Thursday, 4 September 2014

NYUMBA ZA ASKARI NA KITUO CHA POLISI VYABOMOLEWA KARAGWE KAGERA, HUKU FFU WAKISIMAMIA ZOEZI...NYUKI WA AJABU WATIBUA ZOEZI


Ofisi ya mkuu wa jeshi la polisi (OCD) pamoja na nyumba za makazi ya askari polisi vimebomolewa na kampuni inayojenga barabara hiyo China Henan International Group (CHICO) ndiyo iliyoendesha zoezi hilo la bomoabomoa chini ya usimamizi wa F.F.U baada ya maaskari polisi kudaiwa kugoma kuhama.

Katika hali ya kushangaza na iliyowaacha vinywa wazi wananchi, askari wa kutuliza ghasia F.F.U wamesimamia zoezi la kubomoa kituo cha polisi cha wilaya pamoja na nyumba wanazoishi askari polisi wilaya ya Karagwe mkoani Kagera kupisha ujenzi wa barabara yenye urefu wa km. 59.1 toka Kyaka wilayani Missenyi hadi Bugene wilayani Karagwe kwa kiwango cha lami.

Ni tukio lililovuta umakini wa watu wengi huku minong'ono ikitawala ya ukosoaji wa kauli ya polisi "Utii wa sheria bila shuruti", wakihoji maana yake kwani nao (polisi) wamekaidi kutii sheria hadi kuletewa F.F.U kuwashughulikia endapo wangejaribu kuleta fujo.
Meneja wa TANROADS mkoa wa Kagera John Kalupare alipopigiwa simu kuelezea tukio hilo amesema yupo safarini Dar es Salaam na asingeweza kuzungumzia suala hilo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoa wa Kagera (RPC) Henry Mwaibambe alipopigiwa simu juu ya tatizo hilo, simu yake imeita bila kupokelewa.
Mmoja wa maofisa wa TANROADS aliyekuwa anasimamia zoezi hilo ambaye hakupenda jina lake litajwe, amesema kuwa wao wanaonesha mipaka ya barabara na polisi wanabomoa nyumba zao.

Sisi TANROADS tunaonesha mipaka ya barabara na polisi wanabomoa nyumba zao na kituo chao hivyo waulize wao kwanini ubomoaji unafanywa chini ya ulinzi mkali amesema.

Hata hivyo zoezi hilo limeingiwa na dosari baada ya kundi la nyuki kutokea na kuwashambulia wabomoaji, maaskari na mashuhuda wa tukio hilo huku dereva akilazimishwa na wachina kuendelea na ubomoaji licha ya kung'atwa na nyuki hao.
Ni tukio linaloshangaza na kuitia doa serikali kwa jeshi la polisi lenye dhamana ya kulinda usalama na raia ambalo daima huhubiria raia utii wa sheria bila shuruti sasa linaenda kinyume hadi kuletewa F.F.U kulisimamia.

Mkuu wa Jeshi la Polisi wilaya Karagwe hakupatikana kuzungumzia sakata hilo ambapo inadaiwa kuwa bomoabomoa hiyo itaigharimu halmashauri hiyo baadhi ya ofisi zitakazobomolewa ikiwemo ofisi za wabunge wa majimbo ya Karagwe na Kyerwa.
Chanzo: Malunde1 Blog

RAIS KIKWETE AKUTANA NA BIBI YAKE RAIS OBAMA WA MAREKANI,JIJINI NAIROBI



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Bibi yake Rais wa Marekani,Mh. Barack Obama,Mama Sarah Obama walipokutana Nairobi.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA TAREHE O5.O9.2O14

Wednesday, 3 September 2014

MWANAAFA MWINZAGO,STAR WA TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT) 2014 AWA KIVUTIO MITAA YA KARIAKOO.


