Saturday 23 November 2013

BALOZI KAGASHEKI MGENI RASMI MAHAFARI YA KWANZA DARASA LA SABA QUDUS ISLAMIC PRE & PRIMARY SCHOOL, ACHANGIA MILIONI KUMI KUKAMILISHA UJENZI WA CHUMBA CHA KIDATO CHA KWANZA

 Balozi khamis kagasheki akiongea na wazazi na wanafunzi katika mahafali ya kwanza darasa la saba,shule ya Qudus Islamic imekuwa ya tatu kiwilaya katika mtihani wa darasa la saba 2013,ya nane kimkoa na ya 15 kitaifa kati ya shule 915 za msingi Tanzania,Balozi kagasheki  amewachangia milioni 10 kukamilisha ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa ili mwakani wanafunzi waweze kujiunga na kidato cha kwanza
                                      Akina mama walio katika kamati ya ujenzi ya shule
 Balozi kagasheki akipelekwa kuona ujenzi wa bweni la kulala wanafunzi aliloweka jiwe la msingi na kulichangia milioni ishirini na tano ili wakamilishe ujenzi
Hili ndio bweni ambalo siku chache  za nyuma Balozi kagasheki alilichangia milioni 25 ,linaendelea vizuri

 Na hivi ni vyumba vya madarasa kwa ajili ya kidato cha kwanza mwakani ambavyo  Balozi amechangia milioni  10 vikamiliki
                                       Balozi kagasheki akiwa na uongozi wa shule
                                                                             wanafunzi
                                                                    wanafunzi
                                                       wahitimu darasa la saba wakike
                                                       wahitimu darasa la saba wakiume
                                            Wazazi wakimsikiliza mgeni rasmi
 Balozi kagasheki amewataka wazazi kuwapa watoto elimu kwa msingi mzuri wa maisha yao hapo badae
                                                     Wazazi wakimsililiza mgeni rasmi

SENENE BUKOBA NI SUNAMI LEO 23- 11-2013

 Leo katika maeneo mengi na hasa sehemu za biashara  wamekutwa wamama na vijana wakimenya senene kwa kulipwa.
                                                             Senene fresh wanaruka
                                                        Ilikuwa ni umati mkubwa soko kuu leo
                                                             karibu afande
                                                            wengine wanaletwa sokoni
          Mr ruge masabala na bw jamco wakishuhudia watu wanavyonunua senene
                                            Pick up inaleta mzigo sokoni ni senene hao
Haya ni mavero ya senene ambayo hutumika kubebea kahawa na ni mali ya chama kikuu cha ushirika kagera (kcu)swali wanapata wapi haya mavero ya kahawa

Friday 22 November 2013

BALOZI KAGASHEKI ACHANGIA ZAIDI YA MILIONI NANE MRADI WA MAJI MTAA WA RWOME KATA YA KAHORORO LEO 22-11-2013

 Mbunge wa jimbo la bukoba mjini na waziri wa maliasili na utalii balozi Khamis Sued Kagasheki akiongea na wakazi wa mtaa wa rwome kata kahororo ambao wamekuwa na tatizo la maji kwa muda mrefu. Baada ya mradi kuibuliwa na wanamtaa wa rwome  wenye thamani ya milioni 326 unaofadhiliwa na benki ya dunia,wananchi walitakiwa kuchangia asilimia 2.2 kiasi cha shilingi milioni tisa ili uweze kuanza,kitu ambacho kilishindwa kutekelezwa kutokana na hali ya ukata inayowakabili wananchi na kupelekea kupeleka ombi kwa mbunge wao ili aweze kuwasaidia.
 Mh mbunge  Kagasheki akiwasili kwenye viwanja vya zahanati kahororo akisalimiana na diwani wa kata hiyo Chief kalumuna
                                                                      Wanakahororo
                         Kulia wa kwanza Mwenyekiti wa ccm bukoba mjini Yusuf Ngaiza
                         Katibu wa chama bukoba mjini Bi Janat Musa akisalimia wanakahororo
                                                                wananchi wakifurahia
                               Diwani wa kahororo akiwa na mwenyekiti wa mtaa
           Wa pili kulia mzee muyoza aliewahi kuwa diwani wa kata ya kahororo kwa muda mrefu
 Bw bwemero akieleza mradi wa pikipiki unaodhaminiwa na Balozi kagasheki,amewataka vijana kufika ofisini kwao uswahilini mayunga ili waweze kupewa utaratibu wa kukopeshwa pikipiki
                                                           Watangazaji wa kasibante redio
                                                     Wanakahororo wakimsikiliza mbunge wao
 Balozi kagasheki pamoja na kuchangia mradi wa maji kwa wakazi wa rwome, pia amehaidi ndani ya wiki moja kuwanunulia tank kubwa la maji kwa ajili ya zahanati ya kahororo ,baada ya tank la zamani lililojengwa kuharibika,lakini pia kuna tatizo la ngedere wanaosumbua na kuharibu mazao ya wakazi wa kahororo na majirani, amehaidi kulipia gharama za milioni moja kuleta wataalamu waweze kukabiliana na tatizo hilo.
Mkuruganzi wa kiroyera Tours mama Mary Kalikawe nae alihaidi kuchangia dora 500 za kimarekani kuunga jitihada za balozi kagasheki kusaidia wananchi wa jimbo lake katika maendeleo