Saturday, 14 September 2013

KAGERA SUGAR NA AZAM NGOMA DROO 1-1 UWANJA WA KAITABA, BUKOBA

Waamuzi wa Mtanange huu.

Picha ya pamoja

Waamuzi na timu kapteni wakijuzana kuhusu uelekeo wa kila timu


Timu ya Kagera Sugar ndiyo iliyotangulia kupata bao kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, kupitia mchezaji Themi Felix Buhaja aliyefunga bao la kichwa baada ya kupigwa kona katika dakika ya 25 ya kipindi cha kwanza. Kipindi cha pili dakika ya 55 Khamis Mcha ‘Vialli’ aliisawazishia Azam FC bao na kufanya mpira kuisha kwa matokeo hayo hayo mpaka dakika 90 za mchezo.
Katika mechi nyingine Coastal Union ilitoka sare ya bila kufungana na Tanzania Prisons Uwanja wa Mkwakwani, Tanga wakati Ruvu Shooting iliifunga 1-0 Mgambo Shooting kwa bao pekee la Elias Maguri dakika ya 53 Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani
Oljoro JKT ilitoka sare ya 1-1 na Rhino Rangers Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha, wenyeji wakilazimika kusawazisha dakika ya 27 kupitia kwa Amiri Hamad baada ya Saad Kipanga kutangulia kuwafungia wageni dakika ya tano, wakati Ashanti United ililala 1-0 mbele ya JKT Ruvu,
Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam bao pekee la Amos Mgisa dakika ya 81. Matokeo hayo, yanamaanisha JKT Ruvu inaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi zake tisa baada ya kushinda mechi zote tatu, ikifuatiwa na Simba SC katika nafasi ya pili yenye pointi saba.
Timu nyingi zimefungana kwa pointi tano katika nafasi ya tatu, zikiwemo Yanga, Azam na Coastal Union.

Kikosi kilichoanza cha Kagera Sugar
Bechi la Kagera pamoja na Viongozi wake.

Viongozi wa Kagera Suga kulia ni kocha mkuu.

Benchi la Azam Fc

Kipute kianze!!

Timu zote mbili zilianza kwa kukamiana! huku Azam FC wakijaribu kuingia kwenye eneo la Kagera Sugar mara kwa maraMchezaji wa Azam Fc akiondosha mpira kwa kichwa kuelekea goli la Kagera

Makocha wote wawili Azam Na Kagera Sugar wakiwajibika uwanjani hii leo


Kila mchezaji akitaka amchomoke mwenzake hapa!!

Mchezaji matata wa Azam Fc Kipre Cheche akimchomoka mchezaji wa Kagera Sugarr hapa na kuanza mbio za kasi!

Wachezaji wa Kagera Sugar wakimpongeza Themi Felix baada ya kufunga bao dakika ya 25 baada ya kupigwa kona na yeye kumalizia kwa kichwa hadi nyavuni.

Wachezaji Kagera Sugar wakifurahia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam FC.

Patashika!

Mchezaji wa Kagera Sugar akiondosha mbele mpira

Kocha wa Azam FC kulia akiangalia mtanange kipindi cha kwanza kuwa mgumu kwake!!

Mashabiki

Wadau mbalimbali wakitazama mtanange

Ilikuwa patashika hapa kwenye kipindi cha pili Timu ya Azam Fc ilipania kurudisha bao haraka iwezekanavyo na hatimaye kulipata baada ya dakika tano kupita!!

Khamis Mcha Vialli akishangilia baada ya kusawazisha bao dakika ya 55 kipindi cha pili.

Wachezaji wa Azam FC wakishangilia na kumpongeza mchezaji wao Mcha baada ya kusawazisha bao hilo

Angalia Viongozi wa Timu wanavyokuwa hapa, mwanzoni kocha wa Azam alilamika na kipindi hiki baada ya Kagera Sugar akaanza kuleta za kuleta !!

Kocha wa Azam Fc

Mpira umekwisha!!
Timu zote mbili zikitoka nje na sare ya bao 1-1.

