Saturday, 19 October 2013

MZEE PIUS NGEZE ASHEREKEA NA KUMSHUKURU MUNGU KWA KUTIMIZA MIAKA SABINI,BABA ASKOFU KILAINI AONGOZA MISA

 Mzee pius Ngeze alietimiza umri wa miaka 70 akiwa na Baba Askofu Methodius Kilaini
                                     kanisa kuu la katoriki la bukoba ilipofanyika misa ya shukrani
                                                             picha ya familia ya mzee ngeze

 mzee pius ngeze  akiwa na mke wake na wanae,mzee pius ngeze ambae amekuwa kiongozi wa muda mrefu katika nchi ya tanzania katika nyadhifa mbalimbali,mzee ngeze amewahi kwa mbunge mstaafu wa willaya ya ngara,mwenyekiti msaafu wa ccm mkoa wa kagera zaidi ya miaka 20, mjumbe wa halmashauri kuu ya ccm mstaafu, mwenyekiti wa bodi mbalimbali  za mashirika na taasisi,baada ya kustaafu ameendelea na shughuli zake binafsi.
                                                          watoto wa mzee ngeze
                                                familia wakiwa katika ibada
                      bwana pius ngeze na mke wake mama ngeze wakiwa wanatoa shukrani zao
                                                                 wakati wa matoleo
                     mama ngeze akiwa na mzee mgeze katika picha ya pamoja baada ya misa ya shukrani
                                  picha ya pamoja wanafamilia ya mzee pius ngeze na baba askofu kilaini

Friday, 18 October 2013

MISS UNIVERSE TANZANIA AKABIDHIWA BENDERA LEO


Mrembo wa Miss Universe Tanzania 2013 Betty Boniface Omara amekabidhiwa bendera leo na waziri wa mali asili na utalii mheshimiwa Kagasheki.
Zoezi hili limefanyika katika ukumbi wa mkutano wa wizara hiyo tayari kwa safari yake ya kwenda kwenye mashindano ya Miss Universe yatakayofanyika Moscow nchini Urusi mapema mwezi Novemba.
Akimkabidhi bendera huku akimpongeza waziri Kagasheki pia amemtakia mafanikio mema huko aendako.
Betty pia aliwaahidi watanzania kuwa mbali na kurudi na ushindi lakini pia ataenda kuitangazia dunia kuacha kutumia nakshi(Mapambo) yanayotumia pembe za ndovu ili kumaliza tatizo la ujangili nchini.
Zoezi la kukabidhiwa bendera lilifanyika likishuhudiwa na Mkurugenzi wa Kitaifa Miss Universe Tanzania Maria Sarungi Tsehai.
Mashindano ya Miss Universe Tanzania 2013 yamedhaminiwa na hifadhi ya Taifa Tanapa na Mrembo Betty Boniface ameshaanza kutangaza hifadhi hizi kwa njia mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi.

RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE AZINDUA RASMI MKOA WA NJOMBE LEO


