Friday 27 January 2017

RAIS DK. MAGUFULI KUWA MGENI RASMI MAADHIMISHO YA SIKU YA SHERIA NCHINI




Rais John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Sheria nchini zitakazofanyika mwanzoni mwa mwezi ujao katika viwanja vya Mahakama jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Kaimu Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Hamis Juma amesema mahakama itawaelimisha wananchi jitihada mbalimbali ilizochukua zenye lengo la kuboresha huduma zake kupitia mpango mkakati wa miaka mitano inaoutekeleza katika kutoa haki kwa wakati na kuwezesha ukuaji wa uchumi.

Amesema kabla ya kilele cha maadhimisho hayo, mahakama itafanya matembezi maalum yatakayoongozwa na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi  na yataanzia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kuishia katika viwanja vya Mnazi mmoja.

Katika matembezi hayo Rais Mstaafu Mwinyi atazindua rasmi maadhimisho ya wiki ya elimu ya sheria ikiwa ni sehemu ya sherehe za kuelekea maadhimisho ya kilele cha siku ya sheria nchini.

Aidha ametoa rai kwa wananchi kutembelea sehemu zote zilizoandaliwa kwa ajili ya utoaji elimu ya sheria nchini kwa ajili ya kujifunza na kupata huduma mbalimbali za Kisheria.

Alizitaja huduma hizo ni pamoja na taratibu za ufunguaji mashauri katika ngazi mbalimbali za mahakama, taratibu za kesi za mirathi, taratibu za kesi za dhamana, taratibu za rufaa, ndoa na talaka, taratibu za kupokea na kushughulikia malalamiko na Msaada wa Kisheria.

Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini hufanyika kila mwaka mwanzoni mwa mwezi wa pili na mwaka huu yamebeba ujumbe wa Umuhimu wa Utoaji Haki kwa Wakati Kuwezesha Ukuaji wa Uchumi.

MWENYEKITI MSTAAFU WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI JAJI DAMIAN LUBUVA AKABIDHI TAARIFA YA UTENDAJI WAKE WA KAZI WA MIAKA 5 KWA MWENYEKITI WA SASA WA NEC JAJI WA RUFAA SEMISTOCLES KAIJAGE


 MAKABIDHIANO: Mwenyekiti Mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Damian Lubuva (kulia) akimkabidhi  Mwenyekiti wa sasa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage (kushoto) taarifa ya utendaji Kazi wake kwa kipindi miaka 5 alichokuwa madarakani.

 Mwenyekiti Mstaafu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Damian Lubuva akizungumza na Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Sekretarieti ya Tume hiyo mara baada ya kukabidhi taarifa ya utendaji Kazi wake kwa kipindi miaka 5 alichokuwa madarakani

 Mwenyekiti wa sasa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage akizungumza na Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Sekretarieti ya Tume hiyo mara kupokea taarifa ya utendaji Kazi wa Mwenyekiti Mstaafu wa Tume hiyo Jaji Damiani Lubuva jijini Dar es salaam.

 Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Bw. Ramadhan Kailima akizungumza jambo wakati wa makabidhiano hayo jijini Dar es salaam.Katikati ni Mwenyekiti Mstaafu wa Tume Jaji Mstaafu Damian Lubuva na Kulia ni  Mwenyekiti wa Sasa wa NEC, Jaji wa Rufaa, Semistocles Kaijage.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Rufaa Mhe. Semistocles Kaijage akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti Mstaafu wa Tume Jaji Damiani Lubuva , Wajumbe wa Tume na Secretarieti ya Tume hiyo.