Friday 21 June 2013

Friday, June 21, 2013 MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWEKA JIWE LA MSINGI KWENYE ENEO MAALUM LA UWEKEZAJI LA TANGA ECONOMIC CORRIDOR SEZ


Friday, June 21, 2013


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wakazi wa jijini Tanga, wakati alipofika eneo la Pongwe jijini Tanga leo Juni 21, 2013 kwa ajili ya kuweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa Viwanda katika eneo hilo maalum  la Uwekezaji la Tanga Economic Corridor Sez, linalosimamiwa na Wawekezaji kutoka nchini Korea Kusini.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Viwanda, katika eneo maalum la Uwekezaji la Tanga Economic Corridor Sez, wakati wa sherehe hizo zilizofanyika leo Juni 21, 2013 jijini Tanga. Kushoto kwa Makamu ni Mwenyekiti wa Bodi ya Tanga Economic Corridor Ltd, Chris Incheul Chae
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Viwanda, katika eneo maalum la Uwekezaji la Tanga Economic Corridor Sez, wakati wa sherehe hizo zilizofanyika leo Juni 21, 2013 jijini Tanga. Kushoto kwa Makamu ni Mwenyekiti wa Bodi ya Tanga Economic Corridor Ltd, Chris Incheul Chae
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa, Mwenyekiti wa Bodi ya Tanga Economic Corridor Ltd, Chris Incheul Chae na viongozi wengine kwa pamoja wakifurahia baada ya Makamu kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Viwanda, katika eneo maalum la Uwekezaji la Tanga Economic Corridor Sez, wakati wa sherehe hizo zilizofanyika leo Juni 21, 2013 jijini Tanga
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda Mti wa kumbukumbu katika eneo maalum la Uwekezaji la Tanga Economic Corridor Sez, baada ya kuweka rasmi Jiwe la Msingi la ujenzi wa viwanda katika eneo hilo wakati wa sherehe hizo zilizofanyika leo Juni 21, 2013 jijini Tanga
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa ramani ya ujenzi wa Viwanda hivyo, mara baada ya uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Viwanda, katika eneo maalum la Uwekezaji la Tanga Economic Corridor Sez, wakati wa sherehe hizo zilizofanyika leo Juni 21, 2013 jijini Tanga
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa baadhi ya vifaa kama Solar Cooker, ambavyo ni baadhi ya vitakavyokuwa vikizalishwa katika Viwanda hivyo baada ya kukamilika, mara baada ya uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Viwanda, katika eneo maalum la Uwekezaji la Tanga Economic Corridor Sez, wakati wa sherehe hizo zilizofanyika leo Juni 21, 2013 jijini Tanga.
 Makamu wa Rais na baadhi ya Viongozi, wakishirikiana kurusha mchanga ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa ujenzi wa viwanda hivyo.
 Makamu wa Rais na baadhi ya Viongozi, wakishirikiana kurusha mchanga ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa ujenzi wa viwanda hivyo.
                                                                     Picha ya pamoja

BAADA YA MCHUANO MKALI KATIKA MIKOA SITA YA KANDA YA ZIWA SASA REDD'S MISS LAKE ZONE KUFANYIKA 29-06-2013




Ni kitimutimu cha redd's miss lake zone 2013 kitakachofanyika jijini mwanza 29-06-2013 katika ukumbi wa gold crest hotel,warembo watatu kutoka kila mkoa katika mikoa sita ya kanda ya ziwa watachuana kuwapata watatu ambao watakwenda kwenye mashindano ya taifa,mbali na mchuano mkali utakaokuwepo,pia zitakuwepo burudani kutoka kwa ommy dipoz na machael ross. ili uweze kushuhudia mtanange huu itakurazimu uzinasue shilingi za kitanzania elfu ishirini nafasi za kawaida na elfu arobaini kwa nafasi za vip. kwa mujibu wa mkurugenzi wa kampuni ya clara salon & boutique  ndugu clara mwasa  kambi inaanza rasmi 23-06-2013 na waratibu wote wa mikoa wameshapewa maelekezo ya kambi itakuwa wapi.