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibofya kitufe huku  wazee wa Njombe wakirusha njiwa kuashiria kuzinduliwa rasmi mkoa wa Njombe leo Oktoba 18, 2013 katika Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa Maisha Bora  kwa Watanzania hajawezi kuja kwa watu kushinda wanacheza mchezo wa pool badala ya kujihangaisha kwa kufanya kazi na shughuli nyingine za kujiingizia mapato.
Aidha, Rais Kikwete ameahidi kuwa Serikali yake itakomesha haraka iwezekanavyo kero ya wananchi wa sehemu za Mkoa wa Njombe kulazimika kupanda mitini ili kupata mawasiliano ya simu za mkononi.
Rais Kikwete amayesema hayo leo, Ijumaa, Oktoba 18, 2013, wakati alipohutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Wanginyi, Kata ya Lupembe, Wilaya ya Njombe katika Mkoa Mpya wa Njombe kwenye siku yake ya kwanza katika ziara yake ya siku saba kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo katika Mkoa huo.
Akizungumza na wakazi wa Kijiji hicho na vijiji vya jirani, Rais Kikwete amezungumzia dhana nzima ya Maisha Bora kwa Watanzania akisisitiza kuwa maendeleo na Maisha Bora kwa Kila Mtanzania hajawezi kupatikana kwa watu kushinda wanacheza mchezo wa pool mchana kucha.
“Ndugu zangu, nimepata kusema huko nyuma na nataka kurudia tena kuwa Maisha Bora kwa Kila Mtanzania yanawezekana kwa watu kujituma na kuchapa kazi na siyo kwa watu kushinda kwenye meza za pool wakipiga kale kampira huko wakiilaumu Serikali na kuulizana ‘Maisha Bora yako wapi?’”
Ameongeza Rais Kikwete: “Inawezekana kweli Maisha Bora yakaja kwa mtu anayeshinda anagonga mpira wa pool kwenye meza? Ni kwa kufanya kazi kwa bidii na shughuli nyingine za kutuingizia kipato ndipo maisha yetu yatakapokuwa bora.”
Kuhusu hali ya mawasiliano ya simu Mkoani Njombe, Rais Kikwete, baada ya kuwa ameambiwa kuwa katika baadhi ya sehemu za Mkoa huo, watu wanalazimika kupanda juu ya miti ili kupata mawasiliano, alisema kuwa Serikali yake itakomesha haraka kero hiyo.
“Ni ajabu na aibu kabisa kwamba watu wanalazimika kupanda miti ili kupata mawasiliano….Hii ni hatari … kwa sababu mtu anaweza kuanguka na kuvunja viungo…mtu anaweza kuvunja kiuno,” alisema Rais Kikwete huko watu wakiangua kicheko. 
“Tutahakikisha kuwa watu hawavunjiki viungo kwa sababu ya kupiga ama kupokea simu za ndugu zao,” Rais Kikwete amewahakikishia wana-Njombe.
Katika kufafanua azma hiyo ya Serikali kumaliza kero hiyo, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mheshimiwa Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa Serikali italimaliza tatizo la mawasiliano katika Mkoa wa Njombe kwa awamu mbili.
Alisema kuwa katika awamu ya kwanza, kiasi cha sh milioni 260 zimetengwa kwa ajili ya kuboresha mawasiliano katika vijiji 25 vya Jimbo la Uchaguzi la Njombe Kaskazini na kuwa kazi hiyo itakuwa imekamilika ifikapo Machi, mwakani, 2014. “Tunataka watu waache kupanda miti kwa kutafuta mawasiliano ya simu tu.”
Amesema kuwa katika awamu ya pili, kiasi cha sh bilioni 1.552 zitatumika kutoka Mfuko wa Mawasiliano Vijijini kwa ajili ya kuboresha mawasiliano ya simu katika Mkoa mzima wa Njombe.
Amesema kuwa kazi ya kuboresha mawasiliano katika awamu hiyo ya pili, itakamilika ifikapo Agosti, mwakani, 2014.
Kuhusu matumizi ya simu zenyewe, Mheshimiwa Mbarawa amewataka Watanzania kuzitumia simu hizo za mkononi vizuri kwa mawasiliano ya maana na yasiyokuwa na ovyo ikiwa ni pamoja na kutukana watu. “Tuzitumie simu zetu vizuri kwa mawasiliano mazuri na ya maana na siyo kutumia simu kujenga na kusambaza fitina na majungu ama kushiriki matusi dhidi ya watu wengine.”
Baadaye jioni, Rais Kikwete alikuwa anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika sherehe za Uzinduzi Rasmi wa Mkoa wa Njombe kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe.
 

Thursday, 17 October 2013

DAR LIVE ILIVYOZIZIMA KWA BURUDANI ZA EID JANA



Ommy Dimpoz akikamua ndani ya Dar Live.
...Mashabiki wakipagawa na Dimpoz.
Joh Makini 'Mwamba wa Kaskazini' akilishambulia jukwaa la Dar Live. Wanenguaji wa Twanga wakionesha manjonjo. Mwamba wa Kigamboni, Bahati Chaz ‘Mr B’ akishusha mistari ya hip hop Dar Live. Masai wa Kigoma akifanya makamuzi.
Baadhi ya mashabiki baada ya kupandisha mizuka.
Twanga wakikamua stejini.Mwanamuziki wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta International’ Rama Pentagon akikamua na bendi yake.
Mtaalam wa mazingaombwe, Profesa Calabash akiichoma moto fulana.
...Akiirudisha kama ilivyokuwa awali.
Msaidizi wa Profesa Kalabash akionesha glasi kabla ya kuizamisha kichwani kwa mtoto aliye kulia. ...Glasi ikiwa kichwani. ...Glasi imezama kichwani. ...Mtoto akishangaa baada ya glasi kuzama kichwani. Watoto wakifurahia michezo ndani ya Dar Live. ...Watoto wakijiachia kwenye bembea. ...Hawa wakiserereka. Bembea la mzani. Watotio wakiingia kwenye ndege ya Dar Live.

