Friday, 8 November 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHUDHURIA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA SABA YA SIKU YA MLIPAKODI,JIJINI DAR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti na zawadi, mshindi wa kwanza kwa kulipa kodi, Meneje wa Huduma za Fedha wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Alois Qande Maleck, wakati wa Sherehe za maadhimisho ya Saba ya Siku ya Mlipakodi, zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, leo Okt 8, 2013. Kulia ni Naibu Waziri wa Fedha, Janeth Mbene.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akihutubia wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Saba ya Siku ya Mlipakodi, zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam,leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti na zawadi, mshindi wa pili kwa kulipa kodi,Mwakilishi wa Kampuni ya Sigara Tanzania, Paul Makanza, wakati wa Sherehe za maadhimisho ya Saba ya Siku ya Mlipakodi, zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, leo Okt 8, 2013. Kulia ni Naibu Waziri wa Fedha, Janeth Mbene.
 Mshana akipokea Tuzo na Cheti kwa niaba ya Jukwaa la Wahariri.
 Baadhi ya wananchi na walipakodi waliohudhuria sherehe hizo wakimsikiliza Makamu wa Rais.
 Baadhi ya wananchi na walipakodi waliohudhuria sherehe hizo wakimsikiliza Makamu wa Rais.
 Mwakilishi wa Taasisi ya Polisi, akipokea tuzo na Cheti.......
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Harry Kitilya, akimkabidhi Tuzo na Cheti, Mwananchi Shujaa wa Kodi, Dkt. Shumba, aliyediriki kuwekwa ndani kwa kudai Risiti ya malipo yake ya chumba cha Hoteli katika moja ya hotel katika mikoa ya Tanzania Bara, wakati wa Sherehe za maadhimisho ya Saba ya Siku ya Mlipakodi, zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, leo.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Harry Kitilya, akimkabidhi zawadi na Cheti, Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Kibasila, Ally Mshana, wakati wa Sherehe za maadhimisho ya Saba ya Siku ya Mlipakodi, zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, leo.

Daktari mstaafu hosptali ya Mawenzi akamatwa kujihusisha na utoaji Mimba.



 

 Askari polisi wakiwa na silaha wakiwa wamezingira nyumba iliyokuwa
ikitumika kwa shughuli za kutolea Mimba.
  Daktari mstaafu wa hosptali ya rufaa ya Mawenzi Frances Shayo akiwa
mikononi mwa polisi muda mfupi baada ya kumkamata akitaka kuwatoa
mimba wasichana wawili.

MAJANGA MAPATO LIGI KUU, JKT RUVU NA COASTAL ZAINGIZA LAKI 2, KILA KLABU YAPATA ELFU 39

MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya wenyeji JKT Ruvu na Coastal Union ya Tanga iliyochezwa juzi (Novemba 6 mwaka huu) Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam imeingiza sh. 201,000.
JKT Ruvu iliibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mechi hiyo namba 85 na kushuhudiwa na watazamaji 67 waliokata tiketi kwa viingilio vya sh. 3,000 na 10,000.
Kila klabu ilipata mgawo wa sh. 39,010 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 30,661.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 19,835, tiketi sh. 38,100, gharama za mechi sh. 11,901, Bodi ya Ligi sh. 11,901, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 5,950 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 4,628.
Nayo mechi kati ya Ashanti United na Simba iliyochezwa juzi Uwanja wa Taifa imeingiza sh. 24,931,000 ambapo kila klabu ilipata mgawo wa sh. 5,333,590.

Wakati huo huo, mechi za jana (Novemba 7 mwaka huu) kati ya Yanga na Oljoro imeingiza sh. 34,902,000 kutokana na watazamaji 6,045 ambapo kila klabu imepata sh. 7,812,477.95. Mechi ya Azam na Mbeya City iliyochezwa Azam Complex yenyewe imeingiza sh. 15,973,000 kwa watazamaji 4,857 na kila klabu imepata sh. 3,953,162.