Mshindi wa Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 Mwanaafa Mwinzago (Katikati) akisindikizwa na Matron pamoja na Mfanyakazi wa TMT huku akilindwa na Mabaunsa wakati alipopelekwa Katika Mitaa ya Kariakoo kwa ajili ya kununua zawadi za Wazazi wake.
Mfanyakazi wa TMT, Happy Ngatunga (Kushoto) akitoa maelekezo kwa Mabaunsa na Mshindi wa TMT aliyejinyakulia Kitita Cha Shilingi milioni 50 katika fainali ya Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Mlimani City Mwanaafa Mwinzago wakati walipokuwa katika matembezi Kariakoo.
Baadhi ya wafanyabiashara wa Kariakoo wakimpungia Mikono kama ishara ya kumpongeza kwa kuibuka mshindi wa fainali ya Tanzania Movie Talents (TMT) Star wa TMT 2014 kutoka Mtwara, Mwanaafa Mwinzago Wakati alipokatiza kwenye mitaa ya Kariakoo pindi alipokwenda kununua zawadi kwaajili ya wazazi wake
Star Wa TMT 2014, Mwanaafa Mwinzago (katikati) akiwa na furaha mara baada ya kupongezwa na mashabiki waliopata nafasi ya Kumsalimia na kumpongeza wakati akikatiza mitaa ya Kariakoo pindi alipokwenda kununua Zawadi kwaajili ya Wazazi wake
Wanafunzi wa Shule ya Msingi wakimpongeza Star Wa TMT 2014, Mwanaafa Mwinzago kwa kuweza kuibuka mshindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 kwa kuwabwaga mwenzake 9 na kuondoka na Kitita Cha Shilingi Milioni 50 za kitanzania wakati walipomuona katika moja ya mitaa ya Kariakoo wakati Star Huyo wa TMT 2014 alipokwenda Kununua Zawadi kwaajili ya kuwapatia wazazi wake ikiwa kama ishara ya Upendo na shukrani kwao.
Matron wa Kambi ya TMT 2014, Kemmy akichagua baadhi ya vitenge kwa Niaba ya Star Wa TMT 2014 Mwanaafa Mwinzago wakati alipopelekwa Kariakoo kwaajili ya Kununua Vitenge kama zawadi kwa wazazi wake.

Tuesday, 2 September 2014

NI BAADA YA MAMBO KUNOGA SIKU YA KUVUNJA KAMATI YA SEND OFF YA LYDIA PROTAS BUSIMBE KITENDAGURO

 Mama huyu baada ya mzuka kumpanda alimwaga radhi kwa kuonyesha furaha yake na kukubari kile  kilichoandaliwa na Familia ya marehemu  Mzee Protas na Bi Bertha Peter wa Busimbe kwa ajiri ya kuwashukuru wajumbe walioandaa Send off ya kumuaga Bi  Lyidia Protas iliyofanyika siku ya  30-8-2014 katika ukumbi wa Lina's.
 Majirani
 Wajumbe wa kamati
 Nyama choma
 Bi Lydia akisalimia wajumbe mbalimbali na kuwapa mkono.
 Wageni kutoka ukweni kwa mme walialikwa pia
 Bw Victor nae alialikwa ukweni
 Watu wakaserebuka kwa raha zao
 Bw Joel nae akipata nyama choma
 Vinywaji vya kila aina vilikuwepo na kalinyaaa ilikuwepo.
 Mama Matungwa akiwa na Jamco wakifurahia kitu
 Watu kadri muda ulivyokwenda waliwaalika na wengine walio majumbani waje
 Ukafika wakati wa msosi
 Hii kweli ilikuwa vunja kamati ya aina yake
 Vunja kamati
Cheza ngoma
 Kwaito vunja kamati hiyooo
 Kwa raha zao
 Hupo hapooo
 Kila staili katika vunja kamati
 Na huyu nae akatokelezea ki hivi vunja kamati
Hakika watu walicheza ngoma,Vunja kamati ya aina yake.