Wednesday, 16 October 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI SWALA YA EID EL HAJ MSIKITI WA ANWAAR MSASANI

 Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu baada ya kushiriki nao katika Swala ya Sikukuu ya Idd El Haj, iliyofanyika katika Msikiti wa Anwaar uliopo Msasani, jijini Dar es Salaam leo. Picha zote na Ofisi ya Makamu wa Rais
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na waumini kushiriki Swala ya Sikukuu ya Idd El Haj na Waumini wa dini ya Kiislam katika Msikiti wa Anwaar, uliopo Msasani jijini Dar es Salaam, leo asubuhi. 
 Sehemu ya Waumini wa dini ya Kiislamu waliohudhuria katika swala ya Sikukuu ya Idd El Haj na Mhe. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, leo asubuhi katika Msikiti wa Anwaar, uliopo Msasani jijini Dar es Salaam.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na waumini kushiriki Swala ya Sikukuu ya Idd El Haj na Waumini wa dini ya Kiislam katika Msikiti wa Anwaar, uliopo Msasani jijini Dar es Salaam, leo asubuhi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. SHukuru Kawambwa, wakati akiondoka katika Msikiti wa Anwaar, uliopo Msasani jijini Dar es Salaam, baada ya kushiriki Swala ya Sikukuu ya Idd El Haj na waumini wa dini ya kiislam leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislam, wakati akiondoka katika Msikiti wa Anwaar, uliopo Msasani jijini Dar es Salaam, baada ya kushiriki Swala ya Sikukuu ya Idd El Haj na waumini hao leo.

CCM YAMSHUKIA ZITTO KABWE


*Ni kuhusu taarifa yake kuhusu ukaguzi wa mahesabu ya vyama vya siasa
*Nape asema Chadema huenda ndiyo inaongoza kwa hesabu zake kutokaguliwa
*Asema CCM imekuwa ikitii kukaguliwa hata kabla ya vyama vingi nchini
Ndugu Nape, akizungumza leo
NA MWANDISHI WETU
SIKU moja baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu a Serikali (PAC), Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe, kutoa taarifa zinazoshutumu kuwa vyama vya siasa nchini havijafanyiwa ukaguzi wa mahesabu kwa muda mrefu, CCM imeibuka na kuitwisha Chadema tuhuma hizo.

Imesema yenyewe (CCM) imekuwa ikiitika mwito wa sheria hiyo na kwamba hesabu zake zimekuwa zikikaguliwa kwa miaka mingi sasa, hata kabla ya kuanzishwa mfumo wa vyama vingi vya siasa hapa nchini.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye amesema, ni sahihi kwa hesabu za vyama vya siasa kukagukiwa kwani ni kwa mujibu wa sheria, na ndiyo sababu CCM imekua ikitekeleza sheria hiyo kwa miaka mingi hata kabla ya kuanzisha mfumo wa vyama vingi vya siasa.

Nape alisema, badala yake chama kinachopaswa kutiliwa shaka kuhusu ukiukaji wa sheria hiyo, ni Chadema, chama ambacho alidai kimekuwa na tabia ya kufanya mambo mengi kinyume cha sheria
kwa kisingizio cha mwavuli wa siasa.

"Chama Cha Mapinduzi kimekuwa kikiitekeleza sheria hii vizuri. Kwa mfano hesabu za CCM zilikaguliwa na wakaguzi wa nje TAC (Tanzania Audit Corporation) kuanzia mwaka wa Fedha 1977/1978 hadi mwaka 2002/2003. Kuanzia mwaka 2003/2004 hadi 2010/2011 tulikaguliwa na TAC- Associates, shirika hili linatokana na Tanzania Audit Corporation lililobinafisishwa", alisema Nape.

