Waziri wa Tamisem Suleiman Jaffo amewataka watendaji mbalimbali katika wizara yake kuacha tabia ya kunyanyasa wananchi na kujiona miungu Watu , pale wananchi wanapokwenda katika ofisi zao kwa ajili ya kuhitaji huduma mbalimbali kwa ajili ya kuendeleza maisha yao,Waziri Jaffo aliyasema hayo katika Kongamano la Azimio la Kagera lililoandaliwa na kituo cha tv cha Clouds Tv, wakiwa wanatekeleza agizo la rais Dkt John Magufuli wakati wa ziara yake Mkoani Kagera alimtaka Mkurugenzi wa vipindi Clouds Tv Bw Ruge Mutahaba kuandaa kongamona kwa ajili ya kuibua na kujadili Fursa mbalimbali katika nyanja za kibiashara , kilimo, ujasilimari na mambo mengine kwa ajili ya maendeleo ya wananchi, kongamano hili lilifanyika Bukoba katika ukumbi wa Bukoba hotel na washiriki kutoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania walishiriki.(katika picha kulia ni Waziri wa biashara, viwanda na uwekezaji Charles Mwijage, Bw Ruge Muta
haba, Waziri wa Tamisem Suleiman Jaffo na mkuu wa Mkoa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu.)
No comments:
Post a Comment