HATIMAYE PENNY ASALIMU AMRI KWA MTOTO WA SEPETU


 MTANGAZAJI wa Kituo cha Televisheni cha DTV, Peniela Mwingilwa ‘Penny’, ambaye ni mpenzi wa mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amesema yupo tayari kuchangia mapenzi na msichana mwingine yeyote ambaye atachukuliwa na mwanaume huyo anayempenda.
Penny, chaguo la mama mzazi wa staa huyo wa kibao cha My Number One, aliliambia gazeti hili maneno hayo, yanayotafsiriwa kama yupo tayari kuchangia mapenzi na hasimu wake, Wema Sepetu ambaye amerejesha uhusiano wake wa kimapenzi na mwimbaji huyo mpenda vidosho.

“Ninampenda Diamond na sitaki kumpoteza. Nia yangu ni kumuona akiwa na furaha. Kama Diamond anaona kuna msichana mwingine wa kutoka naye na kwake hilo linampa furaha, basi mimi sina matatizo kwa sababu ninataka awe na furaha, nitaendelea kuwa naye,” alisema Penny.
Kumekuwa na habari zisizo shaka kwamba Diamond na Wema wamerejesha uhusiano wao na hivi karibuni walitupia picha katika mitandao ya kijamii zilizowaonyesha wawili hao wakiwa katika mapozi ya kimahaba huko Ughaibuni.

Ingawa bado Diamond anatoka na Penny, lakini kwa siku za karibuni amekuwa karibu zaidi na mrembo huyo aliyetwaa taji la Miss Tanzania mwaka
 
Nasibu Abdul ‘Diamond’.

Thursday, 7 November 2013

*RAIS JAKAYA KIKWETE ALIHUTUBUA TAIFA KUPITIA BUNGE MJINI DODOMA LEO

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akilihutubia Bunge mjini Dodoma leo.
Rais Jakaya Kikwete akiendelea kulihutubia Bunge..........
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Mohammed Gharib Bilal,akiwasili katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo kusikiliza Hotuba ya Rais.
 ************************************************
Mheshimiwa Anne Makinda, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
 Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi;
Mheshimiwa Mizengo Pinda, Waziri Mkuu;
Waheshimiwa Mawaziri na Naibu Mawaziri;
Mheshimiwa Freeman Mbowe, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni;
Waheshimiwa Wabunge;
Mabibi na Mabwana;

          Nakushukuru sana Mheshimiwa Spika kwa kukubali ombi langu na kutenga muda wenu ili niweze kuzungumza na Wabunge wa Bunge lako Tukufu kuhusu masuala muhimu kwa uhai, ustawi na maendeleo ya nchi yetu na watu wake.
Mheshimiwa Spika;
          Nimeambiwa kuwa taarifa ilipotolewa kuwa ninaomba kuja kuzungumza na Waheshimiwa Wabunge, kumekuwepo na dhana mbalimbali.  Wapo waliodhani kuwa nakuja kuzungumzia mchakato wa kuunda Katiba mpya na hasa matukio ya wiki chache zilizopita.   Wapo waliodhani nakuja kuzungumzia “Operesheni Tokomeza”.  Tena wapo waliokwenda mbali na kufikiria kuwa nakuja kuwakaripia Waheshimiwa Wabunge waliotoa maoni yao kuelezea kasoro zilizojitokeza katika utekelezaji wa Operesheni hii muhimu. Na wapo pia waliodhani ninakuja kuzungumzia ushiriki wa majeshi yetu ya Tanzania katika Jeshi la Kulinda Amani la Umoja wa Mataifa nchini Kongo.

