Saturday, 6 July 2013

MICHUANO YA KOMBE LA KAGASHEKI YAANZA LEO HII KWENYE UWANJA WA KAITABA BUKOBA. TIMU YA HAMUGEMBE IKITANDIKWA NA BAKOBA BAO 1-0

Balozi Khamis Kagasheki  akisalimiana na wachezaji muda mfupi kabla ya mtanange kuanza
Balozi Khamis Kagasheki  ndiye anadhamini mashindano haya na hapa akisalimiana na wachezaji




Kikosi cha Timu ya Hamugembe
Kikosi cha timu ya Bakoba
Waamuzi wa mchezo huu wa Bakoba na timu ya Hamugembe
Wachezaji wa Hamugembe wakishangilia kwenda kuanza kandanda
Mchezo ukaanza kati

Wadau wakifatilia mechi hii ya ufunguzi leo hii kwenye uwanja wa Kaitaba



Furaha ikatanda uwanjani Kaitaba baada ya timu ya Bakoba kufunga bao

MAGUFULI AUTAMANI URAIS 2015


 Katika hali inayoonyesha kuwa Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, anautamani urais, amesema anaweza kutangaza nia hiyo kama atakidhi masharti yatakayowekwa kwenye Katiba mpya.

Alisema iwapo Katiba ijayo itakuja na sifa ambazo atakidhi vigezo kuna uwezekano mkubwa wa kuwania nafasi hiyo na kwamba iwapo atapungukiwa sifa zinazohitajika kwa mujibu wa Katiba hataingia kwenye kinyang’anyiro hicho.

Dk. Magufuli ambaye pia ni Mbunge wa Chato alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wazee wa wilaya hiyo kwenye ukumbi wa ‘Mshikamano Saccos’, muda mfupi baada ya mzee Paschal Nyambibo (87) kumsihi agombee nafasi hiyo mwaka 2015 kutokana na sifa zake za uchapakazi ndani ya serikali.

Nyambibo alisema kutokana na uwajibikaji mzuri aliouonyesha Dk. Magufuli tangu mwaka 2000 akiwa Naibu Waziri wa Ujenzi na katika wizara mbalimbali, Watanzania wamekuwa na imani kubwa na uwajibikaji wake na kwamba anastahili kupeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ifikapo mwaka 2015.

Licha ya kauli hiyo kusababisha minong’ono mingi kwa wazee waliohudhuria kikao hicho, Dk. Magufuli alionekana kutuliza hali hiyo kwa kusema isubiriwe Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano iwapo itakuwa na masharti ambayo yatamfanya kujitathimini iwapo ana sifa za kugombea au vinginevyo.

Hata hivyo, Dk. Magufuli hakusita kuonyesha hisia zake za kukerwa na baadhi ya wananchi wanaobeza maendeleo aliyotekeleza katika jimbo lake tangu alipochaguliwa kuwa Mbunge.
Alimshutumu hadharani aliyekuwa Katibu wa CCM wilaya ya Chato kabla ya kuhamishiwa wilayani Mbogwe, Gervas Stephano, kuwa hana shukrani.

Dk. Magufuli alimwelezea katibu huyo kuwa hana fadhila kutokana na mambo mengi aliyomtendea tangu akiwa katibu wa ofisi yake ya jimbo ambapo alimsaidia kupanda ngazi na kuwa Katibu wa CCM wilaya Chato, Kwimba, Kasulu, Kilosa na kurejea tena Chato kabla ya kuhamishiwa wilaya ya Mbogwe mkoani Geita  kuendelea na wadhifa huo.

“Tatizo lenu watu wa Chato hamna shukrani…mambo mengi nimefanya hapa Chato, lakini yote mnaona ziro…hata niliowasaidia kama Gervas naye sasa hivi ananiponda…lakini nawashukuru sana wazee wangu kwa kunikumbusha niliyoyafanya kwenye jimbo letu kupitia risala yenu nzuri,” alisema Dk. Magufuli.

“Kutokana na hali hiyo ninawazawadia Sh. 1,000,000 mfanye sherehe ya kujipongeza kwa kuwa natambua mmejitesa sana mpaka kufanikisha kikao hiki cha leo…na kwa kuwa hamna mradi wowote wa kuwaingizia kipato kama wazee, ninaahidi kuwapa Sh.   3,000,000 kutoka mfuko wa jimbo, ili muanzishe walau saccos ya kukopeshana,” alisema.

Baadhi ya viongozi na wananchi wamekuwa wakilitaja mara kwa mara jina la Waziri Magufuli miongoni mwa watu wanaodhaniwa kutaka kugombea nafasi ya urais wa Tanzania mwaka 2015, ingawa mwenyewe amekuwa akikanusha uvumi huo.

Mbali na Dk. Magufuli, wengine ndani ya CCM wanaotajwa  ni pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa; Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, ambaye anajiita mtaji wa urais; Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe; Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Ushirikiano wa Kimataifa –CCM, Dk. Asha-Rose Migiro na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano na Mambo ya Nje, Bernard Membe, ambaye alipata kusema anasubiri kuiteshwa na Mungu kuwania nafasi hiyo.

