Wednesday 11 November 2015

NEW COFFEE TREE HOTEL YAFUNGWA KUTOA HUDUMA,BUKOBA.

 Tukiwa mtaani na camera yetu ghafla maeneo ya New Coffee Tree tumekuta magari ya kipakia vifaa mbalimbali Tv, vyombo, mashuka, Taulo ,Friji za vyumbani na vifaa vingine vilivyokuwa vikitumika hotelini, Hali hiyo ilibidi kufika na kutaka kujua kwa undani kulikoni kilichotokea,Mpiga picha hizi  alipata fursa ya kuongea na kijana mmoja aliekuwa msimamizi wa hotel hiyo ambae alikuwa mgumu kutaja jina lake alisema... Imebidi tufunge mizigo yetu baada ya Tajiri yetu kushindwa kuelewana na uongozi mpya wa chama cha ushirika wilaya ya Karagwe (KDCU) wamiliki wa hotel, ambao umechukua madaaraka hivi karibuni,ila inavyoelekea miongoni mwa wakurugenzi yupo mtu anapataka, Ila kazi wanayo maana vitu vyetu vyote tunavitoa vitajaa gari mbili zilizopo hapa... Mwisho wa kunukuu. New Coffee Tree ni moja ya hotel iliyokuwa ikitoa huduma ya malazi, chakula na vinywaji,pia huduma ya ukumbi kwa ajili ya maharusi na mikutano, Tupo kwenye jitihada za kumpata aliekuwa  amekodi hotel hii kibiashara Bw Mushema anaeishi jijini Mwanza kupata ukweli wa jambo hili.
 Eneo la jiko la nje kweupe.
 Friji zikiwa zimetolewa nje ya vyumba.

No comments:

Post a Comment