Mheshimiwa Spika;
          Hayo si makusudio yangu.  Kinachonileta mbele ya Bunge lako Tukufu ni kuzungumzia Jumuiya ya Afrika Mashariki na mustakabali wa Tanzania katika Jumuiya hiyo.  Lakini, kwa sababu ya umuhimu wa masuala hayo niliyoyataja na rai niliyopewa kuwa niyasemee japo kidogo.  Nimeona ni vyema nifanye hivyo.
Mheshimiwa Spika;
  Kuhusu mchakato wa Katiba mpya, napenda kusema kuwa tumefikia hatua nzuri katika utekelezaji wake.  Kama mjuavyo Tume ya Mabadiliko ya Katiba imekamilisha, kwa mafanikio, hatua ya mwanzo ya kusikiliza maoni ya wananchi kuhusu Katiba wanayoitaka.  Pia walishatoa Rasimu ya Kwanza ya Katiba na kukamilisha mchakato wa Mabaraza ya Katiba.  Kinachosubiriwa kwa hamu na sisi wote, ni Rasimu ya Pili ya Katiba ambayo inatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 15 Desemba 2013 au kabla ya hapo.
Mheshimiwa Spika;
          Kwa upande wa Bunge lako Tukufu, tunategemea kupata mambo mawili kutoka kwenu yatakayowezesha mchakato kutekelezwa vizuri katika hatua zinazofuata.  Jambo la kwanza ni kutungwa kwa Sheria ya Kura ya Maoni na pili kufanyika kwa marekebisho ya nyongeza ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kuhusu Bunge Maalum ili kuboresha utekelezaji wake. Baada ya Bunge kukamilisha kazi yake hiyo itafuatia uteuzi wa Wajumbe wa Bunge Maalum ili kazi ya kujadili Rasimu ya Pili ya Katiba ifanyike na kutupatia Rasimu ya Mwisho. Rasimu ambayo ikikubaliwa na wananchi katika Kura ya Maoni itakayofanyika wakati wo wote mwakani, tutakuwa tumepata Katiba Mpya.  Hivi sasa katika Serikali tunaendelea kufanya tafakuri na tunachukua hatua za kuwezesha Bunge Maalum na Kura ya Maoni kufanyika kwa mafanikio.

Operesheni Tokomeza
Mheshimiwa Spika;
          Napenda kuwahakikishia Waheshimiwa Wabunge wa Bunge lako Tukufu kuwa sikukasirishwa na maoni yao kuhusu madai ya kuwepo kasoro katika utekelezaji wa Operesheni Tokomeza. Shabaha ya Operesheni hii ni kuokoa maliasili za misitu na wanyamapori dhidi ya uvunaji haramu ambao umefikia kiwango kinachotishia kutoweka kwa raslimali hizo.  Kwa kweli hali inatisha.  Miti inakwisha na ndovu na faru wanaangamia. KUSOMA ZAIDI HOTUBA HII BOFYA READ MORE

*DJ RANKEEM RAMADHAN AZIKWA JIJINI DAR LEO


Waumini wa Kiislam na Wadau mbali mbali wakishirikiana kubeba mwili wa Marehemu RanKeem Ramadhan wakati wa Safari yake ya Mwisho kuelekea kwenye makaburi ya Sinza, Jijini Dar es Salaam jioni hii.
Waumini wa Kiislam na Wadau mbali mbali wakiwa wamekusanyika kwenye mazishi ya Marehemu RanKeem Ramadhan yaliyofanyka kwenye makaburi ya Sinza, Jijini Dar es Salaam jioni hii.
Mwili wa Marehemu RanKeem Ramadhan ukifikishwa kwenye Nyumba yake ya Milele. Mungu iweke roho ya marehemu Rankeem Ramadhan,mahali pepa peponi Amina.

YANGA HESABU ZIMETIMIA, WAONGOZA LIGI KWA KUITANDIKA OLJORO TATU, MBEYA CITY, AZAM SARE


Mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete akifunga bao la pili katika mchezo wao dhidi ya JKT Oljoro

HESABU zilizokuwa zikipigwa na wachezaji, viongozi, benchi la ufundi na mashabiki wa Yanga, zimetimia na kufanikiwa kuongoza Ligi Kuu Tanzania Bara katika mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo.
Yanga walikuwa wakihitaji ushindi katika mchezo wao dhidi ya Oljoro huku ikitaka mchezo kati ya Mbeya City na Azam uliochezwa Chamanzi umalizuike kwa sare na hayo ndiyo yaliyotokea katika mchezo huo.
Mabao matatu yaliyofungwa na Simon Msuva dakika ya 23 na Mrisho Ngassa dakika ya 30 na lile la tatu lililofungwa na Jerry Tegete yalitosha kuifanya Yanga imalize mzunguko wa kwanza ikiwa kileleni baada ya kutimiza pointi 28 baada ya kucheza michezo 13. 

Katika mchezo wa Chamanzi Azam walilazimishwa sare na Mbeya City ya mabao 3-3 na kuifungulia njia Yanga kukaa kileleni baada ya kuwazidi kwa pointi mbili.
Azam na Mbeya City ambao walikuwa kileleni kwa pointi 26 na sare hiyo timu zote sasa zimefikiwa pointi 27 huku Azam wakiwa nafasi ya pili wakati Mbeya itakuwa nafasi ya tatu kwa tofauti na mabao ya kufunga na kufungwa.