Friday, 5 July 2013

NDOYA YA DIAMOND NA PENNY IMEIVA

 Diamond & Penny
SIYO siri kwamba wapenzi wasio na kificho, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Penny Mungilwa wana malengo ya kuja kuishi kama mke na mume lakini maajabu ni namna mwanamuziki huyo alivyopanga sherehe ya ndoa yao iwe siku ikifika. 
 
Akizungumza na gazeti la Ijumaa hivi karibuni, Diamond alisema kuwa yamekuwepo maneno ya chinichini kuwa ameshatoa mahari na siku si nyingi ataingia kwenye maisha ya ndoa ila ukweli ni kwamba kila kitu kinafanyika kwa umakini na mashabiki watajulishwa hatua kwa hatua.
  
“Suala la ndoa yangu nalifanya kwa umakini sana, watu wawe na subira tu ila wanachotakiwa kujua ni kwamba nina plani za kuifanya sherehe ya ndoa yangu kwenye Uwanja wa Leaders Club, pale Kinondoni na watu wataingia kwa kiingilio kisichopungua shilingi elfu kumi (10,000). Itakuwa ni ndoa ya Wasafi bana,” alisema Diamond.

RAIS KIKWETE KUWA REFA TAMASHA LA MATUMAINI


Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.
Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, amekubali kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Usiku wa Matumaini litakalo fanyika Jumapili hii, Julai 7 katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Aidha, Rais atahutubia katika tamasha na pia atakuwa refa wa mechi za wabunge wa Yanga na Simba.

MA PETRONIDA MPILLA HATIMAE AFIKISHA MIAKA 60 YA UTUMISHI WA UMMA ,APONGEZWA NA WAFANYAKAZI HOSPITALI YA MKOA,WANAWE,WAJUKUU, NDUGU NA MARAFIKI

 Ni siku ya historia katika maisha ya  ma Petronida mpilla kustaafu kazi salama akiwa  mtumishi wa serikali,ma petronida amitimiza miaka 60 akiwa kazini na sasa amestaafu,katika kipindi chote cha utumishi amekuwa akifanya kazi katika hospitali ya mkoa wa kagera na mpaka anastaafu alikuwa amefikia cheo cha daktari,katika kutoa shukrani katika sherehe ya kumpongeza amewashukuru wafanyakazi wote ambao amekuwa nao kwa kipindi chote cha utumishi wake,ma petronida mpilla akiwa na furaha aliwasimamisha wanae na wajukuu ukumbini hapo ili wageni waalikwa waweze kuwatambua, Ma petronida sasa amestaafu rasmi.

                                                    ma  petronida akiingia ukumbini
                                        wajukuu wa ma petronida wakijiandaa kuingia ukumbini
                                 wajukuu wakiingia ukumbini kwa kucheza kumpongeza bibi yao
                                                          chezeaa wajukuu weweee
                                                                    ni wakati wa keki
                                                          mjukuu khadija jamal katokelezea
                                                          bibi  petronida akiwasha mshumaa
                             maelekezo ni muhimu kutoka kwa mwanae jamira jamal (kushoto)
                                                                       keki ikakatwa
                                                mdogo mtu nae akawajibika kwa dada
                                                                   wageni wakifuatilia matukio
                                                       wajukuu wakilishwa keki na bibi



 ukafika wakati wajukuu na watoto wakaonyesha ujuzi katika kusakata rumba  usiombee ilikuwa ni balaaaaaa
                                                   ashura ashiraf nae ndani ya nyumba
                                watoto wa ma peto hawa ni mapacha awaachani hata ukumbini ni benet
                                           ikafika wakati ikapingwa ngoma
                                                        u wakaruka juu na kushuka
                                                       ni vijimambo tu katika ngoma
                                              ma peto akasalimia wageni wote na kuwashukuru kwa kufika
                                                                                 mapozzzzz
                             watoto wa ma peto nao wakaselebuka ,nakwambia ilikuwa rahaaa
                                                         daktari mfawidhi akatoa neno
                                                      wajukuu wakaibuka na zawadi ya bibi
                                                            watoto wakaibuka na friji
                                                            mama akakabidhiwa jokofu
                                       wakwe nao wakazuka,jiko la gesi na pochi zikatolewa
                                             wageni waalikwa nao wakaja kutoa zawadi

                                                                 misosi time
                                                                yazidi( mkwe)
                                                       picha ya pamoja,watoto,ndugu na jamaa
                                                                         mapozzzz
                                                                   ongera mama
                                                                 ongera sana mama
                                                   dah wajukuu vituko vingi
mama jamcobukoba.blogspot.com tunakupongeza kwa kuitumikia serikali  na jamii katika utumishi uliotukuka wa miaka 60,mungu akuongoze katika maisha yako mapya katika jamii na hasa hapo nyumbani kitendaguro,ongera sana