Friday, 27 February 2015

MNEC WA BUKOBA VIJIJINI NAZIR KARAMAGI ATOA VIFAA VYA MICHEZO NA VIZIBAO KWA WAENDESHA PIKIPIKI KUIMARISHA CHAMA.

 Mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi anaewakilisha wilaya ya Bukoba vijijini Naziri Karamagi anaendelea na ziara ya kuimarisha chama na hasa kuwawezesha vijana na kuwapa moyo katika shughuli zao na kuwawezesha kupata vifaa vya michezo  Jezi , Mipira na vizibao kwa vijana wanaofanya biashara ya kuendesha pikipiki,Mnec Karamagi akiongelea kuhusu michezo amesema vijana wanayohaki ya kupata vifaa vya michezo na kuonekana katika muonekano nadhifu kama wachezaji wa timu kubwa nchini na nje ya nchi,kwa upande wa waendesha pikipiki amesema  wanapokuwa katika sare maalumu wataweza kutambuana vizuri na  kuonekana na kutambulika kwa  wateja au abiria wanaotumia  pikipiki zao. Mnec Karamangi yupo kwenye ziara ya jimbo zima la Bukoba vijijini,katika  habari hii ametembelea maeneo ya Kaibanja, Katoro, Kyamulaile, Ruhunga na Butelankunzi.
 Katibu wa ccm Bukoba vijijini Mwishehe Maurid Acheni akiongea na wananchi katika  kijiji cha Kaibanja, kueleza na kumshukuru Mnec kwa jitihada za kusaidia vijana.
 Mh Karamagi akiwa na mwenyekiti wa halmashauri ya Bukoba vijijini Mh Kapteni Mstaafu Kateme.
 Mnec  akiongea na vijana.
 Mh Mnec akikabidhi vifaa vya michezo kwa timu za vijana Bukoba vijijini.
 Mh Mnec Karamagi akiwa na Katibu wa uvccm Bukoba vijijini.
 Vijana waendesha pikipiki wakiwa wameshakabidhiwa vizibao vyao.
 Waendesha pikipiki wakimsikiliza Mnec.
 Msaidizi wa Mnec Bi Georgia Kalikawe akitabasamu kwa maana ya kufurahia zoezi  linavyoendelea.
 Mnec akikabidhi vifaa.
 Pande za Katoro.

 Waitu kasinge,ogendelele kubaooo,ta karamagi. Ni maneno ya wananchi yalisikika.
Mh Karamagi anaendelea na ziara katika maeneo mbalimbali Bukoba vijijini.