Nafasi ya nne katika msimamo wa ligi hiyo inashikiliwa na Simba wenye pointi 24 baada ya kushinda mchezo wake wa jana dhidi ya Ashanti United.

AIRTEL SHULE YETU YAFAGILIWA NA WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI ILULU -LINDI ,



 Meneja masoko wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kanda ya kusini na mkoa wa Morogoro Aminata Keita akikabidhi baadhi ya Vitabu vilivyotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa Salma Hamisi ambaye ni mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Ilulu iliyopo mkoani Lindi. Airtel ilitoa vitabu  vyenye thamani ya shilingi Milioni tano kwa shule hiyo.
 Meneja masoko wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kanda ya kusini na mkoa wa Morogoro Aminata Keita akimkabidhi Bernard Swai ambaye ni mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Chalinze. Airtel ilitoa vitabu vyenye thamani ya shilingi milioni tano kwa shule hiyo.
 Meneja masoko wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kanda ya kusini na mkoa wa Morogoro Aminata Keita akimkabidhi Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule ya sekondari ya Chalinze iliyopo mkoani Pwani baadhi ya vitabu vilivyotolewa na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa shule ya sekondari Chalinze. Wanaoshuhudia katikati ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Bw. Emmanuel Kahabi pamoja na msimamizi wa bodi ya shule hiyo Bw. Mzee Madeni.
Meneja masoko wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kanda ya kusini na mkoa wa Morogoro Aminata Keita akiwaelekeza jambo watoto wa shule ya sekondari Nanyamba iliyopo Mkoani Mtwara ikiwa ni muda mfupi baada ya kampuni ya mitandao ya simu za mkononi Airtel kukabidhi vitabu vyenye thamani ya shilingi milioni tano kwa shule hiyo ya sekondari.
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Ilulu iliyoko wilayani Kilwa mkoani Lindi,wameishukuru kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kuwapatia msaada wa vitabu vya masomo ya sayansi vyenye thamani ya shilingi milioni tano.

Wakizungumza shuleni hapo mara baada ya kupokea msaada huo wanafunzi hao wamesema kwamba wanafunzi wasichana wanauwezo wa kusoma masomo ya sayansi na kufanya vizuri isipokuwa changamoto kubwa inayowakabili ni ukosefu wa maabara na vitabu.

Wanafunzi hao wameishukuru kampuni ya simu ya airtel na kusema kwamba hivi sasa watasoma kwa bidii masomo hayo ya sayansi kwani kukosekana kwa vitabu hivyo kulikuwa kunachangia kutofanya vizuri katika masomo hayo.

"Tumekua tunapata shida sana kujifunza masomo ya sayansi kwani hapa shuleni kwetu hakuna hata maktaba wala maabara kwa ajili ya masomo hayo," alisema Rehema Issa.
"Vitabu hivi vitatuwezesha kufaulu masomo yetu ya sayansi japo bado tunakabiwa na tatizo na maabara aliongeza Blandina Charles mwanafunzi wa kidato cha tatu shuleni hapo.
Meneja masoko wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kanda ya kusini na mkoa wa morogoro Aminata Keita, amesema msaada huo ni mchango wa airtel katika elimu hapa nchini.

Keita amesema zoezi hilo la kutoa vitabu vya masomo ya sayansi linaendelea katika shule 35 za sekondari hapa nchini ili kuwawezesha wanafunzi kufanya vizuri katika masomo ya sayansi.
"Kwetu sisi Airtel hii ni fahari kubwa kushirikiana na shule hii katika kukuza ufaulu hasa kupitia vitabu hivi vya kiada ambavyo ni vya masomo ya sayansi" alisisitiza Keita.
"Mpaka sasa tumezifikia shule nyingi sana na Ilulu secondary imepata fursa ya kupata msaa huu, nawasihi mvitumie vitabu hivi kwa manufaa yenu na wenzenu watakaosoma hapa," alimalizia Aminata

Utaratibu wa kusaidia elimu kupitia mpango wa shule yetu ulio chini ya kampuni ya simu za mkononi ya airtel unachangia ukuaji wa sekta ya elimu kupitia vitabu vya masomo ya sayansi.