Thursday 20 June 2013

BONANZA KUBWA KUFANYIKA JUMAPILI 23-06-2013 KATKA UWANJA WA KAITABA BUKOBA MANISPAA


 Bonanza kubwa litafanyika siku ya jumapili katika uwanja wa kaitaba,kwa mujibu wa mwenyekiti wa bukoba veteran ndugu erenest nyambo bonanza hilo litaanza  saa nne kamili asubuhi kwa mchezo wa mpira wa miguu  kati ya timu ya kahawa V/s Banana, na timu itakayoshindwa italazimika kupata adhabu ya kutoa huduma ya supu na chakula cha mchana kwa timu itakayoshinda. mara baada ya mpambano huu timu zote zitaelekea kwenye ufukwe wa kiroyera ambako zitakuwepo burudani mbalimbali ukiwemo mpambano wa kucheza draft kati ya kahabuka na kingereza, katika kusherehesha bonanza hilo hapo ufukweni utakuwepo muziki mkubwa huku moses nyama (farry ipupa) ambae takribani wiki moja sasa karejea kutoka nchini dernmark atakuwa akifanya vitu vyake.Bonanza hili limedhaminiwa na TBL na ni muendelezo wa kila mwezi litakuwa likifanyika na michezo mbalimbali itachezwa

 waliochuchumaa wa tatu  ni moses nyama (farry ipupa) mwana veterani bukoba ,msanii wa kakau band ambae karejea hivi karibuni kutoka dernimark atatoa burudani

 Ni timu ya netball ya bukoba ,kipindi kijacho utakuwepo mchuano wa netball kama walivyosema TBL kuwa bonanza litakuwa likifanyika kila mwe

                                michezo ni afya,michezo ni upendo, michezo ni furaha
 Aliekaa kwenye bench wa kwanza kushoto ni ndugu kahabuka ambae atapambana  na kingereza katika mchezo wa draft katika ufukwe wa kiroyera
                                                                     wanaveterani bukoba
                                    nyuma ya amin  ni thomas,na nyuma ya thomas ni kirimanjaro

                                                   si mchezo patakuwa hapatoshi kaitaba
                                                               dada zetu wapenda michezo
                                                                                asante mwalimu...

MAONYESHO YA 13 YA SABASABA KUZINDULIWA RASMI 26-6-2013 KATIKA VIWANJA VYA JENGO LA CCM BUKOBA MANISPA



Maandalizi ya maonyesho ya 13 ya saba saba mwaka huu yanaendelea vizuri katika jengo la ccm,maonyesho hayo yanayoratibiwa na kampuni ya KAIDEP yatazinduliwa 26-6-2013,kwa mujibu mratibu philimon  kamazima zaidi ya makampuni  mia mbili wanategemea yashiriki yakiwemo na makampuni kutoka nchini uganda,kenya,burundi na rwanda. lakini pia wajasiria mali mbalimbali  wanaosindika bidhaa za hapa nchini watashiriki.

 watu wameanza kupimiwa maeneo ili wajenge vibanda vya muda kwa ajili ya biashara zao
 jengo hili ni la chama cha mapinduzi ambalo limekuwa likitumika katika shughuli mbalimbali hapa buko

                              ni nje ya jengo la ccm,mama huyu mtaalamu wa kuchoma gonja


karibu kwenye maonyesho ya sabasaba ewe mjasiriamali,ni wakati muafaka kuonyesha unachokifanya,au kuzalisha,lakini pia na wakati wa kujifunza mengi

Wednesday 19 June 2013

WAFUASI WA CHADEMA BUKOBA WAPATWA NA BUTWAA UWANJA WA NDEGE BUKOBA,BAADA YA RWAKATARE KUTOONEKANA AKISHUKA KWENYE NDEGE NA KUTAWANYIKA NA BAADA YA MUDA RWAKATARE AKAONEKANA MTAANI AKIELEKEA UWANJA WA UHURU BUKOBA

