Saturday, 24 August 2013

MADIWANI 8 WA CCM MANISPAA YA BUKOBA NI HALALI

Habari zilizotufikia hivi punde kutoka dodoma , kamati kuu ya chama cha mapinduzi taifa imesema madiwani waliokuwa wamefutiwa uanachama na nyadhifa zao ni halali, tutawaleteahabari zaidi badae

BALOZI KHAMIS KAGASHEKI ADHAMINI MRADI WA PIKIPIKI ZA MKOPO 102 AINA YA TOYO CHAMA CHA WAMILIKI NA WAENDESHA PIKIPIKI ZA BIASHARA NA MAENDELEO MANISPAA YA BUKOBA(CPMB)

 Mbunge wa jimbo la bukoba manispaa balozi khamisi kagasheki waziri wa maliasili na utalii akiongea na wamiliki na waendesha pikipiki wa CPMB leo katika viwanja vya uhuru platform bukoba, balozi kagasheki amedhamini chama hiki kupata pikipiki 102 kutoka katika kampuni ya KISHEN ENTERPRISES ikiwa ni pamoja  na kutanguliza kiasi cha pesa  iliwaweze kutoa pikipiki hizo,awali balozi kagasheki amegharamikia gharama zote za chama hiki kuandaa katiba mpaka usajili ili kiwezekutambulika na kukopesheka, leo la mradi huu ni baada ya muda mwanachama anapomaliza mkopo ndani ya muda mfupi anamiliki mwenyewe pikipiki na kukopa nyingine,balozi kagasheki amesema mradi huu utawawezesha vijana na wanachama kujiajili na kuendasha maisha yao ya kila siku.
 maandamano ya waendesha pikipiki yakipita mitaa mbalimbali ya manispaa ya bukoba kuelekea uwanja wa mayunga bukoba
                                         ni mtaa kwa mtaa kufurahia uzinduzi
                                         balozi kagasheki akipokea msafara
 balozi kagasheki akikata utape kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa pikipiki 102 za mkopo kwa wanachama
 mwenyekiti wausalama barabarani mkoa wa kagera bw kabantega akiwa na akiwa na kamanda wa trafiki(RTO) mkoa wa kagera
                                                       baadhi ya pikipiki zilizokabidhiwa leo
                               bidhaa mbalimbali zinazouzwa na kampuni ya kishen enterprises
                                   burudani pia zilikuwepo msanii babu rweyemamu na kundi lake
                                                                                      viongozi wa CPMB
 WAANDISHI WA HABARI  NI JERRY MULO WA TBC AKITETA NA MKURUGENZI WA KASIBANTE REDIO RICHARD LEO AMBAE ALIWAHI KUWA MFANYAKAZI WA TBC
                                                   Viongozi jukwaa kuu
 mwakilishi wa kampuni ya kishen enterpises akieleza utatatibu mzima ulivyokuwa ambae pia ni mwanasheria wa kampuni,amemshukuru balozi kagasheki kwa kutimiza mashariti ya kampuni na leo wanatoa pikipiki katika chama
 mwenyekiti mlezi wa chama cha CPMB  Mzee Samweli ruangisa akimshukuru mbunge kwa jitihada za maendeleo anazozifanya
                 balozi kagasheki akiongea na wanachama cha CPMB  na wananchi viwanja vya mayunga
                                                        wadau mbalimbali wakimsikiliza mbunge
                                             bidhaa mbalimbali za kisheen enterpises
                                                           mh karibu uzindue
                                                    PIKIPIKI YA TOYO NI KIBOKO ....
                                                 Balozi kagasheki akimkabidhi pikipiki mmoja wa wanachama
                        mwandishi wa habari Audax Mtiganzi akifanya mahojiano na balozi kagasheki
 balozi akiteta na RTO kagera na mwenyekiti wa usalama barabarani mkoa wa kagera bw kabantega
                                  jamco akiwa na jerry mulo wa tbc baada ya kazi ya uzinduzi
bw mganyizi mlezi wa chama cha CPMB akiwa na balozi kagasheki na bw andasoni wa nyamkazi

27 WAUAWA, 350 WAKIJERUHIWA KATIKA MILIPUKO NCHINI LEBANON


Mwananchi huyu akchukua picha katika simu yake ya mkononi.
Wananchi wakiangalia uhalibifu uliotokea baada ya mlipuko.
Wananchi wakiwa wamekusanyika eneo la mlipuko nje ya msikiti wa Sunni uliopo jijini Tripoli, Lebanon.
Magari yaliyohabiriwa katika mlipuko huo.MILIPUKO mikubwa miwili imetokea leo nje ya misikiti katika jiji la Tripoli lililopo Kaskazini mwa Lebanon jirani na Syria. Katika milipuko hiyo, watu 27 wanadaiwa kupoteza maisha, wakati 350 wakijeruhiwa. Milipuko hii imeongeza mvutano nchini Lebanon ikiwa ni matokeo ya vita ya wenyewe kwa wenyewe inayoendelea nchini Syria kati ya wafuasi na wapinzani wa utawala wa Rais wa Syria, Bashar Assad.