TAARIFA NA PICHA - DKT. SENGONDO MVUNGI APELEKWA AFRIKA KUSINI KWA MATIBABU ZAIDI LEO - ALHAMISI NOVEMBA 7 2013


 Mke wa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dkt. Sengondo Mvungi, …(kulia) pamoja na marafiki wakiomba dua leo (Alhamisi, Novemba 7, 2013) katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere dakika chache kabla na Dkt. Mvungi hajasafishwa kwenda Afrika Kusini kwa matibabu zaidi. Kushoto ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Bw. James Mbatia. Dkt. Mvungi alivamiwa na kujeruhiwa na watu nyumbani kwake Kibamba jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia Jumapili, Novemba 3, 2013.
Dkt. Mugisha Clement Mazoko wa Kitengo cha Mifupa Muhimbili (MOI) (kushoto), Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Assaa Rashid (mwenye tai) na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Bw. James Mbatia (wa pili kulia) pamoja na ndugu na jamaa wa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dkt. Sengondo Mvungi wakiangalia wakati Mjumbe huyo akipandishwa ndani ya ndege kusafirishwa kwenda Afrika Kusini kwa matibabu zaidi. Dkt. Mvungi alivamiwa na kujeruhiwa na watu nyumbani kwake Kibamba jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia Jumapili, Novemba 3, 2013.
Tume ya Mabadiliko ya Katiba inapenda kuwafahamisha wananchi kuwa Mjumbe wake Dkt. Sengondo Mvungi aliyekuwa akipata matibabu katika Kitengo cha Mifupa Muhimbili (MOI) amesafirishwa leo (Alhamisi, Novemba 7, 2013) saa 5:45 asubuhi kwenda nchini Afrika Kusini kwa uchunguzi na matibabu zaidi.
Akiwa nchini Afrika Kusini, Dkt. Mvungi atapata matibabu katika Hospital ya Milpark iliyopo jijini Johannesburg.

Wednesday, 6 November 2013

UNIC NA YUNA WATEMBELEA SHULE ZA MSINGI, SEKONDARI NA VYUO MBALIMBALI JIJINI ARUSHA



IMG_2521
Wajumbe wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na wawakilishi wa Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA/UNCTN) wakiwa kwenye mazungumzo ya awali na Mkuu wa Shule ya Arusha (Madam Kitigwa) baada ya kuwasili katika shule hiyo kwa lengo la kukutana na Kilabu cha Umoja wa Mataifa shuleni hapo na kuzungumza na Wanafunzi kuhusiana na agenda mbalimbali za Umoja huo. Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa kikishirikiana na Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa (YUNA) wapo katika ziara ya kuzitembelea shule zenye na zisizo na Vilabu vya Umoja huo kwa lengo la kufikisha habari na kazi za Umoja wa Mataifa.
IMG_2563
Afisa Habari wa Kituo cha Umoja Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama akizungumza na wanafunzi-wananchama wa klabu ya Umoja wa Mataifa katika Shule ya Msingi Arusha Medium ambapo amewasisitiza juu ya umuhimu wa kuzifahamu agenda mbalimbali za Umoja Mataifa na nafasi yao katika kuleta maendeleo chanya kwa jamii.
IMG_2602
Mwenyekiti Taifa wa Vilabu vya Umoja wa Mataifa Tanzania Bara na Visiwani (UNCTN) Bw. Rahim Rajab Nasser akizungumza na vijana wa shule ya msingi Arusha Medium juu ya umuhimu wa vilabu hivyo na umuhimu wa ushiriki wao kuanzia shule za msingi mpaka Sekondari na Vyuoni.
IMG_2629
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Bi. Usia Nkhoma Ledama (katikati) akisisitiza jambo kwa vijana wa shule ya msingi Arusha Medium. Kulia ni Mkutubi wa Maktaba ya kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Harriet Macha na kushoto Mwenyekiti Taifa wa Vilabu vya Umoja wa Mataifa Tanzania Bara na Visiwani (UNCTN) Bw. Rahim Rajab Nasser.
IMG_2650
Kobe mwenye umri sawa na shule ya Msingi Arusha Medium iliyojengwa mwaka 1930 akiwa hai mpaka na kuwa kivutio kwa wageni mbalimbali wanaofika shuleni hapo ikiwemo Wajumbe wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na wawakilishi wa Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA/UNCTN).
IMG_2754
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Bi. Usia Nkhoma Ledama akizungumza na Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Arusha kuhusiana na umuhimu wa agenda za malengo ya Milenia (MDG's) yanayotarajia kufikia tamati 2015 ambapo wao kama vijana wameshauriwa kutilia mkazo utekelezaji wa malengo hayo ikiwemo Usawa wa kijinsia na fursa sawa kwa Wanawake, Upatikanaji wa Huduma bora za uzazi na kupambana na Ukimwi, Malaria na magonjwa mengine.
IMG_2748
Pichani juu na chini ni baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Arusha waliobahatika kushiriki mkutano huo ulioendeshwa na Wajumbe wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na wawakilishi wa Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA/UNCTN).
IMG_2782
IMG_2860
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Bi. Usia Nkhoma Ledama akisalimiana na Mkuu wa Shule ya USA Academy Bw. Elibariki Malisa mara baada ya kuwasili shuleni hapo. Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa kikishirikiana na Asasi ya Vijana ya Umoja wa Mataifa (YUNA) wapo katika ziara ya kuzitembelea shule zenye na zisizo na Vilabu vya Umoja huo kwa lengo la kufikisha habari na kazi za Umoja wa Mataifa.
IMG_2868
Wajumbe wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) na wawakilishi wa Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA/UNCTN) wakiwa na mwenyeji wa msafara wao MC Kalinga wa Arusha wakielekea kukutana na wanafunzi wa USA Academy.

MAMA ASHA BILAL MGENI RASMI USIKU WA KHANGA ZA KALE 2013


Asha Bilal 

ASIA IDAROUS katikati akielezea shindano hilo
MKE wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Aisha Bilal, anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye  onesho la Usiku wa Khanga za Kale 2013 ‘5th Extra Vaa Khanga Party’  ndani ya  Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Novemba 8.
 
Akizungunza jana, mwandaaji wa onyesho hilo, Asia Idarous, alisema usiku huo Mama Asha Bilal atakuwa mgeni rasmi sambamba na watu mbalimbali maalufu wa ndani na nje ya Tanzania ambo pia watashuhudia muziki wa bendi ya Mashauzi Classic na DJ  Mkongwe nchini DJ John Dilinga .
 
“Wadau wa mitindo watapata burudani na kufurahia mitindo ya khanga itakayoonyeshwa kwenye shoo hiyo, hii si ya kukosa kwa mwaka huu,” alisema Asia Idarous.
 
Alisema usiku huo vazi la khanga ndilo litakuwa maalumu kwa wadau watakaohudhuria  sambamba na kupinga matumizi ya dawa za kulevya.
 
Onyesho la Usiku wa Khanga za Kale 2013 ambalo mwaka huu limeandaliwa kwa ushirikiano wa Asia Idarous na Fabak Fashions, linatarajiwa kuwa na shangwe mbalimbali ikiwamo kushirikisha watu maarufu na nyota mbalimbali. Wakiwemo Shilole, Snura, Ben Kinyaiya, Kibonde na wengineo.
 
Kiingilio katika onyesho hilo ni sh 30,000 na viti maalumu itakuwa ni sh 50,000 ambako tiketi zimeanza kuuzwa Fabak Fashions Mikocheni na Gift Shop Serena Hotel.
 
Aidha, alisema kati ya pesa zitakazo patikana pia zitaenda kusaidia kituo maalum cha kupambana na waathirika wa dawa za kulevya.
 
 
Usiku wa Khanga za Kale umedhaminiwa na Redd’s, CXC, Clouds FM, Vayle Spring, Magic FM, Eye View, Amina Design, Kabile, Vijimambo blog,Voice of America, Origin Unite, Channel Ten, DTV, Times FM, Michuzi Media Group, Event Light na Miss Tanzania,New Africa tv.com na wengine wengi

Nani awajibike ujenzi ghorofa mbovu K’koo?


Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya Design Plus Architects, Mustafa Maulid akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam  kuhusu ukaguzi wa majengo 67 yaliyojengwa kinyume na utaratibu na chini ya kiwango eneo la Kariakoo. Kushoto ni Mhasibu wa Kampuni hiyo, Zaina Nassor.

