Wednesday 26 October 2016

BENKI YA POSTA TANZANIA(TPB) NA SBFIC WATEMBELEA MASHULE KARAGWE NA KUTOA ZAWADI.

 Katika maadhimisho ya wiki ya kuweka akiba duniani,Benki ya Posta Tanzania(TPB) na SBFIC pamoja na  washirika wake wametembelea shule mbalimbali za msingi na sekondari kujionea namna wanafunzi walivyoweza kufundishwa namna ya kujiwekea akiba benki kwa ajira ya matumizi ya badae,mbali ya kujionea namna wanafunzi hao walivyofundishwa, pia  SBFIC walitoa zawadi ya kalamu na daftari kwa wanafunzi waliojifunza,Shirika la Karudeca  kupitia Benki ya posta Tanzania wamekuwa wakitoa mafunzo katika shule hizo kwa kufadhiliwa na SBFIC.Shule zilizonufaika na mafunzo hayo ni Kayanga shule ya msingi, Ihanda sule ya msingi, Ndama shule ya sekonda, Kayanga shule ya sekondari na shule zingine wilayani Karagwe, Kilele cha maadhimisho ya wiki ya kuweka akiba kitafanyika siku ya Jumamosi 28-10-2016 katika uwanja wa mpira wa Kayanga kuanzia saa nne asubuhi,mbali ya viongozi mbalimbali  watakuwepo pia wasanii maarufu Mpoke wa Ze COMED na Bk Sande.(katika picha ni mtendaji mkuu wa SBFIC makao makuu Dar-es-salaam Bw  Marco Projosky akiuliza maswali  wanafunzi.)
 Katika ofisi za Karudeca maandalizi ya kutembelea mashule yakifanyika.

 Vitabu vya mafunzo vilivyotolewa na  SBFIC.
 Bi Karunde akimpa zawadi  ya shilingi elfu kumi mwanafunzi alijibu swali vizuri kuhusiana na namna ya kuweka akiba,
 Bw Miki Meneja wa Benki ya Posta Karagwe akitoa somo kwa wanafunzi.
  Zawadi zikitolewa.


Monday 24 October 2016

HAPPY BIRTHDAY JUDY ZACHWA, USIKU WA WHITE & BLACK PARTY NDANI YA WALKGARD TRANSIT.

 Ilikuwa ni siku ya aina yake kwa Bi Judy Zachwa ,akiwa na wazazi , ndugu , jamaa na marafiki waliofika katika sherehe ya kumpongeza(siku ya kuzaliwa) katika ukumbi mzuri wa Walkgard Ttransit,Hakika  ni moja  ya sherehe kubwa na ya aina yake , wageni waalikwa walionekana  katika mavazi meupe na meusi na kusababisha manzari ya ukumbi  kupendeza, lakini pia utaratibu wa vyakula na vinywa uliowekwa ulikuwa ni wa kuifanya sherehe kuonekana na viwango fulani hivi..Wageni waalikwa hakika walipendeza.(katika picha kulia ni Bi Judy akirishwa keki na rafiki yake mpenzi Bi Beaty rweyendera.)Happy Birthday Judy.

 Ni bango kubwa ,unakutana nalo lango kuu.sehemu ya waalikwa kupigia picha.

 Mazingira ya Walkgard Transit.
 Kulia ni Mr Jamal Kalumuna(Mwenyekiti wa sherehe akiwa na Mr Bube).
 Waalikwa wakiingia ukumbini.
 Muonekano wa meza kila meza.
 Wakati ukiingia unapokelewa na kupata  Welcome drink -Cocktail ( Alcoholic-Sangria, Mock tail ( Non - Alcoholic- V irgin-Pinacolada.
Edgar akipata Welcome drink.
Mama Matungwa aliutendea ukumbi haki kwa mapambo,chakula vinywaji Walkgard Transit ilihusika.

Maua Daftari akiingia ukumbini.
Bw Ally akiingia ukumbini.
Bw Samora Lyakulwa akiingia ukumbini.
Mrs Deo Rugaibura.
Mc Jerry  nae akaja kama mgeni.
Mr  & Mrs Alex katika ubora wao.
Kila kitu kilikuwepo.
Watu walitokelezea hatariii.
Kushoto Bi  Judy Zachwa akiwa na Mama Matungwa.
Watatu kutoka kushoto ni meya wa Manispaa ya Bukoba Chief Kalumuna  akiwa na diwani A lmasoud Kalumuna wakiwasili ukumbini.
Mr Muganyizi (kushoto ) akiwa na Bw Samora.
Bi Judy Zachwa amitimiza miaka kadhaa, happy birthday.
Dj Anord Mushumbusi akiwa na Dj Sray wa kasibante redio.
Mwenyekiti wa sherehe Jamal Kalumuna akifungua sherehe rasmi.
Watu wakifurahi.

Ikakatwa keki.

Rahim Kabyemela akirishwa keki.
Judy akiwashukuru wadada waliompa ushirikiano mkubwa katika maandalizi.
Mr & Mrs Aderius katika ubora wao.
Vijimambo.
Mr Muganyizi akatoa neno  na zawadi kwa mwanae.
Beaty Nangai rafiki mpenzi wa Judy akatoa zawadi.
Dollar za kimarekani zikahusika