Saturday 5 April 2014

KAGERA SUGAR 1 v SIMBA 1, MTANANGE WAMALIZIKA KWA SARE! HAKUNA MBABE!


Timu zikiingia uwanjani.

Wachezaji wakisalimiana
Karibu sana Bukoba, Salaam sana...Wachezaji wakisalimiana..

Kikosi cha Kagera kilichoanzaKikosi cha Simba kilichoanza

Waamuzi wa Mtanange huu kati ya Kagera Sugar na Simba
Kikosi cha Kagera Wakiomba muda mchache kabla ya kuanza mtanange
Ivo Mapunda Kipa wa Simba na Timu Kapteini akisalimiana na waamuzi wa mtanange huu wa leo

Mtaanzia  upande huu...
Viongozi wa Kagera Sugar
Benchi la Kagera Sugar
Benchi la Simba

Mchezo umemalizika Kaitaba ambapo wenyeji wa uwanja huo wamewakaribisha wekundu wa Msimbazi Simba sc.
Mtanange umemalizika kwa sare ya bao 1-1.
Simba walikuwa wa kwanza kuandika bao la kuongoza katika dakika ya 45 kipindi cha kwanza kupitia kwa Zahor Idd Pazzi akipokea krosi kutoka kwa nahodha wao, Nassor Masoud Cholo.
Kagera walisawazisha bao hilo dakika ya 51 kipindi cha pili kupitia kwa mshambuliaji wao hatari, Them Felix `Mnyama`.
Kwa matokeo hayo, Simba sc wamefikisha pointi 37 katika nafasi ya 4 baada ya kushuka dimbani mara 24.
Kagera Sugar wamefikisha pointi 34 katika nafasi ya 5 baada ya kushuka dimbani mara 23.
Mechi ya Kaitaba haikuwa na ushindani mkubwa kwani timu zote hazikuwa na cha kupoteza, kwa maana ya kutotafuta ubingwa wala nafasi ya pili.
Timu zote zilikuwa zinashambuliana kwa zamu, lakini Kagera Sugar walipata nafasi nyingi zaidi ya Simba.
Hata hivyo ubutu wa safu za ushambuliaji kwa timu zote, kumeamuru matokeo yawe 1-1 mpaka dakika 90 zinamalizika.
Dakika ya 51 Kagera wanasawazisha kupitia kwa Temi Felix ..1-1. Kipindi cha pili kimekuwa kigumu pande zote mbili kila timu ikimnyemelea mwenzake na dakika lala salama Simba walipata nafasi ya bao lakini mwamuzi wa pembeni alinyoonya kibendera kuashilia siyo bao na Kufanya mtanange kumalizika kwa kugawana pointi ya bao 1-1.

Mashabiki wa Timu ya Simba SC Kaitaba wakiipa nguvu timu yao kwa kushangilia..

Mashabiki wa Simba
Mashabiki wa Simba wakishangilia...

Azam Tv, Picha zikichuliwa live juu ya paa za jukwaa kuu kwenye Uwanja wa Kaitaba leo hii wakati wa kipute kilichomalizika kwa bao 1-1

Wadau..

Hapa hukatizi..
Wachezaji wa Simba wakipongezana baada ya kupata bao la kwanza katika dakika za mwishoni mwa kipindi cha kwanza


Wachezaji wa Kagera Sugar wakipongezana baada ya kusawazisha bao na kufanya 1-1 dakika ya 48
hapa hakuna kulala!

Mashabiki wa Timu ya Kagera Sugar wakishangilia...

Furaha za hapa na pale za mashabiki wa Kagera baada ya timu yao kusawazisha bao

Mashabiki wa Kagera Sugar

Kipute kikiendelea

Mchezaji wa Kagera aliumia hapa na anakimbiliwa na docta wa timu kupewa huduma ya haraka

kazi kwako!!! ni mimi na wewe!!

Kimbiza kimbiza katikati ya uwanja, Simba wakiendesha mashambulizi
Mchezaji wa Kagera Sugar Chini..
Kocha wa Simba Zdravko Logarusic akiwa kwenye mwonekano tofauti sana huku akilaumu waamuzi kwa kile lichotokea...

Visingizio baada ya mtanange kumalizika!!!
Kocha wa Simba Zdravko Logarusic akiwapa maneno waamuzi

Kocha Loga..na mbwembwe mbele ya mwamuzi
KOCHA wa Simba Zdravko Logarusic akiwateja jambo kwa Vitedo baada ya mtanange kumalizika
Kocha wa Simba Zdravko Logarusic akiteta tena na waamuzi wote watatu wa mtanange huu wa leo ambapo Timu zote zimetoshana nguvu kwa bao 1-1

Kocha wa Kagera akiteta jambo na mchambuzi wa Soka Kaijage katika uwanja wa Kaitaba leo hii

Friday 4 April 2014

AJALI YA GARI LATUMBUKIA DARAJA LA MTO KANONI BARABARA IENDAYO KASTAMU BANDARINI ,USIKU WA MANANE KUAMKIA 5-4-2014,YASEMEKANA DEREVA ALIKUWA KALEWA

 Ni ajali mbaya iliyotokea usiku wa manane kuamkia 5-4-2014  katika daraja la mto Kanoni barabara iendayo Bandari ya Bukoba, Gari ndogo Toyota yenye namba za usajili T 910 CTC, ambalo mmiliki wake hajajulikana,japo katika eneo la tukio mwananchi mmoja alisikika akisema ni mal;i ya Askari Polisi ambae hakutaja jina, Mwananchi huyo alieeleza kuwa yeye anahishi maeneo ya ajali ilipotokea alisema Dereva wa gari hili alikuwa mwendo kasi usiku wa manane na alikuwa amelewa na kutumbukia kwenye daraja na badae waliokolewa. Jamcobukoba.blogspot tulifika Polisi kujilidhisha na nilikutana na Bw Magayane ambae ni msaidizi katika kitengo cha Uaslama Barabarani alikiri kuwa na Tarifa za ajali hiyo na kusibitisha kuwa hakuna alieumia, na nilipotaka kujua mmiliki wa Gari hili alisema hawamjui wapo katika jitihada za kumtambua.
 Wananchi wakiangalia ajali ya gari  Daraja la mto Kanoni barabara iendayo Kastam bandarini
 Hali kama unavyoona
 Kama kweli ni ulevi ni nomaaaa
 Jamani umakini Barabarani ni muhimu
Mwendo kasi, ulevi, kuongea na simu ni hatari unapoendesha gari kuwa makini.