Friday, 26 April 2013

KALA JEREMAYA, DYNA, KITARE MASELE, H.BABA WAPANGAWISHA WAKAZI WA JIJI LA MWANZA KATIKA UKUMBI WA VILLA PARK RESORT.

Msanii wa kizazi kipya almaarufu kama Dyna akiimba leo Ijumaa hii usiku kwenye Uzinduzi wa Album ya Kala Jeremaya kwenye ukumbi wa raha Jijini Mwanza Villa Park Resort.
Msanii wa kizazi kipya Dyna akiimba nyimbo yake ya Nivute kwako kwenye ukumbi wa Villa Park.
Jukwaa lilisheheni, nyomi ..

Djz wakifanya mambo yao jukwaani

Msanii wa kizazi kipya Dyna akiimba huku mashabiki wakipagawa na nyimbo zake

Msanii wa kizazi kipya Dyna akiimba kwa hisia wimbo wake wa "Nivute kwako" usiku huu

Shabiki ilibidi apande jukwaani kumsindikiza Dyna
Jukwaa likitikiswa na Dyna
Babuuuu...Kitare Masele akaanza kupagawisha
Ilikuwa patashika Villa Park usiku huu Masele amewashika vilivyo mashabiki wake.
Nyimbo kama mbuzi kagoma kwenda na nyinginezo ndizo zilizokuwa zikimnesa Masele
Umati wa watu wangi na mashabiki wa nyimbo za Bongo flava waliitikia kwa wingi usiku huu Villa Park

Mtoto wa nyumbani ... H.Baba naye akapanda jukwaani kupagawisha vilivyo katika ukumbi wa Villa Park


Msanii H.Baba akiwa ameshilia album mpya ya Kala Jeremaya usiku huu ambayo imezindulia leo hii rasmi ikiwa na nyimbo 23 ya PASAKA.

Kala Jeremaya kama kawaida yake kutikisa jukwaa ...full mizuka ikiwapanda mashabiki wake leo hii wakati anazindua Album yake ya PASAKA yenye nyimbo kibao 23 ambayo pia amedai kuwa kuifanisha album hiyo ilimchukua muda wake mwingi wa kukaa studio na pia ikiwa ni album moja wapo ya kumjenga kimuziki hapa nchini na nje






Mashabiki wakimsikiliza Kala Jeremaya wakati akitumbuiza leo hii usiku kwenye Ukumbi wa Villa Park Resort uliopo jijini Mwanza.

Mdau Jamco (kushoto) H.Baba na Babu Masele wakiwa ndani ya kiwanja cha raha Cha Villa Park usiku huu baada ya kukutana kwa mara nyingine tena

Wadau wamekutana jukwaani

Dada mizuka ikimpanda

Wednesday, 24 April 2013

KOCHA MKUU WA TAIFA STARS, KIM POULSEN ATANGAZA KIKOSI CHA PILI CHA VIJANA CHA TIMU YA TAIFA


Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen (katikati) akizungumza na waandishi wa habari. Kulia ni Meneja wa Timu Leopold Tasso Mukebezi na (kushoto) ni Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura.

Na Boniface Wambura, TFF
Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametangaza timu ya pili ya Taifa (Young Taifa Stars) atakayoitumia kuangalia wachezaji ambao baadaye anaweza kuwajumuisha kwenye timu ya wakubwa.

Akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo (Aprili 23 mwaka huu) kabla ya kutaja kikosi hicho, Kim amesema timu hiyo ni sehemu ya Mpango wa Maendeleo wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) uliozinduliwa Aprili 4 mwaka huu ukilenga kuendeleza wachezaji.

Amesema timu hiyo inajumuisha wachezaji ambao wamepita umri wa kuchezea timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) na wakubwa ambao hawajapata fursa ya kuingia Taifa Stars, lakini atatumia Young Taifa Stars kuangalia uwezo wao.

“Timu hii ni kiungo kati ya vijana na wakubwa. Wengi wa wachezaji watakuwa vijana, lakini wakubwa wachache watapata fursa ya kuwemo ili kuangalia uwezo wao hata kama uko nyuma waliwahi kuchezea Taifa Stars. Lakini timu hii vilevile ni changamoto wa wachezaji wa Taifa Stars kuwa wapo wanaosubiri wazembee ili wachukue nafasi zao,” amesema.

Young Taifa Stars yenye wachezaji 30 itakuwa na kambi ya siku tano jijini Dar es Salaam kuanzia Mei 2 hadi 6 mwaka huu.

Wachezaji walioitwa ni Aishi Manula (Azam), Hussein Shariff (Mtibwa Sugar) na Ali Mustapha (Yanga) ambao ni makipa. Mabeki ni Kessy Hassan (Mtibwa Sugar), Kennan Ngoma (Barnsley FC, Uingereza), Himid Mao (Azam), Ismail Gambo (Azam), David Mwantika (Azam), Miraji Adam (Simba), Mohamed Hussein (Kagera Sugar), Waziri Salum (Azam), Samih Nuhu (Azam) na Emily Mgeta (Simba).

