Thursday 24 October 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWASILI MKOANI KIGOMA KUZINDUA KIVUKO KIPYA CHA MV MALAGALASI WILAYANI UVINZA KESHO.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Kigoma wakati walipokuwa wakimpokea kwenye Uwanja wa Ndege wa Kigoma leo mchana. Makamu amewasili mkoani Kigoma leo kwa ajili ya kuzindua Kivuko kipya cha Malagalasi katika Wilaya ya Uvinza kesho. Picha na OMR.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia burudani ya ngoma za asili kutoka kwa wakazi wa Mkoa wa Kigoma, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kigoma leo mchana, kwa ajili ya kuzindua Kivuko kipya cha Mv Malagalasi kesho katika Wilaya ya Uvinza.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia burudani ya ngoma za asili na kumpongeza mmoja wa wasanii hao wakazi wa Mkoa wa Kigoma, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kigoma leo mchana, kwa ajili ya kuzindua Kivuko kipya cha Mv Malagalasi kesho katika Wilaya ya Uvinza.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza baada ya kukabidhiwa ripoti ya Mkoa wa Kigoma leo mchana.

CHAMA CHA WAPISHI CHAANDAA TAMASHA KWA WATOTO YATIMA


Baadhi ya wapishi katika hotel maarufu jijini Arusha wakiwa wanajadiliana wakati Tamasha la watoto yatima na walemavu wa viungo likiwa linaendelea ambapo siku hiyo ilikuwa imeandaliwa na chama cha wapishi duniani lengo ni kuwaleta pamoja watoto.

Watoto waliofika katika tamasha hilo ambapo zaidi ya watoto 300 walishiriki kutoka sehemu mbalimbali jijini Arusha

Mtoto Daudi Izrael Mshana mwenye ulemavu wa utindio wa ubongo(12)akiwa amepakatwa na mama yake Belinda Izrael katika tamasha la watoto katika hotel ya Mt.Meru jijini Arusha

Watoto wakiwa wanaimba nyimbo ya huzuni iliyokuwa imebeba ujumbe kuhusu watoto yatima

.Mustapha na Ibraa Mhinda ni watoto waliokuja kujumuika pamoja na watoto yatima ambapo kwa nyakati tofauti walitoa rai kwa jamii kuwathamini watoto wanaoishi katika mazingira magumu ikiwa ni pamoja na kuwapa mapenzi mema,malazi,mavazi,elimu na chakula bora

.Chef Tom akiwa anaongelea juu ya tamasha hilo na vyombo vya habari ambapo alisema kuwa jamii imesahau kwa kiasi kikubwa watoto wanaoishi katika vituo vya kulelea watoto yatima pamoja na walemavu

Kushoto Mkurugenzi wa Bearfoot entainment Dorothy Mustapha akiwa anawakabidhi msaada wasimamizi wa vituo vya watoto yatima

Picha ikimuonyesha msemaji wa World Chef day Chef Method Mrosso akiwa anawakatia keki watoto wanaoishi katika mazingira magumu,mwishoni mwa wiki jijini Arusha katika hotel ya Mt.Meru siku ambayo chama cha wapishi duniani hujutolea kwa kuwapikia na kula pamoja

.Baadhi ya wapishi wakiwa katika picha ya pamoja .(Picha zote na Pamela Mollel wa jamiiblog.co.tz)

RITA KUONGEZA IDADI YA WANANCHI WALIOSAJILIWA NA KUPATA VYETI VYA KUZALIWA NCHINI


Meneja Masoko na Mawasiliano toka Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini(RITA) Bw. Josephat Kimaro akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu mikakati ya wakala hao ya kuongeza idadi ya wananchi waliosajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa nchini, wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Afisa Habari wa Idara ya Habari(MAELEZO) Bi.Georgina Misama.

Wakili wa Serikali toka Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) Bi.Patricia Mpuya akifafanua kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu maboresho ya sheria ya Usajili wa vizazi na Vifo itakayowezesha kusogeza huduma za upatikanaji vyeti vya kuzaliwa karibu na maeneo ya wananchi, wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam
Picha na Eliphace Marwa-MAELEZO.

Monday 21 October 2013

MAKAMU WA RAIS DK. BILAL AFUNGUA MKUTANO MKUU WA 21 WA SABA

IMG_8257
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua mkutano mkuu wa 21 wa Vyombo vya Habari na Utangazaji kwa nchi za Kusini mwa Afrika (SABA) katika ukumbi wa A I C C jijini Arusha leo 21 Oktoba 2013.  IMG_8240
Baadhi ya washiriki wa mkutano mkuu wa 21 wa Vyombo vya Habari na Utangazaji kwa nchi za Kusini mwa Afrika (SABA) wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt Mohammed Gharib Bilal, alipokua akifungua mkutano huo leo Oktoba 21 2013 katika ukumbi wa A I C C jijini Arusha. IMG_8287
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na wasanii wa ngoma ya kimasai waliokua wakitumbiza  nje ya ukumbi wa mikutano wa A I C C jijini Arusha, baada ya kufungua  mkutano mkuu wa 21 wa Vyombo vya Habari na Utangazaji kwa nchi za Kusini mwa Afrika (SABA) leo 21 Oktoba 2013.

DK. SHEIN AFUNGUA SEMINA YA WATENDAJI WA CCM, DODOMA

 


1
Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, akifungua semina ya mafunzo ya siku nne kwa Watendaji na viongozi wa CCM ngazi za mikoa na wilaya nchini, katika jengo la White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma leo, Oktoba 21, 2013. Wapili kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (zanzibar) Vuai Ali Vuai.
2 .
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitoa maelezo kuhusu lengo la mafunzo hayo.3
Katibu wa NEC, Itikasi na Uenezi Nape Nnauye akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Kartibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kuzungumza  kwenye semina hiyo. 4
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpokea Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Dk. Ali Mohamed Shein alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Dodoma, leo kwa ajili ya kufungua semina hiyo. 5
Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein mara baada ya kuwasili katika ukumbini kwa ajili ya kufungua semina ya mafunzo kwa watendaji na viongozi wa CCM ngazi za mikoa na wilaya, leo kwenye Jengo la White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba, na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa. 6
Wajumbe wakishangilia, Dk. Shein alipowasili ukumbini. Washiriki wa semina hiyo wakiwa ukumbini

CATHERINE FOUNDATION YAZINDULIWA RASMI


 Mwemyekiti wa Taasisi ya Catherine Foundation ambaye pia ni Mbunge wa viti Maalum UVCCM Arusha, Catherine Magige akizungumza wakati wa uzinduzi wa taasisi yake uliofanyika hivi karibuni jijini Arusha.

Catherine Foundation ni taasisi isyofungamana na upande wowote na inatoa huduma za kijamii kwa makundi mbalimbali yakiwapo ya Vijana, watoto na wanawake wajane
 Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki akizungumza wakati akizundua rasmi taasisi ya Catherine Foundation.
 Mbali na uzinduzi huo Catherine Foundation ilitoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watu wenye uhitaji maalum.

AJALI MBAYA YATOKEA TENA MKOANI MBEYA


GARI AINA YA SUZUKI NA NISSAN ZIMEGONGANA USO KWA USO MAENEO YA IWAMBI JIJINI MBEYA MCHANA WA LEO KISA CHA AJALI HIYO MAPAKA SASA HAKIJAJULIKANA