Friday 4 April 2014

AJALI YA GARI LATUMBUKIA DARAJA LA MTO KANONI BARABARA IENDAYO KASTAMU BANDARINI ,USIKU WA MANANE KUAMKIA 5-4-2014,YASEMEKANA DEREVA ALIKUWA KALEWA

 Ni ajali mbaya iliyotokea usiku wa manane kuamkia 5-4-2014  katika daraja la mto Kanoni barabara iendayo Bandari ya Bukoba, Gari ndogo Toyota yenye namba za usajili T 910 CTC, ambalo mmiliki wake hajajulikana,japo katika eneo la tukio mwananchi mmoja alisikika akisema ni mal;i ya Askari Polisi ambae hakutaja jina, Mwananchi huyo alieeleza kuwa yeye anahishi maeneo ya ajali ilipotokea alisema Dereva wa gari hili alikuwa mwendo kasi usiku wa manane na alikuwa amelewa na kutumbukia kwenye daraja na badae waliokolewa. Jamcobukoba.blogspot tulifika Polisi kujilidhisha na nilikutana na Bw Magayane ambae ni msaidizi katika kitengo cha Uaslama Barabarani alikiri kuwa na Tarifa za ajali hiyo na kusibitisha kuwa hakuna alieumia, na nilipotaka kujua mmiliki wa Gari hili alisema hawamjui wapo katika jitihada za kumtambua.
 Wananchi wakiangalia ajali ya gari  Daraja la mto Kanoni barabara iendayo Kastam bandarini
 Hali kama unavyoona
 Kama kweli ni ulevi ni nomaaaa
 Jamani umakini Barabarani ni muhimu
Mwendo kasi, ulevi, kuongea na simu ni hatari unapoendesha gari kuwa makini.

No comments:

Post a Comment