Sunday 17 December 2017

WAHITIMU TIA WAMEASWA KUTOJIHUSISHA NA UBADHIRIFU WA MALI ZA UMMA NA RUSHWA


Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Wakili Said Chiguma akielezea weledi wa wahitimu wa Chuo hicho unaosababisha wengi kupata taaluma ya juu ya Uhasibu- CPA wakati wa Mahafali ya 15 ya Chuo hicho kwa Kampasi ya Mtwara na Dar es Salaam, yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akizungumza na wahitimu wa Kozi mbalimbali katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania – TIA kuhusu kujiepusha na masuala ya Rushwa wawapo kazini wakati wa Mahafali ya 15 ya Chuo hicho kwa Kampasi ya Mtwara na Dar es Salaam, Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Wahitimu wa Kozi mbalimbali wa katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania-TIA Kampasi ya Dar es Salaam na Mtwara, wakisubiri kwa hamu kutunukiwa shahada zao katika Mahafali ya 15 ya Chuo hicho kwa Kampasi ya Mtwara na Dar es Salaam, Jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) ( kushoto) akimpa zawadi Bw. Fransis Levis Mwanafunzi aliyefanya vizuri katika masomo yake katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Jijini Dar es Salaam.
Wahitimu wa Shahada ya Kwanza katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania – TIA wakiwa na furaha baada ya kutunukiwa vyeti vya Kozi mbalimbali na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (hayupo pichani) Jijini Dar es Salaam.

Na. Benny Mwaipaja
NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango Mhe Dkt. Ashatu Kijaji, amewataka wahitimu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kujiepusha na vitendo vya rushwa na ubadhilrifu wawapo kazini na badala yake wafanye kazi kwa bidii, uadilifu, umakini kwa kuzingatia Sera, sheria, kanuni na taratibu za kitaaluma zilizowekwa.
Dkt. Kijaji aliyasema hayo wakati akiwatunuku vyeti vya kozi mbalimbali wahitimu 3,538 wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania- TIA, wakati wa mahafali ya 15 ya Chuo hicho kwa Kampasi ya Dar es Salaam na Mtwara, Jijini Dar es Salaam.

‘Vitendo vya rushwa na ubadhirifu vina madhara makubwa kwa maisha ya mtu mmoja mmoja na uchumi wa Taifa letu kwa ujumla, ni vyema kila wakati mkumbuke kuwa rushwa ni adui wa haki na maendeleo ya Taifa.’ Alieleza Dkt. Kijaji.

No comments:

Post a Comment