Thursday, 12 September 2013

CHUO CHA UALIMU-ERA KUANZA MAPEMA MWAKANI,NDOTO YA PASKAZIA BARONGO KUTIMIA

 Mkurugenzi wa kampuni ya passy community service Ltd Paskazia Barongo akiwakaribisha wadau wa elimu kutoka katika manispaa ya bukoba na maeneo mengine aliowakaribisha kuja kumpa mawazo,ushauri jinsi atakavyoanzisha chuo cha ualimu-ERA kinachotarajiwa kuanza mwakani mwezi wasaba katika manispaa  ya bukoba kata ya kitendaguro.Akiongea na wadau wa elimu bi paskazia barongo amesema anatarajia chuo wanachoanzisha kitakuwa cha mfano kwa kutoa elimu bora na kuigwa na vyuo vingine.
                                    baadhi ya wakuu wa shule za sekondari wakimsikiliza bi paskazia barongo
                                                               mdau amin akiwa na varelian
 mkurugenzi wa cosadakisikiliza kwa makini mipango ya uanzishwaji wa chuo cha ualimu mwakani
                          mzee kasimu,mmoja mwa wadau waliohudhulia mwaliko
 ni mchoro wa majengo ya chuo kitakavyokuwa kitakapokamilika,ila majengo yaliyopo wataanza nayo
                      bi paskazia barongo akiwatembeza wadau wa elimu kuangalia mazingira ya chuo
                 Bi paskazia barongo akieleza mikakati waliyonayo chuo kikianza mapema mwakani
                                                muonekano wa vyumba utakavyokua chuoni hapo
                                                              wadau ukiangalia maeneo ya chuo
                                                       majengo ya chuo ambayo yako tayari
                         chuo kitakuwa na eneo kubwa na mazingira ya kumuwezesha mwanachuo kusoma
                 picha ya pamoja ya wadau wa elimu walioudhuria mwaliko wa bi paskazia barongo
Ilikuwa ni ndoto ya muda mrefu ya bi paskazia barongo anaeishi sweden kufanya kitu cha maendeleo nyumbani,sasa ndoto yake inaelekea kutimia mwakani kuanzisha chuo cha elimu,na kikubwa amesema si biashara lengo kuwapa elimu bora wanafunzi na kuelimisha jamii kwa ujumla. bi passy jamcobukoba.blogspot.com inakutakia afya njema,nguvu ili uweze kutimiza ndoto yako .

MKURUGENZI MKUU WA KAMPUNI YA BIA SERENGETI BREWERIES TANZANIA BW STEPHEN GANNON ATEMBELEA WAKALA WA SERENGETI BREWERIES WA KAGERA NA GEITA, KAMPUNI YA ZACHWA INVESTMENT KUJIONEA UFANISI WA KAZI




                                 Mkurugenzi mkuu wa serengeti  breweries bw Stephen Gannon



mkurugenzi wa zachwa investment bw muganyizi wakala wa kagera na geita akiongea na mkurugenzi mkuu wa serengeti breweries bw stephen gannon nyumbani kwa bwana muganyizi



                                bw  muganyizi na mkewe,wakiwa na  bw stephen gannon

                                                             Ni katika hoteli ya victorius


mmoja wa wakurugenzi wa zachwa investment jane muganyizi akiongea na wageni waliokaribishwa chakula cha usiku  katika hotel ya victorius


mkurugenzi mkuu tanzania wa serengeti breweries akiongea na wateja na wadau mbalimbali wa serengeti





                                     naikubali kazi yenu........tutaendelea  kufanya kazi na nyie


        mkurugenzi wa zachwa investment bw muganyizi akielezea kinywaji kipya cha serengeti

si utani serengeti ni kiboko...

                                         wanasema waenga upele umepata mkunaji,




jamani sina mengi , kunywa bia za serengeti

                                                    chakula cha bukoba si mchezo.......



                                    wadau wa serengeti wakipata chakula victorius hotel bukoba



                                                                 enangaaaa...

                                                     mkurugenzi akanogewa .....

                                                            ukafika wakati wa muziki



                                                                        serengeti breweries si mchezo