Thursday 27 June 2019

NI MJUBULO WA SHAMILA MKUDE , JUMAPILI 30/6/2019,SI YA KUKOSA HII,LINAS


RWEGASIRA CUP YAANZA , TIMU NANE KUSHIRIKI, MDHAMINI ASEMA NI KUMUENZI MZEE RWEGASIRA.




Ni kinyanganyilo cha timu nane  zinachuana katika mashindano ya Rwegasila cup yanayofanyika katika kata ya Kitendagulo uwanja wa Chuo cha afya Kagemu, Manispaa ya Bukoba.Mdhamini wa mashindano hayo Bw Edward Rwegasila amesema ameamua kuanzisha mashindano hayo kwa ajili ya kumuenzi marehemu baba yake Mzee Emanuel Rwegasila ambae katika uai wake alikuwa akipenda michezo na vijana wengi kijijini kwake walikuwa wakicheza mpira katika uwanja wa nyumba yake, na mara nyingi alikuwa akiwapa pipi na kuangali Tv nyumbani kwake,Bw Edward amesema kwa kutambua hilo ndio maana ameamua kuanzisha mashindano hayo ,ili vijana wafurahi na waweze kuendeleza vipaji vyao, Bw Edward Rwegasira anafadhili mashindano hayo kwa kughalamikia gharama zote za uendeshaji, ikiwa ni pamoja na kununua jezi kwa Timu zote, posho za waamuzi ,usafiri wa timu, matibabu, maji na kutoa zawadi kwa mshindi wa kwana, wa pili na wa tatu, Timu zinazoshiriki ni Rwegasila Fc, Mafumbo FC, Kibeta FC, Kagemu Fc, Busimbe Fc, Bukoba Manispaa FC, Bunena FC na Ijuganyondo FC. katika picha Mgeni rasmi , Mwenyekiti wa ccm Bukoba Manispaa Muganyizi Zachwa akikagua timu ,Rwegasila FC na Mafumbo FC.





Bw Richard Rwegasira akisalimiana na mgeni Rasmi.



Wachezaji wakiwasiri uwanjani.









Makamu Mwenyekiti wa Chama cha mpira Mkoa wa Kagera Bw Kazinja.







Mgeni rasmi akikabidhi Jezi kwa Timu zote zinazoshiriki mashindano .



Mgeni rasmi akikagua timu.



Rwegasira Fc




Mafumbo Fc




Kocha wa Rwegasira Fc