 Ni majira ya saa sita na nusu mchana katika uwanja wa ndege wa bukoba wafuasi wa chadema walikuwa wakifika katika maeneo hayo wakiwa na mabango,baiskeli ,pikipiki na wengine kwa magari na miguu kuja kumpokea wilfred rwakatare mwenyekiti wa chadema mkoa wa kagera ambae alikuwa gerezani siku 92 ,katika hali ya kushangaza mara baada ya ndege kuwasili uwanja wa ndege bukoba katika ndege hiyo walishuka abiria watatu na miongoni mwao rwakatare hakuwepo,na habari zilienea uwanjani hapo kuwa hakuna ndege yoyote itakayotua tena maana kuanzia saa nane mkandarasi wa uwanja anaendelea na ujenzi wa uwanja,hali hiyo ilisababisha watu kuondoka uwanjani hapo kwa kujiuliza maswali mengi ambayo majibu yake hayakuwa rahisi,mara baada ya muda,wafuasi walitangaziwa na mwenyekiti wa chadema wilaya ya bukoba ndugu sherejei kuwa  ndugu rwakatare amechelewa ndege ila chama kinafanya mpango wa kukodi ndege ili afike bukoba,kauli hii ilileta maswali ,maana tayari ilishakuwa saa nane na nusu na uwanja ulishafungwa kwa shughuli za ujenzi,hapo watu walitawanyika na kuondoka,ghafla katika hali kusitaajabu rwakatare akaonekana mtaani akiwa kwenye gari ya wazi akipunga mkono na kuelekea uwanja wa uhuru  uswahilini ambako mkutano wa hadhara ulikuwa unafanyika huko,kwa mujibu wa mtu wandani kwa mashariti ya kutotajwa jina rwakatare aliwasili bukoba kwa basi toka jana na kufichwa mahala.



                     watu waliamua kuzimua na kutafuta stimu wakiwa uwanja wa ndege wakisubiri

           muda ukazidi kwenda,na watu wakazidi kunywa huku wakiimba rwakatare mjerajera original
 baada ya mambo kukolea watu wakakumbuka waliokufa arusha,wakajifunga vitambaa vyeusi
 ni full vituko uwanja wa ndege wa bukoba leo,ila rwakatare hakutokea ,baadae akaonekana mtaani
                                                       ngoma zikachezwa kumsubiri mgeni
                                                                  full mzuka

 sherejei ikabidi atangaze, jamani ndege imemuacha ila chama kinatafuta namna ya kukodi ndege
                                                            ulinzi ulikuwepo
                                                             matax dreva wa sokoni
                                 ndege ilipowasili walishuka abiria 3 rwakatare hakuwemo
 alikuwa ni abiria wa mwisho katika ndege hiyo ,rwakatare hakuwemo,watu walikata tamaa na kutawanyika
                                                watu wakiwa uwanja wa mashujaa uswahilini


                                                          rwakatare akiwa uwanja wa uhuru plat form bukoba


                                     zainabu almas akitangaza kuama cuf na kwenda chadema


                                         wananchi wakisubiri rwakatare azungumze
                                      vareliani  wa vision redio akipata maelekezo kutoka kwa sherejei
                                              mmoja wa wasemaji akiongea
                                                        akipanga cha kuongea kabla hajasimama




 alisimama rwakatare kikubwa alisema na kutoa ushuhuda kuwa mungu yupo na kila anaeamini na kumuomba atamsaidia,alizungumza mengi aliyokutana nayo katika siku 92 akiwa gerezani,lakini mwisho alisema ametunga kitabu cha maisha akiwa gerezani na anaandika kitabu cha maisha yake hivyo kinatumia gharama kuchapishwa akapitisha mnada kwa kunadi vitu, kama asali,mafuta ya kula, mifagio nk ili pesa itakayopatikana isaidiekuchapisha kitabu chake.chezeea rwakatare weweee