Kariakoo ni eneo kubwa lenye msongamano mkubwa wa watu, kwani ndio kituo chenye mkusanyiko wa watu kutoka wilaya zote za Mkoa wa Dar es Salaam na sehemu nyingine, ikiwamo Zanzibar.


Jana tulichapisha habari ya kutia hofu na iliyoashiria kwamba upo uwezekano mkubwa wa wananchi wengi kupoteza maisha wakati wowote kutokana na Sekta ya Ujenzi kuendeshwa kiholela na bila usimamizi wa viwango. Kampuni ya Design Plus Archtects (DPA), ambayo ilipewa zabuni ya kufanya ukaguzi wa majengo katika Manispaa ya Ilala, jijini Dar es Salaam imegundua kuwa, kati ya majengo ya ghorofa 90 yaliyokaguliwa katika manispaa hiyo, 67 yamejengwa chini ya kiwango na kinyume na sheria.
Msemaji wa kampuni hiyo ya DPA, Mustafa Maulid aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi kwamba hali ni mbaya katika majengo waliyoyakagua, huku akisema majengo hayo yana nyufa nyingi na yanaweza kuporomoka wakati wowote. Uamuzi wa kuipa kampuni binafsi kazi ya kukagua majengo ulikuja baada ya jengo lenye orofa 16 katika manispaa hiyo kuanguka Machi 26, mwaka huu na kuua watu 36, mbali na majengo mengine yaliyoanguka na kusababisha maafa makubwa huko nyuma.
Tunasema hizi ni habari za kutia hofu kutokana na ukweli kwamba hali hiyo mbovu ya majengo siyo tatizo la Manispaa ya Ilala pekee, bali pia ndiyo hali ya majengo katika maeneo mengi ya miji yetu hivi sasa. Sekta ya Ujenzi katika nchi yetu katika miaka ya hivi karibuni inaweza kufananishwa na mtoto yatima aliyeachwa duniani pasipo usimamizi au matunzo stahiki ya kumfanya aishi maisha ya heshima na katika mazingira yasiyo ya udhalilishaji. Hofu pia inatokana na mamlaka zilizopewa dhima ya kusimamia Sekta ya Ujenzi kushindwa kufanya hivyo kutokana na kugubikwa na vitendo vya rushwa na ufisadi.
Kariakoo ni eneo kubwa lenye msongamano mkubwa wa watu, kwani ndio kituo chenye mkusanyiko wa watu kutoka wilaya zote za Mkoa wa Dar es Salaam na sehemu nyingine, ikiwamo Zanzibar. Tunaambiwa hata kama siyo mtaalamu wa ujenzi, ukipita Kariakoo utagundua kwamba majengo mengi ya ghorofa yamejengwa bila kuzingatia sheria za ujenzi.
Hali hiyo imethibitishwa pia na Kampuni ya DPA iliyofanya ukaguzi wa majengo katika Manispaa ya Ilala. Kampuni hiyo inasema imegundua watu wengi wanafanya ujenzi bila vibali, wanajenga bila kufuata michoro iliyoidhinishwa na Manispaa ya Ilala na watu wanahamia kwenye majengo ya ghorofa kabla ujenzi wake haujakamilika. DPA pia inasema majengo yanatofautiana na michoro iliyotoka kwa wataalamu husika. Kwa mfano, pamoja na majengo yote ya Kariakoo kutakiwa kuwa na maegesho ya magari, wajenzi wameweka fremu za maduka.
Bahati mbaya hata Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa hana jibu sahihi kuhusu nini kifanyike. Kwa kudhani kwamba vikao vya madiwani ndivyo vitakavyotoa jibu kuhusu tatizo hilo, Meya Silaa anaonyesha bayana kwamba hata yeye hajui ukubwa wa tatizo hilo. Pamoja na kwamba kisheria madiwani ndio wenye dhima ya kusimamia sera za ukuaji wa miji, matatizo yaliyobainishwa na DPA ni mazito mno kutatuliwa na madiwani hao.
Sisi tunadhani mamlaka ya kufanya uamuzi mgumu kuhusu ghorofa nyingi mbovu za Kariakoo na kwingineko ni Serikali Kuu, ambayo pamoja na mambo mengine inapaswa kuwawajibisha walioshindwa kuzuia ujenzi holela. Hapa tuna maana kwamba uamuzi huo ufanywe na Waziri Mkuu, Makamu wa Rais au Rais mwenyewe.