FILAMU YA LULU YAPIGWA STOP KUINGIA SOKONI





Msanii wa filamu Elizabeth Michael (Lulu) akiweka sahihi yake kuashiria amekubaliana na taratibu zote alizoelekezwa na Bodi ya Filamu wakati wa ukaguzi wa filamu yake ya “Foolish Age”.PIX 1 

Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo akiwaonyesha wajumbe pamoja na wahusika wa Kampuni ya Proin Promotions baadhi ya maeneo muhimu ya kufanyiwa marekebisho wakati walipowasilisha filamu yao ya “Foolish Age” katika Bodi ya Filamu kwa ajili ya ukaguzi. PIX 2

Msanii wa filamu Elizabeth Michael (Lulu) akieleza jambo mbele ya Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo wakati kampuni ya Proin Promotions ikiwasilisha filamu yake ya “Foolish Age” kwa ajili ya ukaguzi. Bodi ya ukaguzi wa filamu na michezo ya kuigiza nchini imeipiga stop filamu ya Foolish age ya msanii wa kike mwenye mvuto Bongo Elizabeth Michael ‘Lulu’ baada ya kukuta picha zilizo nje ya maadili ya Kitanzania katika filamu hiyo....

Filamu hiyo ambayo ilipanga kuzinduliwa mwezi huu tarehe 30 katika ukumbi wa Mlimani City inahitaji marekebisho.

Kikwazo kilichoikumba filamu hiyo ni nguo fupi zilizotumiwa na waigizaji walioshiriki katika filamu hiyo ambayo inatabiriwa kufanya vizuri katika soko la filamu Bongo kama itafanikiwa kuzinduliwa na kuingia sokoni, Kwa  mujibu  wa  Lulu  Michael,  juhudi zinafanyika kuhakikisha kuwa marekebisho yanafanyika ili kwenda na ratiba kama ilivyopangwa.

DOUBLE TREE BY HILTON DAR ES SALAAM YAGAWA TAA 200 NA KUTOA MAFUNZO KWA WANAFUNZI JUU YA MATUMIZI YA UMEME WA NISHATI YA JUA.


DSC_0240
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Angellah Kairuki (Mb) akitoa risala yake kwenye hafla ya kukabidhi Taa 200 za Nishati ya Jua kwa Shule ya Msingi Mji Mpya iliyopo Mabwepande ikiwa ni mwendelezo ya kampeni iliyozinduliwa na Hoteli ya DoubleTree By Hilton jijini Dar kwa wanafunzi wa shule za msingi ambapo ameipongeza hoteli hiyo kwa kubuni kampeni kama hiyo kwani Taa hizo ni rafiki wa mazingira kwa kuwa zinatumia Nishati ya Jua zitawasaidia wanafunzi kujisomea na familia zao pia kupata Mwanga kunapokuwa tatizo la kukatika kwa Umeme na pia itaongeza ufaulu kwa Wanafunzi kwa sababu watakuwa wanauwezo wa kujisomea nyakati za usiku.
Aidha amewaasa wanafunzi hao kuzitunza taa hizo na kuzitumia kwa maelngo yaliyokusudiwa. Kushoto ni Mwenyekiti wa bodi ya Shule hiyo Epimack Vinivuni na Kulia ni Meneja Mkuu wa Hoteli ya Double Tree by Hilton Rode Perk pamoja na Mkurugenzi wa Mauzo wa Hoteli ya Double Tree by Hilton Florenso Kirambata (wa pili kulia).
DSC_0234
Mkurugenzi wa Mauzo wa Hoteli ya Double Tree by Hilton Florenso Kirambata (katikati) akitoa maelezo ya jinsi ya kutumia taa ndogo za mezani zinazotumia Nishati ya Jua na umuhimu wake tofauti na kutumia Mafuta ya Taa kwa Wanafunzi wa darasa la saba wa shule ya msingi ya Mji Mpya wakati uongozi wa hoteli hiyo ulipotembelea shule hiyo iliyopo Mabwepande kwa nia ya kuendesha mafunzo na kugawa Taa 200 bure kwa Wanafunzi hao. Kushoto ni Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Angellah Kairuki (Mb) na Kulia ni Meneja Mkuu wa Hoteli ya Double Tree by Hilton Rode Perk.
DSC_0249
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Angellah Kairuki (Mb) akikabidhi rasmi Taa hizo kwa mmoja wa Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mji Mpya iliyopo Mabwepande leo jijini Dar. Katikati ni Mkurugenzi wa Mauzo wa Hoteli ya Double Tree by Hilton Florenso Kirambata na Kulia ni Meneja Mkuu wa Hoteli ya Double Tree by Hilton Rode Perk.
DSC_0229
Mwenyekiti wa bodi ya Shule hiyo Epimack Vinivuni akitoa shukrani kwa uongozi wa hoteli ya Double Tree by Hilton kwa kuwa na mkakati madhubuti wa kuwaelimisha vijana umuhimu wa matumizi ya Umeme mbadala wa Nishati ya Jua ambao ni rafiki wa mazingira.
DSC_0226
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mji Mpya Davis Mkaruka akizungumza baada ya mafunzo yaliyolewa na Double Tree by Hilton kwa wanafunzi wa darasa la saba akisema ilikuwa ni njia nzuri ya kuwaelimisha watoto juu ya nishati ya jua na kuwa wamefurahi kupewa bure taa ndogo za mezani ambazo ni rahisi kutumia na zina faida nyingi kwao na familia zao.
DSC_0253
Wanafunzo hao wakifurahia Taa ndogo la ‘Solar Energy’ walizopewa. Nyuma ni Bw. Florenso Kirambata na Meneja Mkuu wa hoteli ya Double Tree by Hilton Hotel Rode Perk.
Hoteli ya Double Tree by Hilton Dar es Salaam leo imefanya ziara katika Shule ya Msingi Mji Mpya iliyopo Mabwepande kwa lengo la kuendesha mafunzo kwa wanafunzi wa darasa la saba kuhusu umuhimu wa umeme wa nishati ya jua.
Mafunzo hayo ni sehemu ya mkakati wa Double Tree by Hilton wa miaka miwili wa kuwakufahamisha na kuwashirikisha wanafunzi juu ya faida za nishati ya jua tofauti na matumizi ya mafuta ya taa, kuni na vyanzo vingine vya mwanga ambavyo vina madhara kwa mazingira, afya na vifaa vya nyumbani.
Katika ziara hiyo shule hapo Hoteli ya Double Tree by Hiltonimegawa kwa wanafunzi hao taa ndogo za mezani 200 zinazotumia nishati ya jua, ambazo wanafunzi hao wamekwenda nazo majumbani kwao kuzitumia kusomea usiku kwa faida yao na familia yao.

Friday, 23 August 2013

WAJUMBE WA NEC KUTOKA ZANZIBAR NA DAR, WAENDA DODOMA LEO



 Wajumbe wa NEC ya CCM kutoka Zanzibar na mjini Dar es Salaam, wakiwa tayari kuondoka kwa basi la kukodi kutoka Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya safari ya kwenda mjini Dodoma kushiriki kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, kinachoanza kesho .
 Ofisa Utawala wa CCM, Mary Nchimbi, akiwaambia abiria kuwa tayari kwa safari
 Wajumbe wa NEC na baadhi ya maofisa wa Chama wakiwa kwenye gari
Wajumbe wa NEC na baadhi ya maofisa wa Chama wakiwa kwenye gasi leo asubuhi.

MWENYEKITI WA CCM AWASILI DODOMA,AFUNGUA KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU TAIFA



 Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mkono Viongozi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi waliofika uwanjani kumlaki.
 Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana .
 Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma na Mjumbe wa Kamati Kuu Ndugu Adam Kimbisa.

 Mwenyekiti wa CCM Taifa , Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Ndugu Khamis Sadifa Juma.

 Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mtumishi wa Chama Cha Mapinduzi  ndugu Octavian Kimario .
 Watumishi na wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakishangilia kwa furaha ujio wa Mwenyekiti wa CCM Taifa , Rais Jakaya Mrisho Kikwete mara tu alipowasili Dodoma tayari kwa Mkutano wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu Taifa ya Chama.


 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akibadilishina mawazo na Mjumbe wa Kamati Kuu Ndugu Stephen Wassira kabla ya Kikao cha Kamati kuanza leo Dodoma kwenye Ukumbi wa NEC.
 Wajumbe wa Kamati Kuu wakijadiliana jambo ndani ya ukumbi wa NEC kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu,Dodoma 23 Agosti 2013.
 Mjumbe wa NEC, Prof. Anna Tibaijuka akipitia Katiba ya Chama kabla ya kuanza kwa Kikao cha Kamati Kuu ndani ya ukumbi wa NEC.
Mwenyekiti wa CCM Taifa,Rais Jakaya Mrisho Kikwete ,akifungua kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa CCM,Kushoto kwake ni Makamu wa CCM Zanzibar Ali Mohamed Shein na kulia ni Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana.