Saturday, 18 April 2015

Zitto Ajibu Tuhuma Za Kumchongea Mengi Kwamba Alichochea Wabunge Kuiangusha Serikali ya JK


Katika gazeti la Taifa Imara la tarehe 23 Machi 2015 kulikuwa na habari yenye kichwa cha maneno ' Zitto amchongea Mengi kwa JK?' Habari hiyo ilibeba maudhui ya 'post' iliyoandikwa katika mtandao wa Mwanahalisi online.
Habari hiyo inaonyesha kuwa Mimi nilikutana na Rais kwa msaada wa watu mbalimbali na katika kikao hicho inadaiwa nilisema kuwa Mengi ndiye aliyechochea wabunge kuishughikia Serikali ya Rais Kikwete ili ianguke.
Ni vema ifahamike kuwa gazeti la Taifa Imara linamilikiwa na Bwana James Rugemalira wa kashfa ya Escrow na kuendeshwa na Bwana Prince Bagenda aliye organise press conference ya mmoja wa mawaziri waliofukuzwa kazi kwa kashfa hiyo. Vile vile chanzo cha habari hiyo ni mtandao wa mwanahalisi online ambao unaendeshwa mmiliki wa Mawio gazeti ambalo kila wiki lina habari za kutunga dhidi yangu na chama cha ACT Wazalendo.

DECEMBER BUKOBA HUWA NI HEKAHEKA , UNAIKUMBUKA HII.

 Ben Mulokozi, Ben Mulokozi, ni maneno  ya waimbaji wa malaika  band,kadri unavyoimba  na kurudia bila kujari ni mara ngapi  unapokea  noti nyekundu zisizonaidadi, matukio kama haya  hutokea mwezi wa kumi na mbili , Imekuwa ni desturi ya wahaya wengi kuja nyumbani kupumzika kuwaona ndugu na jamaa na kusherekea x -mas na mwaka mpya, hii ilikuwa ndani ya  Lina's.
 Shamila, mama wa mirindimo wa Kasibante redio akiwa na Richard .
 Mr Jamal na mkewe Mainda, nao wakivinjari ndani ya Lina's.
 Rahim Kabyemela sambamba na Ben Mulokozi.
 Justuce Rugaibula akiwa na Ben Kataruga.
 Christian Bella akifanya vitu vyake jukwaani.
 Kijana Jerry.
 Wa kicheka na camera yetu.
 Mama Adve akiwa na familia.
Ni moja ya matukio ya mwezi wa December 2014, FULL SHANGWE.

Wednesday, 15 April 2015

BALOZI KHAMIS KAGASHEKI MTEMBELEA MZEE SAMWEL RWANGISA NEW YORK MAREKANI KUMJULIA HALI YA AFYA YAKE.

 Mbunge wa jimbo la Bukoba mjini Balozi Khamis Sued Kagasheki amemtembelea Mwanasiasa mkonge katika Taifa hili la Tanzania Mzee Samwel Ntambala Rwangisa nyumbani kwake New York Marekani kumjulia hali ya afya yake,Mzee Rwangisa yuko nchini marekani kwa matibabu ya afya yake takribani miezi mitano sasa.(katika picha Kushoto ni Mzee Rwangisa, Murungi kichwabuta na Balozi Kagasheki)wakiwa nyumbani kwa mzee Rwangisa New york Marekani.
 Mzee Rwangisa akiongea na wananchi  kwa njia ya simu akiwa New York Marekani kupitia redio Kasibante 88.5 ya Mjini Bukoba, Kikubwa amewaomba wananchi kuwa wamoja na shikamano.
 Akiongea na Redio Kasibante.
 Balozi Kagasheki akiongea na Redio Kasibante akiwa New York Marekani  akimshukuru Mkuu wa wilaya  ya Bukoba  kwa namna anavyoshughulikia tatizo la chakula kwa shule za sekondari zilizofungwa, pia amelipongeza jeshi la polisi linavyoendelea na jitihada za kuhakikisha hali ya usalama kwa wananchi jimboni.
 Mh Murungi Kichwabuta (Diwani viti maalumu) akiongea na redio Kasibante akiwa New york Marekani , ameelezea maendeleo ya hali ya afya ya baba yake mzee Rwangisa, pia amewataka wanawake kuwa na mshikamano na hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
 Katikati ni binti mkubwa wa Balozi Kagasheki anaeishi Marekani Tausi Kagasheki.
Jamcobukoba.blogspot.com inakutakia afya njema mzee Rwangisa, picha hizi kwa hisani ya Bi Tausi Kagasheki kutoka Marekani.

TANGAZO LA KIFO CHA BI SHADYA ABDUL HAKIMU KICHWABUTA

Familia ya marehemu Alhaj Hussein Omary Kichwabuta wa Ishozi Bukoba wanasikitika kutangaza kifo cha marehemu Shadya Abdul Hakimu Kichwabuta kilichotokea leo 15-4-2015 katika hospital ya rufaa Kagera, mazishi yatafanyika leo 15-4-2015 Ishozi Bukoba saa 10.00 jioni, habari ziwafikie ndugu, jamaa na marafiki popote walipo. INNALAAH WAINALILAAH LYAJIHUN.

Monday, 13 April 2015

ALLAN MUGISHA ASHEREKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA, WALKGARD HOTEL ILIKUWA NI SHIDAAAA.

 Kushoto ni Kijana mpole  kwa muonekano wa nje , lakini mtu makini akidhamilia kitu Bw Allan Mugisha akifurahi namna mwanadada huyo pichani alivyokuwa akiikata keki,Ilikuwa ni bonge la party iliyofanyika katika moja ya hotel kubwa Katika Mkoa wa Kagera Walkgard hotel iliyoko katika kilima cha Kashura barabara iendayo Maruku,Kikubwa ni mpangilio na shughuli ilivyopangiliwa ni kimaanisha, mkao, vinywaji na chakula, nikirudi upande wa wa eneo ilipofanyika shughuli kwa pembeni kuna bonge la swimming pool na kiupepo kizuri kutoka ziwa victoria, Kwa upande wa waalikwa namna walivyotokelezea, walipendeza sana, Hongera sana Allan Mugisha kwa kutimiza miaka kadhaa.
 Muonekano wa eneo la wageni waalikwa.
 Ni Kijana Mwanawasu mtaalamu wa kuchoma nyama akiendelea na maandalizi.
 Kwa upande wa vinywaji unaona mwenyewe, kwa wale waliokuwa na speed walilala mapema sana , hata tukio la kukata keki hawakuliona, maana kijana alijipanga, milioni kadhaa zilitumika kwenye maandalizi.
 Waalikwa.
 Rehema Ridhiwan.
 Jeni MTK akiwa na rafiki yake.
 Mc Jerry akiendesha ratiba.
 Mchanganyiko wa waalikwa ulikuwa poa sana.
 Mitandao ni shidaaa, kila mtu busy.
 Sima Isaya na msanii kamdingi furani walikuwepo kuwapa waalikwa burudani.
 Huyu alimua atoke kihivi.
 Staili ya Mtoto alie zaliwa  namna alivyoingia ukumbini, ilikuwa ghafla bila taarifa ndani ya nyumba, ilikuwa ya aina yake.
 Ni kijana Paul Manyama akionyesha uwezo wake wa kusakata rumba.
 Akaingia kati binti mwenye mvuto  Rehema Ridhiwani nae akaweka mambo.
 Mtoto aliezaliwa muda wote ni furaha.
 Bw na Bi Adamu Kagasheki.
 Ilikuwa shidaaaa.
 Admin wa Group la mia mia Oscar(kushoto) mratibu wa shughuli nzima.
 Neema na mdogo wake katika pozz.
 Dj Slay ndio alikuwa akipangilia program ya muziki.
Hongera sana Allan Mugisha.