Sunday 8 July 2018

OMWAMI MA HELENA RUGAIBULA KIFO CHAKE CHA ACHA SIMANZI,AFARIKI MASAA MACHACHE BAADA YA MME WAKE KUZIKWA.

 Ni moja ya tukio ambalo halijazoeleka sana katika jamii ambalo lilitokea katika familia ya Omulangira Rugaibura baada ya Omulangira Adeodatus Rugaibula kuzikwa tarehe 2/7/2018 na mke wake kufariki dunia tarehe 3/7/2018 saa nne na nusu usiku katika hospital ya Rufaa Kagera. Ilikuwa ni pigo kubwa kwa familia , ndugu ,jamaa na marafiki kwa msiba huo wa ghafla sana. Omwami Ma Helena baada ya kupta taarifa ya kifo cha mme wake kilichotokea Jijini Dar tarehe 28/6/2018 katika hospital ya Taifa Muhimbili, alipata mstuko uliopelekea kulazwa na kutoshuhudia  mapokezi ya mwili wa mme wake na mazishi.Tulikupenda sana Omwami Ma Helena Rugaibula ila mungu amekupenda zaidi.(katika picha ni watoto wa marehemu ambao kwa sasa ni yatima.)
 Ng'ombe walipata taabu sana.
 Kulia ni mtoto mkubwa wa marehemu Deo akiwa na mdogo wake Dvo wakitete jambo kabla ya ibada ya mazishi.
 Rambilambi zikitolewa kabla ya misa ya mazishi kuanza.
 Mandalizi ya ibada ya mazishi ikiongozwa na baba Askofu Methodius Kilain.
 Watoto wa marehemu.
 Kushoto ni stahiki Meya Manispaa Bukoba Chief Kalumuna akiwa na Mzee Pius Ngeze mwenyekiti Mstaafu wa ccm Mkoa wa Kagera.

 Kulia ni Mh Mbunge wa jimbo la Nkenge Diodorus Kamala akiwa katika ibada ya mazishi.
 Kushoto Ni Mama Ailen akiwa na Anitha waolewaji katika fami Rugaibula.lia ya
 Waombolezaji.
 Wakati wa kutoa heshima za mwisho
 Mkurugenzi wa bohari ya dawa Nchini Laurian Rugabwa akisoma historia fupi ya maisha ya marehemu.
 Mwenyekiti wa chama cha mawakili Mkoa Kagera Alon Kabunga akiwasilisha rambirambi.
 Wanafamilia wakiaga mwili.
 Bw Optat Rwebugisa akitoa rambirambi za wanapamoja group.
Pumzika kwa amani Ma Helena Rugaibula, tulikupenda sana ila mungu kakupenda zaidi.