MARUKU VANILLA WAENDELEA NA ZOEZI LA KUGAWA MICHE YA VANILLA

https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/?ui=2&ik=383a4cad12&view=att&th=1422dbe88cbc2cce&attid=0.4&disp=inline&realattid=f_hnon33mr3&safe=1&zw&saduie=AG9B_P8iTi55sRzrwVGNWyZCFNxu&sadet=1383766002783&sads=fJrNyzs5P7GFtDnZp3nuzxippH0
Mkurugenzi akigawa miche ya vanilla kwa wakulima
https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/?ui=2&ik=383a4cad12&view=att&th=1422dbe88cbc2cce&attid=0.3&disp=inline&realattid=f_hnon33mc2&safe=1&zw&saduie=AG9B_P8iTi55sRzrwVGNWyZCFNxu&sadet=1383766048729&sads=xzgNwQxZMcXaIJxTX6lADKbsqMw
Mkulima akifurahia baada ya kupata miche ya vanilla
https://mail-attachment.googleusercontent.com/attachment/?ui=2&ik=383a4cad12&view=att&th=1422dbe88cbc2cce&attid=0.2&disp=inline&realattid=f_hnon33lm1&safe=1&zw&saduie=AG9B_P8iTi55sRzrwVGNWyZCFNxu&sadet=1383766128045&sads=vdKxZRTzrOtjWIRf9bxHLxHEerc
Baadhi ya wakulima wa vanilla wakiwa kwenye mkutano na uongozi wa maruku vanilla

JACK WOLPER AZISALITI FEDHA ZA DALASI,AAMUA KUOKOKA UPYA


 STAA anayefanya vyema katika tasnia ya filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper ameamua kurudi katika imani yake ya awali ya Kikristo ikiwa ni miezi michache tangu alipotangaza kubadili dini na kuwa Muislamu.
Novemba 3, mwaka huu (Jumapili iliyopita) paparazi wetu alimnasa Wolper katika Kanisa la KKKT lililopo Kijitonyama jijini Dar, akisali sambamba na waumini wa kanisa hilo.
Bila ya kificho, Wolper ambaye alipokuwa Muislamu alikuwa akitumia jina la Ilham alisimama na kujitambulisha kama muumini mpya wakati mchungaji wa kanisa hilo alipowataka waumini wapya kufanya hivyo.
Wakati ibada hiyo ikiendelea, Wolper alionekana kuimba pambio kwa hisia kali na ibada ilipoisha, alitoka kanisani huku mkononi mwake akiwa ameshika Biblia.
 Paparazi wetu alimfuata Wolper na kumuuliza kilichomfanya arudi kwenye dini yake ya awali, naye alisema kwamba amefanya hivyo kutokana na msukumo wa wazazi wake ambao kwa muda mrefu walikuwa wakipinga kitendo chake cha kuwa Muislamu. 
“Nimeamua kuurudia Ukristo kwa kuwa wazazi wangu kwa muda mrefu walikataa mimi kuwa Muislamu, kwa hiyo kuanzia sasa siyo Ilham tena, niite Jacqueline kama zamani,” alisema Wolper.
Mwaka jana, Wolper alibadili dini na kuwa Muislamu kutokana na kuwa na uhusiano na Abdallah Mtoro ‘Dallas’. Dallas akiwa nje ya nchi akamtaka Wolper kubadili dini ili akirudi wafunge ndoa ya Kiislamu, Wolper alikubali na
Jacqueline Wolper (kulia), akiingia kanisani na rafiki yake kipenzi
kufanya hivyo katika Msikiti wa Kichangani uliopo Magomeni jijini Dar na kuchagua jina la Ilham. Dallas alirudi nchini lakini wawili hao hawakufunga ndoa bali penzi lao likaingia doa na kumwagana, Wolper akaendelea na msimamo wa imani yake hiyo mpya na mara kwa mara alikuwa akidai kwamba hataiacha dini hiyo pamoja na kumwagana na Dallas
Jack wlper katika akiwa akisali na waumini wenzake wa kanisa la K KKT jumapili iliyopita.