Alisema, 29/01/2013 CCM iliandika barua yenye kumbukumbu CMM/F. 20/80/89 kuwasilisha rasimu ya hesabu za mwaka wa fedha wa 2011/2012 ili Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) aipangie mkaguzi.

"Kufuatia barua hiyo, CAG alitupangia TAC-Associates kukagua hesabu hizo za mwaka 2011/2012. 


Kwa kawaida muda wa wakaguzi ni miaka mitatu hivyo TAC- Associates watakua wakaguzi wetu mpaka mwaka wa fedha wa 2013/2014, baada ya hapo CAG anaweza kuteua wakaguzi wengine", alisema Nape.

Nape alisema, hesabu za CCM zilizokaguliwa na wakaguzi wa nje TAC- Associates mwaka wa fedha 2009/2010 na 2010/2011 zilikwishawasilishwa kwa CAG na kwamba hesabu za mwaka wa fedha 2011/2012 bado ziko kwa wakaguzi wa nje, wakishakamilisha nazo zitawasilishwa kwenye vikao vya Chama na hatimaye kwa CAG.

Alifafanua kwamba,  hesabu hizo zikikaguliwa kwa mujibu wa utaratibu, anapelekewa CAG ambaye ndiye anazipeleka kwa Msajili wa vyama vya siasa.

Nape alisema kutokana na maelezo haya CCM haihusiki na agizo la PAC na kama kamati ya bunge ikitaka CCM ipo tayari kwenda kukutana kamati hiyo, huku CCM ikiwa na mahesabu yake yaliyokaguliwa.

"Mwito wetu kwa Zitto aanze kwa kutoa boriti kwenye jicho lake ndipo aone kibanzi kwenye jicho la mwenzake. Tunaamini kwa sababu mbalimbali zikiwemo za kuwa na vyanzo vya fedha visivyo visafi na tabia iliyokubuhu ya kupenda kukiuka kila sheria nchini wakidhani ndio staili ya kujenga chama chao, si ajabu kuwa Chadema wanaweza kuwa hawajakaguliwa kwa miaka yote hiyo. Zitto kama Naibu Katibu Mkuu wa Chama chake anapaswa kuwajibika kwa hili, yeye na Chama chake", alisema Nape na kuongeza;

"Wote tunakumbuka kelele zilizopo mtaani juu ya matumizi mabaya ya ruzuku zinazoelekezwa na Chadema na viongozi wake kutoka kwa wanachama wao, hivyo si ajabu wakawa wanakiuka sheria hii na ndio chanzo cha kelele hizo za wanachama wao".

Nape alitaka ikibainika kuwa ni kweli Chadema wamekiuka sheria hiyo muhimu, basi viongozi wa vyama husika wawajibike kwa kuwa si busara kuwa na viongozi wa kisiasa walikubuhu kwa kuvunja sheria za nchi na kujificha chiniya mwamvuli wa siasa.


"Uvunjaji wa sheria hii kwa wenzetu sio kwa bahati mbaya kwani wamezoea kutoheshimu sheria za nchi mpaka kufikia mahali pa kutangaza hadharani kuwa wanatamani nchi isitawalike. Ni muhimu kujenga utamaduni", alisema Nape.

WAUMINI WA DINI YA KIISLAM WASHEREKEA EID,SHEKHE KICHWABUTA AWAASA KUPENDANA

 shekhe haruna kichwabuta amewataka waumini wa kislamu kupendana na kuwa wamoja,pia amewasihi wajitahidi kusomesha watoto
                                                                         bw chakindo akiwa katika ibada
 mwenyekiti wa bakwata wilaya ya bukoba alhaji kagire akitoa mkono wa eid
               waumini wakisikiliza khotuba leo msikiti wa ijumaa bukoba
                                                  shekhe kakwekwe akiongea na waumini
                                                                    shekhe Haruna kichwabuta akiwa na jamco
                                                            bwana bushira baada ya sawla ya eid
                                         Waumini wakitoka kwenye swala ya eid msikiti wa ijumaa