Monday 29 August 2016

KANISA LA KIGANGO BUGANDIKA LAZINDULIWA RASMI,WANABUGANDIKA WAMUOMBA BABA ASKOFU KUWAPA PAROKIA.

 Ilikuwa ni shangwe, hoihoi, nderemo na vifijo katika parokia ya Mugana kigango cha Bugandika baada ya kukamilisha ujenzi wa kanisa kubwa na la kisasa, mgeni rasmi katika sherehe ya ufunguzi wa kanisa alikuwa ni muashamu Baba Askofu Deziderius Rwoma wa jimbo katoliki la Bukoba.Waumini kutoka maeneo mbalimbali walimiminilka kushuhudia tukio kubwa na la aina yake katika kigango cha Bugandika,tukio hilo lilitanguliwa na ibada takatifu ya ufunguzi  wa kanisa na badae ubatizo waumini zaidi ya mia nne,baada ya ibada ya ubatizo waumini wote walipata chakula na vinywaji,Hakika mambo yalizidi kunoga, pale ukumbi ulipobadilika na kujielekeza kwenye burudani  na risala mbalimbali kusomwa  na kutambua watu ambao kwa kiasi kikubwa wamefanikisha kukamilisha ujenzi wa kanisa,Ndipo baba parokia ya mugana padre Godwin Rugumbwa aliposimama na kutamka kuwa kipekee kabisa naomba kutambua uwepo wa mwakilishi wa mfadhili wetu mkubwa Justin Lambert asimame atoe neno,Akasimama Bw Kashasha alianza kwa kuwapongeza kwa tukio la kihistoria na kubwa,nanukuu..(Naomba niongee yale niliyotumwa na Bw Justin Lambert, alipenda awepo leo hapa, lakini yupo nje ya nchi, amenituma na kuniomba nimuwakilishe, anawasalimu sana na kuwapongeza kwa tukio hili la leo la ufunguzi wa kanisa,amesema ataendelea kushirikiana na nyi siku zote, naomba nikabidhi hundi.)Hundi hiyo ya kiasi cha shilingi milioni tano kwa ajili ya kutengeneza benchi nzuri kwa ajili ya kutumika kanisani,Bw Kashasha yeye binafsi alichangia kiasi cha shilingi milioni mbili na kuhaidi kuleta vyombo vya matangazo kanisani kabla ya chrismas ya mwaka huu, kanisa limeghalimu zaidi ya milioni 150 mpaka kukamilika,na sasa umeanza mchakato wa ujenzi wa nyumba kubwa kwa ajili ya mapadre inayohitaji milioni 200,Baba Askofu Deziderius Rwoma wakati wa kuongea na waumini aliwashukuru wote waliochangia kidogo na kikubwa mpaka kukamilisha ujenzi wa kanisa, pia alitumia nafasi hiyo kujibu baadhi ya maombi mbalimbali likiwemo la Bugandika kuwa parokia, ilo alisema siwezi kulitolea majibu leo, ila litafanyiwa kazi, wakati mkiendelea na mchakato wa kujenga nyumba ya mapadre.
 Muonekana wa Kanisa la kigango Bugandika.
 Kulia ni Mama mzazi wa mmoja wa wafadhili wakubwa wa kigango Bugandika mama mzazi wa Justin Lambert.
 Kushoto Bw  Kashasha akiwa na mzee Lambert  Rweimbao.
 Waalikwa
 Wanakwaya kigango cha Bugandika.
Wana kipaimara.
 Ibada ya misa ikianza.
 Mapadre.
 Kanisa likifunguliwa rasmi.
 Kwa ndani kanisani.
 Kakau bendi

No comments:

Post a Comment