Viungo ni Haruna Chanongo (Simba), Edward Christopher (Simba), Mudathiri Yahya (Azam), William Lucian (Simba), Jonas Mkude (Simba), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Jimmy Shoji (JKT Ruvu), Abdallah Seseme (Simba), Ramadhan Singano (Simba), Farid Mussa (Azam) na Vicent Barnabas (Mtibwa Sugar).

Washambuliaji ni Hussein Javu (Mtibwa Sugar), Jerome Lambele (Ashanti United), Zahoro Pazi (JKT Ruvu), Twaha Hussein (Coastal Union), Abdallah Karihe (Azam) na Juma Luizio (Mtibwa Sugar).

TASWA FC, TASWA QUEENS KUCHEZA LEO HII JUMATANO PWANI


Kikosi cha Taswa Fc.
TIMU ya soka ya waandishi wa habari za Michezo nchini (Taswa FC) na timu ya netboli (Taswa Queens) iliyoondoka jijini jana Jumatano alfajiri kwenda Kibiti, mkoa wa Pwani kwa ajili ya mechi maalum ya kirafiki.

Kikosi cha Taswa Queens.
Mechi hiyo imepangwa kufanyika kwenye uwanja wa Samora imeandaliwa kwa ajili ya kuanzisha uhusiano wa karibu baina ya waandishi wa habari za michezo na walimu wa wilaya hiyo katika kuendeleza sekta hiyo hapa nchini.

Mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto Omary alisema kuwa mechi ya kwanza siku hiyo itakuwa kati ya Taswa Queens na kombaini ya walimu iliyopangwa kuanza saa 9.00 ambapo mechi ya pili itakuwa kati ya Taswa FC na kombaini ya walimu iliyopangwa kuanza saa 10.00 jioni.

Majuto alisema kuwa mbali ya kuanzisha uhusiano na kupromoti michezo katika wilaya hiyo, mechi hizo pia zitakuwa sehemu ya maandalizi ya Taswa FC na Taswa Queens kwa ajili ya ziara ya kimichezo mkoani Arusha na Tanga mwezi ujao.

“Maandalizi ya safari yamekamilika na tunawaomba wachezaji wazingatie muda wa kufika ili tuweze kuondoka kwa mujibu wa ratiba yetu, lengo ni kuwahi kufika na kumaliza mapema na kuendelea na ratiba nyingine kwa mujibu wa wenyeji wetu,” alisema Majuto.

Alisema kuwa timu zao zote zimejiandaa kwa ushindi katika mechi hizo ambazo zinatarajiwa kuwa na ushindani mkali kutokana na maandalizi. Taswa FC haijapoteza hata mechi moja toka kuanza kwa mwaka huu. Timu zote mbili zilitoa vipigo kwa timu ya Kiliflora ya Arusha kwa mabao 4-1 kwa upande wa soka na mabao 28-8 kwa upande wa netiboli.

Mratibu wa mechi hiyo, mwalimu Paul Nyoni amesema kuwa maandalizi yote yamekamilika na wanawasubiri kwa hamu waandishi wa habari. Nyoni alisema kuwa wamewaandaa mapokezi mazuri kwa waandishi na wanaamini mechi hizo mbili.

JACKIE APPIAH AJIACHIA KWA MWIGIZAJI WA KINAIGERIA BOBBY OBODO, KUOANA SASA...

Mcheza filamu na Staa wa Ghana, Jackie Appiah ameangukia kwenye penzi la mwigizaji wa Nigeria, bobby Obodo na sasa wanatarajia kupanga mipango ya kufunga pingu za Maisha. 

Mlimbwende huyo alikuwa kwenye kesi ya madai ya talaka kutoka kwa mumewe mienzi michache iliyopita na sasa anatarajia kula kiapo kwa mcheza filamu huyo wa Nigeria kwa mara nyingine.
jackie alifunga pingu miaka mitano iliyopita na mghana mwenzake aliyejulikana kwa majina mawili Peter agyman na ndoa hiyo kufanikiwa kufungwa na Kujaaliwa kupata mtoto wa kiume na hatimaye kutengana na sasa mwana dada huyo ameangukia kwenye penzi la mtu mwingine wa Nigeria.

Mwigizaji huyo wa Nigeria tayari ameisha jitambulisha rasmi kwa familia ya Mwanadada huyo na kupata baraka zote.



The real gist is that the two are planning a glamorous wedding ceremony.
Though no date has been set, we learnt Jackie Appiah has started putting things in order on her end.
Wishing them a happy married life in advance.


Kwa hisani ya bukobasports.com