Thursday 16 March 2017

MAKAMU WA RAIS AMEWASILI MBABANE SWAZILAND










Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan  amewasili mjini Mbabane - Swaziland leo 16-Mar-2017 kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika(SADC).


Mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Kimataifa wa Mfalme Mswati III mjini Mbabane – Swaziland, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amepokelewa na Viongozi mbalimbali ambao wameongozwa na Waziri wa Utumishi wa Umma wa Serikali ya Swaziland Owen Nxumalo.



Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan baada ya kuwasili uwanjani hapo amekagua gwaride la heshima lililoandaliwa kwa ajili yake na kushuhudia vikundi mbalimbali vya burudani uwanjani hapo.



Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan atamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dakta JOHN POMBE MAGUFULI ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama inayojulikana kama SADC DOUBLE TROIKA kwenye mkutano huo.



Hapo kesho tarehe 17-Marchi-2017, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan atahudhuria mkutano wa Wakuu na Serikali wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama unaojulikana kama SADC Double Troika  ambao utajadili kwa kina hali ya ulinzi na usalama katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)na Falme ya Lesotho.



Mkutano huo wa SADC Double Troika utafanyika kwa kuzingatia mapendekezo ya mkutano wa Mawaziri wa Kamati Ndogo ya Siasa na Diplomasia uliofanyika Dar es Salaam tarehe 24 februari 2017 ambapo mawaziri hao walionyesha ipo haja ya kuitisha mkutano huo ili kujadili kwa kina hali ya ulinzi na usalama kwenye hizo.



Mkutano wa SADC Double Troika utahusisha nchi Sita wanachama wa asasi hiyo ambazo ni Tanzania,Swaziland, Afrika Kusini, Angola, Botswana na Msumbiji.



Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan katika msafara wake amefuatana na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kikanda na Kimataifa Dakta Augustine Mahiga, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Balozi Amina Salum Ali.


MARAIS WASTAAFU WAONGOZA KUAGA MWILI WA MAREHEMU SIR GEORGE KAHAMA


Thursday, March 16, 2017

 Mke wa Marehemu Sir Georeg Kahma, Janeth Kahama akiaga mwili wa Mumewe katika ukumbi Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam
 Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete akiaga Mwili wa Marehemu Sir George Kahama
 Rais Mstaafu wa awamu ya tatu , Benjamini Mkapa  akitoa pole kwa watoto wa Marehemu Sir George Kahama katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam
 Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi akiaga mwili wa Marehemu Sir George Kahama.
 Waziri wa Habari Sanaa  Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye akiaga Mwili wa Marehemu Sir George Kahama.
 Waziri mkuu Mstaafu, Salim Ahmed Salim akiaga mwili wa Marehemu Sir George Kahama katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam
 Spika Mstaafu wa Bunge , Anna Makinda akitoa pole kwa wanafamilia ya Marehemu Sir George Kahama.
 Kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni , Freeman Mbowe  akiaga mwili wa Marehemu Sir George Kahama katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam
Mtoto wa Marehemu Sir George Kahama  akiaga mwili wa babake
 Sehemu ya ndugu wa familia wakiaga mwili wa Marehemu Sir George Kahama
 Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowasa akitoa pole kwa watoto Marehemu Sir George Kahamakatika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam
 Mawaziri wakuu wa Staafu pamoja na wake zao wakiwa katika msiba huo kwa uhuzuni
 Marais Wastaafu na wake zao wakiwa wanatafakari  kabla ya kuaga mwili wa Marehemu Sir George Kahama.
Mawaziri wakuu wastaafu wakitafakari jambo kabla ya kuaga Mwili wa Marehemu Sir George Kahama  katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam