Saturday 13 December 2014

MWIGULU NCHEMBA AFUNGA KAMPEINI KATA YA KASHAI,AMSIMIKA KAMANDA WA VIJANA WA MANISPAA YA BUKOBA PHILBERT KATABAZI NYERERE.

 Naibu Katibu wa siasa na uenezi Taifa ambae pia ni (MB) Naibu waziri wa fedha Mh Mwigulu Nchemba amewataka na kuwaomba wananchi kuwapa kura za ndio wagombea wote wa chama cha mapinduzi katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika nchini 14-12-2014,akiongea kwa kujiamini ,Mh  Mwigulu amesema serikali iliyoko madarakani ni ya CCM  hivyo ili iweze kutekeleza ilani ni vizuri mkawachagua viongozi wa ccm,pia amemsimika kamanda wa vijana wilaya ya Bukoba Mjini Bw Philibert Katabazi Nyerere,mmoja wa wafanyabiashara wa Manispaa ya Bukoba.
 Chopa anayotumia Naibu katibu wa siasa na uenezi Mh MWIGULU.
 Ni katika viwanja vya kashai shule ya msingi ilipotua chopa.
 Gari la wazi alilopanda mh Mwigulu kuelekea viwanja vya mkutano.
 Katibu wa ccm Manispaa ya Bukoba akiongea na wananchi.
 Waandishi wakifuatilia habari.
 Mwenyekiti wa ccm manispaa ya Bukoba Yusuf Ngaiza akihutubia wananchi.
 MNEC wa Manispaa ya Bukoba Abdul Kagasheki.
 Mgombea wa uenyekiti mtaa wa kashai harisi  maarufu kwa jina la Rugambwa akiomba .kura
 Ukafika wakati wa kumsimika kamanda wa Wilaya.
 Kam,anda Philibert Nyerere akasimikwa.
 Mh Mwigulu akiteta na kamanda wa vijana kata ya Miembeni Jamal Kalumuna.
 Mh Diwani viti maalum Mwajabu Galiatano  akiamasisha akina mama kuwapa kura za ndio ccm.

 Hawa ndio wagombea uwenyekiti mitaa yote kata ya kashai.
 Kamanda wa Vijana wa wilaya akimnadi mgombea uenyekiti kashai halisi.
 Kamanda akimnadi mzee Robya.
 Kamanda akimnadi mzee Abibu mayolo.
 Kamanda akimnadi cryspiline.
 Alie kuwa mwenyekiti wa kashai halisi ,mzee Kikoti akimkabidhi  viatu vyake bw Rugambwa kama ishara ya kuamini viatu vyake vinamtosha aendeleze jahazi.
 Kamanda wa vijana wilaya Phiribert Katabazi Nyerere akieleza  namna walivyojipanga kuzibiti wale wte waliojiandikia eneo zaidi ya moja, na wale wote ambao si wakazi wa eneo husika.
 Wagombea ujumbe wa mitaa wakiomba kura.
 Burudani.
Mmoja wa wagombea ujumbe wa mtaa akiomba kura kwa wananchi kata ya Kashai,jamcobukoba.blogspot.com inawatakia uchaguzi mwema na amani na upendo vitawale.