Thursday, 7 May 2015

ZOOM POLYTECHNIC COLLEGE AND DAN COMPUTER INSTITUTE YAFANYA MAHAFALI YA TATU,KAGASHEKI MGENI RASMI

 Kushoto ni mgeni rasmi Balozi Khamis Kagasheki, Mkugenzi wa chuo Bw Abdul na  mkuu wa chuo Bw Najimu bwanika katika mahafali ya tatu ya chuo cha Dan  Computer Institute, wahitimu zaidi ya 90 wamehitimu masomo kwa kiwango  cha cheti na diploma.Hawali wakisoma risala kwa mgeni rasmi Mkurugenzi wa chuo amesema wanao upungufu  wa vyumba vya madarasa viwili na walimuomba mgeni rasmi awasaidie kuendesha harambee kwa wageni waalikwa, Akijibu risala hiyo Balozi Kagasheki ambae pia ni mbunge wa jimbo  la Bukoba Mjini amehaidi kujipanga vizuri na kuandaa harambee itakayoleta tija kwa kuweka utaratibu mzuri wa kushirikisha watu mbalimbambali wa ndani na nje ya Mkoa wetu ili kupata ufanisi zaidi, pia amewapongeza wahitimu na kuwataka kuwa mfano bora kwa jamii na kuitumia elimu waliyoipata iweze kuwa na tija kwa jamii na kikubwa amewasihi wahitimu kuwa na nidhamu ndio msingi mkubwa katika jamii na maisha yao.
 Mmoja wa wanafunzi akitoa maelezo kwa mgeni rasmi.
 Mkurugenzi wa Buwasa Bw Chagaka akisalimiana na mgeni rasmi.
 Mwenyekiti wa Bodi ya chuo akifungua sherehe.
 Wanachuo waliohitimu.
 Wazazi.
 Wahitimu wakisoma risala yao.
 Mkuu wa chuo bw Najimu Bwanika.
 Mhasibu wa chuo.
 Bw Almasoud Kalumuna.
 Hongera.
 Mgeni rasm akitoa hotuba yake.
 Hongera mwanangu.
 Baba na mama wakimpongeza mtoto.
Endelea kuangalia jamcobukoba.blogspot.com