa takatifu ya Erick na Peace, Eric nae bila kusita wala kutafuna maneno kwa sauti nzito ya kiume iliyosheheni mahaaba, upendo na matumaini alitamka Peace naahaidi kuishi nawe katika maisha yangu yote kwa kukupenda, kukuhudumia na kutimiza yote unayostaili, ...Hakika ilikuwa ni shangwe, vifijo, hoihoi na nderemo pale wote walipovishana pete,Baada ya yote shughuli nzima ikaishia kwenye kiwanja cha maraha Lina's . Chini ya mshereheshaji (MC) Peter kutoka jijini Dar ambae hana maneno mengi ya kuchosha wageni, akifanya kazi yake kwa kujiamini aliendeleza mtanange, hakika ilikuwa ni sherehe iliyopangwa na kupangika chini ya mwenyekiti wa sherehe Mh Denis na wajumbe wake wote,sherehe ilihudhuliwa na watu mbalimbali wakiwemo majaji, msajili, mahakimu, wanasheria wa serikali , mawakili wa kujitegemea, ndugu, jamaa na marafiki, jamcobukoba.blogspot.com inawatakia maisha mema maharusi.
 Ni eneo la walkgard Transt, eneo hili lilitumika kwa picha za maharusi.
 Mh Mwakyaba akiwa akiwa na furaha kwenye msafara wa maharusi.
 Ni moja ya pozz kati ya nyingi.
 Matron na patron katika ubora wao.
 Kama hutaki unaacha, aisee ni shidaaaa.
 Eric walayaaaaa.....
 Hata siamini , leo tumekuwa mwili mmoja, asante mungu...
 Lalaaa mama kwa raha zako.
 Shuguli ikaamia ukumbini, kamati ya makaribisho wakiwa kazini.
 Kulia ni kijana mdogo machachali sana Mc Peter kutoka Dar akiwa na mwenyekiti wa sherehe Mh Denis.
 Moja ya bango kubwa kwa ajili ya kupigia picha , vitu hivi vinapatikana Jamco video production wapigie 0754-757157.
 Dada Eliza nae akapata picha ya ukombusho.
 Moja ya sifa katika kamati ya makaribisho ni kuwa na mvuto na bashasha, macho ya kuita ili mtu aitike, hakika kwa hapa walipatia.
 Mc Pete akifanya yake, maneno kidogo, vitendo zaidi  mpigie 0755- 182300 au 0653-567884.
 Mc Kuwa smart katika shughuli za watu ni muhimu.
 Kwa upande wa keki mama Simeo alihusika.
 Sherehe ni furaha.
 Kulia Mh Jaji akisalimiana na Bw Kamuntu.
 Waalikwa.
 Kibeta one, wasanii.
 Maharusi.
 Hapana chezea Bw harusi anayaweza...
 Baba wa bi harusi.
 Mama wa bi harusi.
 Kamati.
 Kushoto mama Simeo, mtaalamu wa keki akiwa na Bi Goodselda.
 Mstahiki Meya Manispaa Bukoba Chief Kalumuna akiendelea kutoa huduma ya vinywaji kwa wageni waalikwa.
 Kulia MH Msajili akiwa na Jaji.
 Mr & mRS Matete wakili msomi na mahili wa kujitegemea.
 Mh Bagenda , Bw harusi mtarajiwa akiwa na Bi harusi mtarajiwa
 Mh Katika ubora wake.
 Wafanyakazi mahakama ya mwanzo Bukoba mjini katika ubora wao wakienda kupokea keki.
 Mh Ishebakaki akipokea keki.
 Wafanyakazi mahakama kuu na Mkoa wakipokea keki.
 Vijana machachari sana kakau Bendi.
 Mwenyekiti Mh Denis akipokea keki ya kamati.
 Katika mapambo mama Matungwa kama kawaida yake, viwango vinajionyesha, mpigie bei ni kulingana na uwezo wako 0754-630900.
Kakau bendi wakifanya vitu vyao.
jamcobukoba.blogspot.com inawatakia heri na fanaka Mr &Mrs Eric katika maisha yenu ya ndoa, ukihitaji tukio lako lirushwe usisite kututafuta kwa namba 0754 757157, 0788-707027 au 0714-707027.