Tuesday 6 January 2015

OMULANGIRA JUSTUCE RUGAIBULA ATOA SHUKRANI.

 Kulia katika picha ni Omulangira Justuce Rugaibula ,anapenda kutoa shukrani zake za dhati kwa ndugu, jamaa na marafiki wote waliofika  katika hafla ya Kutabaruki na kumkabidhi nyumba ya kuishi mama yake mzazi Ma Grace Alexander,iliyofanyika Kashenye Kanyigo siku ya mwaka mpya,Omulangira Justuce Rugaibula akiongea kwa njia ya simu na mmiliki wa mtandoa wa Jamcobukoba.blogspot.com akiwa Jijini Dar es salaam amesema alitamani sana amfikie kila mmoja na kuonana nae ana kwa ana lakini ni vigumu kutokana na wingi wa watu waliojitokeza, lakini pia ufinyo wa muda kutokana na majukumu kuwa mengi, hivyo anaamini kupitia vyombo vya habari kama Tv,Redio, Tv cable,simu na mitandao ya kijamii  shukrani zake zitafika kwa kila mmoja alieshiriki hafla hiyo. Amesema umati mkubwa ulijitokeza umemfanya kuwa na deni kubwa kuhakikisha anadumisha na kuendeleza mapenzi makubwa mliyomuonyesha, anaomba kila mmoja kwa  nafasi yake atambue kuwa anamdhamini kwa kutenga muda wake na hasa ukizingatia ilikuwa ni siku ya kuanza mwaka 2015  lakini waliacha majukumu mengine na kushiriki nae anasema asante sana mungu awabariki sana.
 Baadhi ya maeneo ya nyumba ya Ma Graice.

 Padre akitabaruki nyumba.
 Wageni waliofika kwenye hafla.
 Bw Al amin Abdul akimpongeza Bw Justuce kwa tendo zuri alilomfanyia mama yake.
 Marafiki mbalimbali wakifurahia.
 Bw Yakubu Kabaka akimpongeza Bw Justuce.
 Mwenye suti nyeupe ni Bw Hafidh Karugira akionyesha furaha yake kwa tukio lililofanyika.
 Kushoto ni Ma Graice, mama mzazi wa Justuce.
 Omulangira Justuce akiwa na mkewe Kisha, au mama Jojo.

 ILIKUWA NI FURAHA SIKU HIYO.
 Mbali nas kukabidhiwa nyumba,pia mama mzazi wa Justuce alikabidhiwa gari na wajukuu kwa ajiri ya kumsaidia hapo nyumbani.
 Mjuni Kataraiya akipata kitu kikali.
Hakika ilikuwa ni shughuli pevu.Wote mliofika Omulangira Justuce Rugaibura anawashukuru sana,Mutalihwao.Nabagonza muno(Anawapenda sana.)

HONGERA DANIEL NDYEKOBORA NA DIANA SIMA RUGUMILA KWA KUFUNGA NDOA.

 Ni Mr & Mrs  Daniel Ndyekobora wanaonekana na nyuso za furaha,muda mfupi baada ya kufunga ndoa katika kanisa la kilutheri usharika wa Ibura Bukoba Mjini na badae sherehe ya kuwapongeza ilifanyika Kanyigo Bukoba.
 Wakiingia kanisani kula kiapo.
 Mchungaji akiendelea na Ibada.
 Mme wangu nahaidi mbele ya umma huu uliombele yetu na kila kona ya mahala hapa patakatifu kukupenda, kukuheshimu, kukulinda katika raha na gharika la aina yoyote kwa kipindi chote tutakachoishi hapa duniani.
 Mkataba tayari.
 Siku hizi mapaparazi kibao.
 Kushoto mdau mkubwa wa jamcoblog Bi Erica katika picha ya pamoja na  maharusi.
 Patron na Matron wakakumbushana enzi hizooooo.
 Full shangwe.
 Wakiingia ukumbini kijijini Kanyigo.
 Mchungaji akafungua sherehe kwa sala.
 Wapambe pendeza sana.
 Ikakatwa keki.
 Stail ya kurishana,ni shidaaaa.
Hongera maharusi.
Mungu awabariki katika maisha ya ndoa.